Hoteli ya NASHERA imejiharibia?

Kama ni kweli kikundi cha majambazi/wezi kiliweza kuingia kwenye hoteli yenye hadhi kubwa kama Nashera na kuweza kumuibia Naibu Waziri maswali mengi yameachwa juu ya hoteli hiyo. Maelezo yote ambayo yametolewa hadi hivi sasa yanaionesha hoteli kwenye mwanga mbaya zaidi kuliko hata Malima. Think about it. Nadhani Hoteli itabidi ijisafishe tu kwa kueleza vya ukweli kwani watu wengine mashuhuri wanaweza kuhofia sana kwenda hapo sasa...

Lakini pia inaonekana hoteli haina SOP za kuonesha wafanyakazi wanatakiwa washughulikie vipi matatizo ya wateja. Inawezekana Malima kaenda kuripoti wizi kwenye front desk (kitu ambacho pia kinachangaza kwani ningeassume angempigia moja kwa moja meneja wa hoteli) na wale vijana wa FD walipopiga simu kwa meneja wakati huo huo waka sms marafiki zao "aisee Malima kachapwa hapa". Maana nasikia taarifa za Malima kuibiwa zilikuwa zimeenea kwa watu wengi kabla hazijaandikwa magazetini for at least 24 hours.

Je, wafanyakazi wanapotoa taarifa za ndani kama hizo yawezekana ni kwa sababu hawajali ajira zao au hata taswira ya hoteli yao? au hawana hisia kuwa ni "hoteli yao"?
Mkuu Mwanakijiji hili suala bado lina kizungmkuti: Kuna theory mbili; moja kwamba Naibu aliibiwa na mwanamke aliyeingia naye humo Hotelini. Huenda wafanyaazi walitumiana sms kwa kushangilia kwamba bwana mkubwa kapatikana. Malima mwenyewe amekanusha hilo. Sawa tumuamini.
Ya pili ni kwamba vibaka wamekuja na kuvunja dirisha na kufungua mlango na kumuibia Naibu waziri vitu vyote hivyo bial kuonekana na walinzi. Hapa ulinzi hotelini unakuwa na mashaka mno kwani hakuna tofauti kati ya hiyo Hoteli na Guest moja kule Unga limited ambapo jamaa walinichukulia simu yangu baada ya kukata wavu wa dirisha; ulinzi ulikuwa sifuri na mazingira yalikuwa hatarishi. Hilo la vibaka siliamini sana; kama ni vibaka basi ni JAMAA walikuja kuchukua document zao.
 
Kama ni kweli kikundi cha majambazi/wezi kiliweza kuingia kwenye hoteli yenye hadhi kubwa kama Nashera na kuweza kumuibia Naibu Waziri maswali mengi yameachwa juu ya hoteli hiyo. Maelezo yote ambayo yametolewa hadi hivi sasa yanaionesha hoteli kwenye mwanga mbaya zaidi kuliko hata Malima. Think about it. Nadhani Hoteli itabidi ijisafishe tu kwa kueleza vya ukweli kwani watu wengine mashuhuri wanaweza kuhofia sana kwenda hapo sasa...

Lakini pia inaonekana hoteli haina SOP za kuonesha wafanyakazi wanatakiwa washughulikie vipi matatizo ya wateja. Inawezekana Malima kaenda kuripoti wizi kwenye front desk (kitu ambacho pia kinachangaza kwani ningeassume angempigia moja kwa moja meneja wa hoteli) na wale vijana wa FD walipopiga simu kwa meneja wakati huo huo waka sms marafiki zao "aisee Malima kachapwa hapa". Maana nasikia taarifa za Malima kuibiwa zilikuwa zimeenea kwa watu wengi kabla hazijaandikwa magazetini for at least 24 hours.

Je, wafanyakazi wanapotoa taarifa za ndani kama hizo yawezekana ni kwa sababu hawajali ajira zao au hata taswira ya hoteli yao? au hawana hisia kuwa ni "hoteli yao"?

Sadly itapita tu, tutaishia kuwaza na kuwazua anyways aibu yake na kithethe chake
 
Uongozi wa hoteli bila shaka utakuwa umeshinikizwa kukubali kuharibu jina la hoteli yao kwa gharama ya kumlinda Malima.

Sijui kama watakuwa wametafakari kwa kina madhara ya ''kukubali'' kuwa hotel yao haina ulinzi hadi vibaka kujifunza kuiba.

Watakuwa wametafakari na kugundua kuwa hawana cha kupoteza sababu wameichunga fedheha ya serikali na wizara hivyo warsha zote (labda japo za wizara) zitaenda hapo, mafunzo na semina elekezi yote ni hapo tu labda kwa hiari serikali iamue kuwatelekeza hao jamaa na hoteli yao...
kwa wageni binafsi na watalii wengine wasahau
 
Issue ninayojiuliza ni kwamba, inakuwaje walinzi wa hotel hawapo among the suspects? ningetegemea tuambiwe kwamba nao wamekamatwa na wanahojiwa! Hii picha sijui itaishiaje!
 
Ningependa kuuliza tu wajemeni. Je ndugu Malima alikuwa kwenye safari za kazi au binafsi? Kama alikuwa safari za kikazi, sijuhi kwanini alikwenda hotelini.

Miaka ya zamani. Kila mkoa na kila wilaya ilikuwa na Ikulu ndogo ambayo viongozi wa kitaifa walifikia. Na hizi Ikulu zilikuwa na ulinzi wa polisi.

Au siku zilibinafsishwa?
 
Bad image kwa kweli inabidi manager aje kuongea ukweli la sivyo anachangia kuipaka matope hotel kwa manufaa ya mtu m1.
 
MMM hilo wala haliwasumbui wamiliki wa hotel kwani nao wanatumikia malipo ya mshahara wa zambi.Haiingii akilini hotel kama ile mwanamke aliyeingia na mteja (Naibu waziri)atoke usiku /asubuhi sana na maegi bila walizi/wahusika kutilia mashaka.

Hawa wahudumu /walinzi walijua mchezo wote wakaacha mambo yaende kama yalivyoenda.Pia kuna suala jingine ambalo huwa hawa baadhi ya wakubwa wanajisahau kutokana na dharau zao .

Uwezekano upo kuwa huyu bwana ana tabia mbovu kama za baazi ya viongozi kuwakaripia wahudumu wa hiyo hotel /lodge kutokuwathamini,labda haachi tips.Hili linaweza pia ikawa sababu ya wafanyakazi wa hiyo hotel kumchukia na kuacha atendwe vibaya .

Hii ni fundisho kwa hawa viongozi wetu wenye tabia kama za huyu bwana.
 
Issue ninayojiuliza ni kwamba, inakuwaje walinzi wa hotel hawapo among the suspects? ningetegemea tuambiwe kwamba nao wamekamatwa na wanahojiwa! Hii picha sijui itaishiaje!
Mkuu Hapo kwenye panamaliza msala wote Jamaa kaibiwa na mtu aliyekuwa naye ndani ndo maana hakuna mtu wa kuwagusa walinzi wa hotel kwa sababu wao ndo wanaujua ukweli wote, jinsi jamaa alivyorambwa na demu. If u touch them watasanua kila kitu.
 
Bongo hakuna consumer criticality wala hotel review services, na watu baada ya wiki mbili tu watasahau wataenda kama kawaida.

Watu wanapanda mi boti iliyochakaa bila kuweka kibesi boti ziwe na mipira ya kusaidia kuogele, itakuwa hiyo hoteli?
 
Hii nchi inaendeshwa hovyo hovyo kiasi kwamba wana siasa wanakuwa na nguvu kuliko biashara. Najua wamiliki wa hotel wanalazimika kuwa wapole kwakuwa hata eneo la hotel walipora ardhi ya jeshi la magereza na chuo cha LITI. Mi kama ukimwaga mboga tunamwaga ugali. But mwisho wa siku watu wasio na hatia, walalahoi wanaadhibiwa na kuteswa kucover uovu wa wana siasa na zinaa zao

Ndio TAnzania hii, unaweza hata kujigawaia ardhi ya magogoni ukajenga a tourist hotel.
Ngojeni mamvi awe rais, utapata muziki wake akiondoka madarakani.
 
MMM hilo wala haliwasumbui wamiliki wa hotel kwani nao wanatumikia malipo ya mshahara wa zambi.Haiingii akilini hotel kama ile mwanamke aliyeingia na mteja (Naibu waziri)atoke usiku /asubuhi sana na maegi bila walizi/wahusika kutilia mashaka.

Hawa wahudumu /walinzi walijua mchezo wote wakaacha mambo yaende kama yalivyoenda.Pia kuna suala jingine ambalo huwa hawa baadhi ya wakubwa wanajisahau kutokana na dharau zao .

Uwezekano upo kuwa huyu bwana ana tabia mbovu kama za baazi ya viongozi kuwakaripia wahudumu wa hiyo hotel /lodge kutokuwathamini,labda haachi tips.Hili linaweza pia ikawa sababu ya wafanyakazi wa hiyo hotel kumchukia na kuacha atendwe vibaya .

Hii ni fundisho kwa hawa viongozi wetu wenye tabia kama za huyu bwana.

Hii kampuni ya mahita ina scandals nyingi sana hapo Morogoro. Hiyo siyo mara ya kwanza.
The reasons is simple: mshahara kiduchu, walinzi wanatafuta namna ya kuishi.
Sasa kama Shemeji kamtoka/kamlamba mkuu, akawagaia kidogo wano wana noma gani?
Hata wakilinda inavyotakiwa pesa kiduchu.
 
Mi naona hakuna sababu ya kuitia lawama hoteli kwa sababu za upuuzi. Unaweza kutoa lawama kama wewe si mwenyeji wa Morogoro. Mji kasoro bahari hakuna kahaba asiye mwizi. Mtu anachukua malaya kutoka Kahumba night club, au Makuti bar. Ataacha kuibiwa? Kwa ushahidi wa kimazingira jamaa hakuibiwa na wezi wa kawaida. Huo ulikuwa mchongo wa malaya tu.
 
Wala business yao haitakuwa affected! Nashera single room ni 150$ bed and bfast! Suite ni 300$ na deluxe double room ndo 200$. Wateja wao wanajulikana na hawajali publicity manake sio wa kusoma mwananchi newspaper!
Mahesabu yanajulikana hapo, ngoja tutaona maigizo part 2. Hata kama wafanyakazi walileak habari kwa waandishi wa habari, huwezi kunishawishi ati meneja wa hoteli alishindwa kukanusha ili kumlinda mteja. Kwa wanaoenda morogoro kikazi wanajua kabisa kulizwa na machangudoa ni kawaida sana na hata siku moja wakirudi hawatoi reports za kuibiwa laptop!
 
inawezekana imejiharibia au IMEHARIBIWA
Kwa hadhi ya Nashera na bei yake hatutarajii mwizi wa kuvunja dirisha..tena akiwa nyayo tupu na tope.
Upelelezi ule wa kufuata nyayo kama msukuma aliyeibiwa ng'ombe na mmasai[samahani watani wangu] ni kama kuweka benki bila CCTV..ukitokea wizi unawauliza wateja waliokuwepo kama wanamtambua suspect
 
Wala business yao haitakuwa affected! Nashera single room ni 150$ bed and bfast! Suite ni 300$ na deluxe double room ndo 200$. Wateja wao wanajulikana na hawajali publicity manake sio wa kusoma mwananchi newspaper!
Mahesabu yanajulikana hapo, ngoja tutaona maigizo part 2. Hata kama wafanyakazi walileak habari kwa waandishi wa habari, huwezi kunishawishi ati meneja wa hoteli alishindwa kukanusha ili kumlinda mteja. Kwa wanaoenda morogoro kikazi wanajua kabisa kulizwa na machangudoa ni kawaida sana na hata siku moja wakirudi hawatoi reports za kuibiwa laptop!

Uzuri ni kwamba it is not within the reach of most of the Tanzanians!
Tutaishia kulala B One, California, Zawadi, Gwami, Glonency, 88......
 
Back
Top Bottom