Injinia
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 849
- 26
Jamani, kama ninakosea nirekebishwe, lakini, hivi udaktari si kati ya fani za kuheshimika na hivyo ktk nchi nyingi madaktari ni watu ambao huwa na maslahi bora? Sasa iweje jamaa zangu madaktari kcmc wachoke hivyo? Nilitembelea Ms nikakuta wanaishi maisha yasiyoweza fananishwa na ya wenzao wa Muhimbili au Bugando ambako nako ni hospitali ya shirika la dini? Wanahemea mshahara mdogo ktk ngazi zote, ni aibu kutaja.. Ukiongea nao wamejawa malalamiko, hasa juu ya jinsi palivyogeuka sehemu ya miradi ya utafiti wa kimataifa wanayodai hainufaishi wafanyakazi bali uongozi wa juu!