Fantastic Beast
Member
- Feb 18, 2019
- 50
- 533
Kwa wale ambao mmebahatika kupata watoto na mkatumia hospitali za serikali nadhani mnaelewa ninachoongea, kama kuna mtu hakuchangia hata senti basi aje hapa kunipinga.
Hizi kelele za eti huduma za uzazi ni fix tu za wanasiasa huko majukwaani, ila ukifika labor ndiyo utajua hujui.
Kuna mambo mawili ambayo huwa yanafanyika kulingana na level ya facility:
1. Low Level Facilities kama Dispensari, Vituo vya Afyana Hospitali za Wilaya huwa wajawazito wanapewa lists ya vitu vya kununua kabla hawajafika siku ya kujifungua kama vile Gloves, Vibana Vitovu, Nyuzi za Kushonea endapo mama atapasuka msamba nk.
Ukiachana na hivyo vifaa ambavyo wamama huambiwa waviandae, vipimo vyote vya maabara na ultrasound atakavyofanya mama mjamzito ni lazima alipie. Hakuna kitu cha bure.
2. Higher level facilities kama Hospitali za Mikoa, Hospitali za Kanda na Hospitali ya Taifa (MNH) huko mama hauendi na kitu. Kila kitu utakikuta kulekule lakini itakubidi ulipie.
Mathalani Muhimbili gharama zao ziko kama ifuatavyo:
A. Kujifungua kawaida ni 125,000/=
B. Kujifungua kwa Upasuaji ni 250,000/=
Hizo ni gharama za kujifungua tu, hizo ni tofauti na vitu vingine kama kufungua faili, gloves, mabomba ya sindano, dawa, vipimo vya maabara na vikorokoro vingine vyooooote mama atakavyotumia. Kila kitu unalipia, hakuna msamaha hata wa bomba la sindano hapo Muhimbili.
Ni wakati sasa serikali hasa wizara yake ya afya iache kudanganya majukwaani kwamba huduma za uzazi ni bure wakati siyo kweli. Ni unalipia kila kitu.
Kuna muda wafanyakazi wa afya huwa wanaonekana ni waongo mbele ya wananchi, kwa sababu huku mitaani mwanasiasa anajitapa huduma fulani ni buree, lakini mwananchi akifika hospitali anakutana na mkeka mreefu wa bili mpaka anashangaa.