POTIZILLAH
Member
- Apr 30, 2011
- 87
- 157
Jana nimeenda hospital moja hapa Tegeta kibaoni, na imeshajijua maana ipo peke yake pele kibaoni. Waanapiga bei kubwa sana wateja wao, kujiandikisha tu pale ni 7,500/= na sijui ni yanini maana hata file hupewi mambo yote yapo kwenye system za computer. Baada ya hapo anakwambia inachofuata ukamuone daktari, kumuona daktari ni 15,000/=. Dokata anakupa vipimo ukafanye, achana na gharama za vipimo hizi sibishani nazo.
Noma ilikuja baada ya vipimo vyote tukaandikiwa sindano 3 na dawa za kutuliza maumivu. Tuliambiwa gharama za sindano moja ni 37,000/= Hapo ndio kengele ikalia kichwani na kujua hapa kuna shida. Nikaomba niandikiwe ni sindano gani ili nichome mbele kwa mbele, hapo dokta akaanza kukataa anasema harusiwi kutoa hicho kitu inaweza kumletea shida kikazi, ilileta ubishi mkubwa sana kwakuwa mimi nimeshalipa kukuona na kila kitu kitoka kwako nimeshalipia na gharama za vipimo hapa niandikie hizo dawa mi niondoke, ndio kwa mbinde nikapewa majina ya hizo dawa.
Nikaenda pharmacy ipo opposite tu na hiyo hospital hizo dawa hapo wanauza 7,000/= tu na lile bomba la sindano ni 500/= Nikamlipa nesi 3000 nikachomwa sindano yaani 10,000/= nikawa nimepata tiba ambayo ilibidi nilipe 37,000/=
HOSPITALI MUWE NA HURUMA NA WATEJA WENU, MTU AKIUMWA ISIWE NAFASI YA KUMPIGA, SIO POA KABISA