Hoteli ya NASHERA imejiharibia?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kama ni kweli kikundi cha majambazi/wezi kiliweza kuingia kwenye hoteli yenye hadhi kubwa kama Nashera na kuweza kumuibia Naibu Waziri maswali mengi yameachwa juu ya hoteli hiyo. Maelezo yote ambayo yametolewa hadi hivi sasa yanaionesha hoteli kwenye mwanga mbaya zaidi kuliko hata Malima. Think about it. Nadhani Hoteli itabidi ijisafishe tu kwa kueleza vya ukweli kwani watu wengine mashuhuri wanaweza kuhofia sana kwenda hapo sasa...

Lakini pia inaonekana hoteli haina SOP za kuonesha wafanyakazi wanatakiwa washughulikie vipi matatizo ya wateja. Inawezekana Malima kaenda kuripoti wizi kwenye front desk (kitu ambacho pia kinashangaza kwani ningeassume angempigia moja kwa moja meneja wa hoteli) na wale vijana wa FD walipopiga simu kwa meneja wakati huo huo waka sms marafiki zao "aisee Malima kachapwa hapa". Maana nasikia taarifa za Malima kuibiwa zilikuwa zimeenea kwa watu wengi kabla hazijaandikwa magazetini for at least 24 hours.

Je, wafanyakazi wanapotoa taarifa za ndani kama hizo yawezekana ni kwa sababu hawajali ajira zao au hata taswira ya hoteli yao? au hawana hisia kuwa ni "hoteli yao"?
 
Mkuu, hotel waseme nini tena wakati walishajitahidi kutoa issue mapema, ......mweupe mrefu.....

Sasa Kama mukulu ndanda Kosovo, I mean mzee manywele ameshasema wanyamaze, si unajua tena, walalaji wa hotel hiyo watakuwa walewale....

Soma Alama za issue yenyewe mkuu
 
wenye hotel wangeelza ukweli ingeliwasaidia sana otherwise imekula kwao.Picha za ndani na madirisha zinaonyesha hoteli yenyewe bado ya kishamba sana.
 
Hii nchi inaendeshwa hovyo hovyo kiasi kwamba wana siasa wanakuwa na nguvu kuliko biashara. Najua wamiliki wa hotel wanalazimika kuwa wapole kwakuwa hata eneo la hotel walipora ardhi ya jeshi la magereza na chuo cha LITI. Mi kama ukimwaga mboga tunamwaga ugali. But mwisho wa siku watu wasio na hatia, walalahoi wanaadhibiwa na kuteswa kucover uovu wa wana siasa na zinaa zao
 
Habari zilishavuja,na ukweli unaeleweka kuwa mhusika kachezewa maujanja na mpenzi wake wa sekunde mbili.....ila kwa vile hotel na uongozi wao wamekubali habari halisi igeuzwe kuwa skendo lingine wamejishusha hata kibiashara
 
Mkuu, hotel waseme nini tena wakati walishajitahidi kutoa issue mapema, ......mweupe mrefu.....

Sasa Kama mukulu ndanda Kosovo, I mean mzee manywele ameshasema wanyamaze, si unajua tena, walalaji wa hotel hiyo watakuwa walewale....

Soma Alama za issue yenyewe mkuu

Mamvi anahusikaje hapa?Tujuze

Sioni haja ya wao kujisafisha kwa sasa coz nao wamejiharibia..Hivi kwanini isiwepo sheria ambayo itakataza watu kuingia na silaha za moto kwenye nyumba za wageni?

iwe inakabidhiwa kituo cha karibu cha polisi..

Wakijisafisha watasemaje?
 
Kitu ya Mamvi ile mkuu!!
Mamvi anahusikaje hapa?Tujuze

Sioni haja ya wao kujisafisha kwa sasa coz nao wamejiharibia..Hivi kwanini isiwepo sheria ambayo itakataza watu kuingia na silaha za moto kwenye nyumba za wageni?

iwe inakabidhiwa kituo cha karibu cha polisi..

Wakijisafisha watasemaje?
 
Na madhara mabaya ya huu mchezo wao wa kijinga ''yataishi na kuzaana'' kwa muda mrefu. Fikiria watu kama police wa ngazi za chini wooote wanajua hili dili halfu wanamwona mkuu wao anaongopa mchana kweupeee, wao watafanya nini? Ni kumdharau na hata nidhamu kushuka..
 
Mamvi anahusikaje hapa?Tujuze

Sioni haja ya wao kujisafisha kwa sasa coz nao wamejiharibia..Hivi kwanini isiwepo sheria ambayo itakataza watu kuingia na silaha za moto kwenye nyumba za wageni?

iwe inakabidhiwa kituo cha karibu cha polisi..

Wakijisafisha watasemaje?

Maana ya mtu kuwa na silaha ya kujilinda mwenyewe itakuwa hipi iwapo atakabidhi kituo cha polisi?
 
Uongozi wa hoteli bila shaka utakuwa umeshinikizwa kukubali kuharibu jina la hoteli yao kwa gharama ya kumlinda Malima.

Sijui kama watakuwa wametafakari kwa kina madhara ya ''kukubali'' kuwa hotel yao haina ulinzi hadi vibaka kujifunza kuiba.
 
Mkuu MwanaKijiji,
Cha kusikitisha zaidi ni jinsi Jeshi letu la Polisi lilivyokubali kutumiwa vibaya kwa kuamrishwa kuwachukuwa Mahabusu ambao hawana mashtaka yoyote na kuwabambikizia hii kesi. Inauma sana lakini ndipo tulipofika kwamba vyombo vya dola vipo tayari kutumiwa kuzima michezo michafu inayochezwa na watawala wetu mahotelini! Wanachosahau ni kwamba tunapishana nao kwenye madisco na mitaa ya Machangudoa!
 
Nashera is a victim wa umalaya wa wanasiasa wanaotumia nguvu na nafasi zao kwa nafsi zao

imeshikwa pabaya, lakini kwasbabu most of their business ni wekshop na transit, na kwasbabu watanzania huwa hatujui kufuatilia profile ya chochote zaidi ya kusikiliza unrealistic matangazo, basi hii haitawasumbua sana... ni kidogo tu

ILA JAMAA AKOME KUVUTA MILUPO NA KUFAKAMIA NYONYO ZAO

I HOPE HAKULIWA NDOGO, MAANA NI BORA WAKUIBIE KILA KITU KULIKO KUKULA NDOGO, HUWA HAIRUDISHWI ILE

NA HII YA KUSEMA KILA KITU KIMEPATIKANA HADIO FEDHA TASLIMU INATIA SHAKA
 
Hiyo ndo faida kuzurumu. Kiwanja kimeporwa toka kilimo mkoa.feza ya kujengea imetoka richimondi . Unategemea nini ? Pale pana ufisadi zambi yake iwatafuna milele mpaka atuludishie maela yetu
 
Boss akiwa mwongo wote mnakuwa waongo waongo tu.
Na boss akiwa kilaza wote mnafanana nae tu!

Hence, serikali ya vilaza na waongo waongo tu!
 
Back
Top Bottom