Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,448
- 16,313
Malalamiko kwa Wizara ya Afya kwenda Hospitali ya Kitengule iliyoko Tegeta jijini Dar es Salaam.
Leo ndugu yangu alizidiwa ghafla, ikabidi wakimbize Kitengule kwani wanaishi karibu na hapo.
Alikuwa na tatizo la mguu kupata ganzi, na kupata maumivu ya mgonjo, tatizo ambalo limekuwepo kwa muda sasa. Hivyo leo maumizi yalizidi ndipo wakaamua wamuwahishe hapo Kitengule.
Baada ya vipimo ikiwemo xray, ameonekana ana tatizo kwenye misuli ya mgongo, ndiyo inayompelekea mpaka anapata ganzi za mguu.
Hivyo walianza na kumpa "Physiotherapy" kwanza ndipo wakafuatia suala la kumpa dawa.
Kimbembe kimekuja hapa kwenye dawa, daktari alowahudumia akawaambia dawa zinacost elfu 30 (30,000/=). Ndugu kwa wakati huo wakawa wameishiwa pesa, wakamuomba daktari japo awaandikie hiyo dawa kisha watanunua baadaye wakishajipigapiga angalau wanunue hata za kuanzia.
Cha kushangaza daktari amegoma katakata kuwandikia dawa kama hawana hiyi elfu 30. Na akaondoka kabisa ofisini kwake maana ilishakuwa jioni..
Hili jambo ni jipya kwa utaratibu wa matibabu ulivyo. Mgonjwa akishalipia gharama ya matibabu ina maana ni pamoja na kuandikiwa dawa la tatizo lake lililogundulika baada ya vipimo.
Wajibu wa daktari ni kumuandikia dawa mgonjwa, suala la atanunulia wapi halimuhusu, kama ipo hapo hospitali husika basi ni jambo jema, kama haipo basi ni haki ya mgonjwa kuandikiwa "Prescription" ili akanunue mahali inapopatikana.
Ni kosa kisheria na kimaadili kwa daktari kukataa kumuandikia mgonjwa dawa kwa sababu yoyote ile. Huyu mgonjwa akipatwa na lolote huko aliko huyo daktari na Hospitali kwa ujumla watakuwa wamehusika 100% kufa kwake.
Bado sijapata jina la huyo daktari, lakini nikilipata nitaliweka wazi hapa ili wahusike wasaidie kukomesha hawa wahuni walioingilia fani nyeti kama hii inayohusika na uhai wa wanadamu wenzetu.
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara Maendeleo ya Jamii