Hospitali zituheshimu wateja, mnatuibia sana

Halafu kuna hii tabia ya kurundikiana dawa, unakuta unapewa pain killer aina mbili tofauti, antibiotics aina tatu tofauti na dawa ya malaria hapo unaumwa malaria tu.
Wengine wanakucharge dawa za wiki halafu ukienda pharmacy unapewa dawa za siku tatu tu. Nilishapotezaga imani na hizi zahanati binafsi.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
 
Nilienda kituo binafsi nikapatwa nina U.T.I. Kwenda kwa daktari akanambia ni kali sana ilipofikia na vitisho juu, akaniandikia Azuma. Nilipoenda dirisha la dawa wakataka hela nikawaambia si nina bima wwkanirudisha kwa daktari. Daktari akafuta Azuma akaandika dawa nyingine.

Mwenyewe nilishangaa, Azuma si naisoma JF kuwa ni kali sasa inakuaje mimi naumwa mgongo na uchovu ndio nipewe hii. Nilipeleka karatasi ya vipimo kwa brother wangu graduate wa udaktari akanambia vipimo havioneshi kiwango cha kuhitajika Azuma
 
Halafu kuna hii tabia ya kurundikiana dawa, unakuta unapewa pain killer aina mbili tofauti, antibiotics aina tatu tofauti na dawa ya malaria hapo unaumwa malaria tu.
Wengine wanakucharge dawa za wiki halafu ukienda pharmacy unapewa dawa za siku tatu tu. Nilishapotezaga imani na hizi zahanati binafsi.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
Unaijua synergistic na additive effect?
Kabla haujapewa dawa jaribu kuuliza maswali kwa mtoa huduma wa afya
 
Halafu kuna hii tabia ya kurundikiana dawa, unakuta unapewa pain killer aina mbili tofauti, antibiotics aina tatu tofauti na dawa ya malaria hapo unaumwa malaria tu.
Wengine wanakucharge dawa za wiki halafu ukienda pharmacy unapewa dawa za siku tatu tu. Nilishapotezaga imani na hizi zahanati binafsi.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
Ukigundua hili.... Take time kumchallenge anayekurundikia madawa yote hayo.
 
Naifahamu.
Kuan situation hicho kitu hakihitajiki na hizo dawa zinatolewa ili mradi tu. Binafsi sio professional yangu hiyo but nimezungukwa na watu wa kwenye hiyo kada. Dawa nyingi zinatolewa kwa business na sio ukubwa wa tatizo.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
 
Jana nimeenda hospital moja hapa Tegeta kibaoni, na imeshajijua maana ipo peke yake pele kibaoni. Waanapiga bei kubwa sana wateja wao, kujiandikisha tu pale ni 7,500/= na sijui ni yanini maana hata file hupewi mambo yote yapo kwenye system za computer. Baada ya hapo anakwambia inachofuata ukamuone daktari, kumuona daktari ni 15,000/=. Dokata anakupa vipimo ukafanye, achana na gharama za vipimo hizi sibishani nazo.

Noma ilikuja baada ya vipimo vyote tukaandikiwa sindano 3 na dawa za kutuliza maumivu. Tuliambiwa gharama za sindano moja ni 37,000/= Hapo ndio kengele ikalia kichwani na kujua hapa kuna shida. Nikaomba niandikiwe ni sindano gani ili nichome mbele kwa mbele, hapo dokta akaanza kukataa anasema harusiwi kutoa hicho kitu inaweza kumletea shida kikazi, ilileta ubishi mkubwa sana kwakuwa mimi nimeshalipa kukuona na kila kitu kitoka kwako nimeshalipia na gharama za vipimo hapa niandikie hizo dawa mi niondoke, ndio kwa mbinde nikapewa majina ya hizo dawa.

Nikaenda pharmacy ipo opposite tu na hiyo hospital hizo dawa hapo wanauza 7,000/= tu na lile bomba la sindano ni 500/= Nikamlipa nesi 3000 nikachomwa sindano yaani 10,000/= nikawa nimepata tiba ambayo ilibidi nilipe 37,000/=

HOSPITALI MUWE NA HURUMA NA WATEJA WENU, MTU AKIUMWA ISIWE NAFASI YA KUMPIGA, SIO POA KABISA
Kuna hospital ipo mbezi kwa msuguri,
Mwanangu wa kike alilazwa siku 2 bili ikaja 670000,
Mm nilikuwa na kidonda nikaenda kufanyiwa dressing na dawa tu bili ikaja 135000, mpaka leo sina hamu nao hata kama nalipa kwa Bima
 
Ukigundua hili.... Take time kumchallenge anayekurundikia madawa yote hayo.
Kuna hospitali wanaitwa wauguzi wanaulizwa mbn dawa hizi na hizi hamziandiki zimejaa store tu. Kuna siku et jamaa kaandikisha cheti wanapigiana simu huyo anapesa fanya kweli. Hivi hii ethic kweli?.
Mtu unaenda unasema unaumwa kifua unaambiwa upime UTI na Malaria, hujasema unaumwa kichwa wala kupandisha homa.
Kuna dogo nilimpeleka hospital ana vipele mwilini, but aliambiwa apime UTI na Malaria.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom