Hoteli wanayopika ugali asubuhi

Sasa si afadhali hata huo unapikwa asubuhi watu tushakula sana kiporo cha ugali na chai asubuhi alafu freesh tu unadunda mtaani!
Hiyo ni kawaida kwa Wachagga. Kwa Wachagga bila kupiga Kiporo cha machalari/ngararimo/Shiro/ngashi/sowe/shia na chai siku yao haijaanza.
 
Mie napenda ugali na maharage yaliyolala, tena yawe yaliungwa kwa maziwa fresh. Nikishukia na mtindi roho kwatu.

Mie hadi leo kuna siku napiga ugali asubuhi home.

Kwa kawaida(watu waliokulia mjni tunakuwa washamba kwa mambo ya kijijini). Hata mm siku ya kwanza kuona ugali asbh nilipoenda Mugumu mwaka 2010, sa1 watu na nguna...hakika nilishangaa sana! Ndipo nikawa najua kumbe ugali ni chai
 
kati ya watu walionishangaza kwa mwaka huu we ni wakwanza, kwani manyerere ameelezea kichuri ni nini? na mbaya zaidi kwa kujiamini unasema umezugwa,soma upya post ya manyerere kwa umakini utamwelewa kitu alichokieleza.
"Lete rungu kwa kichuri". Maana yake ni ugali wa mtama uliochanganywa kwa mhongo kwa nyama ya mbuzi. Pembeni lazima kuwe na pilipili.

WAKURYA hampo humu?! Ni kweli KICHURI ni nyama ya mbuzi wajameni??
 
tehe Ugali, au kwa kizungu inatamkwa Yugalai hahaaa aka chapa nguvu noma tupu, mie nipo ugali na kipande cha samaki hapo umenimaliza! Iwe asubuhi sijui mchana twende tu!
 

Yeeeeeuuuuuwwwwiiiiii...... Mkuu itabidi likizo ya mwaka huu niende home special kwa ajili ya hivyo vitu... Kwanza Kichuri, pili ubhusara, tatu ekhimoro, nne na mwisho huo uji unaotengenezwa kwa mafuta ya maziwa a.k.a NTOBHEKHE
 
Teh... mie nimesoma Kiribho mura!!!!
Aaah! umenikumbusha mbali sana, Nguku nilikwea nikiwa na miaka minne, kutokea Kibumaye via Kenyamanyori kila siku, sijui ng;enyi bado ipo! Irityambwe? jamani ile mboga ya thamani sana sijawahi ona!

Kubhusugurya amobha!! sijui km bado ipo hiyo!
 
Mmiliki na wateja wa hiyo hotel itakuwa from Mbeya
 
Dar! wewe huijui vizuri Mzee Mgaru wa Pugu/ Lumumba anapika ugari saa kumi na moja kila siku na nyama mchemsho vichwa vya ngombe. Mpaka saa sita mchana anamaliza mchezo!
 
Imekaa vizuri sana hii.
Dar! wewe huijui vizuri Mzee Mgaru wa Pugu/ Lumumba anapika ugari saa kumi na moja kila siku na nyama mchemsho vichwa vya ngombe. Mpaka saa sita mchana anamaliza mchezo!
 
Kigali ni kawaida ugali wa mhogo hotelini au mgahawani
 
Nyie wanaume wa kinondoni mtajua ninii!!!?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hizo mambo nyie hamuwezani kabisa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Njoo hapa kwetu Iringa keepleft ya uwanja wa samora, kama waelekea down ya ipogolo asubuhi nguna unapata tena nyeupe kabisa haina pumba kwa nyama choma .........
Akumbukwe daima mkuu Nelly Nyamachoma RIP
 
Mkuu hii Mwanza kawaida kanisa ugali saa 2 asubuhi umeshaiva unakula supu na ugali nilikua naona ajabu lkn siku hizi Nimeacha kushangaa
 
Kiafya ndivyo ipasavyo kuwa,

Asubuhi kula kama mfalme

Mchana kula kama malkia

Jioni/usiku kula kama mtumwa!

Na sababu za kufanya hivyo zipo
 
Miaka ile barabara mbovu sijui Sasa hv, Pawaga nililima mpunga, nimefika zangu na kile kibaridi nataka chai naambiwa hamna Kuna ugali na nyama za kuchoma/ kukaanga na rost la bamia.
Duuh nikachagua zangu nikawaambia ntakuja saa sita niifadhie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…