Betterhalf
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 2,879
- 2,554
Habarini wakuu.Poleni kwa majukumu ya mchana kutwa. Naomba nijielekeze kwenye mada moja kwa moja.
Tangu awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na wimbi kubwa la wanasiasa hususan Wabunge( nasita kuwaita kwa lile jina lao la utambulisho) kuhama hama vyama wengi wakijiuzulu nyadhifa zao.
Kinondoni, Liwale, Manyara n.k yamekuwa ni baadhi ya majimbo ambayo yamepitia nyakati za namna hii.
Pamoja na wimbi hilo, nimekutwa na kimuhemuhe cha kuja na uzi huu kama changamoto ya kupima ueledi au utashi wa wabunge wa kike na wa kiume. Kwanini? Ni kwa sababu kwa rekodi nilizonazo, wabunge wote waliohama vyama ni wa kiume. Kwa nini kusiwe na wabunge wa kike?
Je, hii inaashiria uimara wa wabunge wanawake au nini?
Wakati nasubiri majibu yenu juu ya mitazamo yenu, nadiriki kusema HONGERENI SANA WABUNGE WANAWAKE. Kwangu mimi mmekuwa imara zaidi kuliko wale waliohama vyama na kuwaacha wapiga kura wao ambao waliwapambania wakibaki hawana la kufanya.
Nawasilisha.