Hongereni wabunge wanawake kwa ujasiri wenu wa kutohama vyama kuunga juhudi

Betterhalf

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
2,879
2,554
Habarini wakuu.Poleni kwa majukumu ya mchana kutwa. Naomba nijielekeze kwenye mada moja kwa moja.

Tangu awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na wimbi kubwa la wanasiasa hususan Wabunge( nasita kuwaita kwa lile jina lao la utambulisho) kuhama hama vyama wengi wakijiuzulu nyadhifa zao.

Kinondoni, Liwale, Manyara n.k yamekuwa ni baadhi ya majimbo ambayo yamepitia nyakati za namna hii.

Pamoja na wimbi hilo, nimekutwa na kimuhemuhe cha kuja na uzi huu kama changamoto ya kupima ueledi au utashi wa wabunge wa kike na wa kiume. Kwanini? Ni kwa sababu kwa rekodi nilizonazo, wabunge wote waliohama vyama ni wa kiume. Kwa nini kusiwe na wabunge wa kike?

Je, hii inaashiria uimara wa wabunge wanawake au nini?

Wakati nasubiri majibu yenu juu ya mitazamo yenu, nadiriki kusema HONGERENI SANA WABUNGE WANAWAKE. Kwangu mimi mmekuwa imara zaidi kuliko wale waliohama vyama na kuwaacha wapiga kura wao ambao waliwapambania wakibaki hawana la kufanya.

Nawasilisha.
 
Wanawake tukiamua ku support kitu huamua toka moyoni. Wanawake tukijitambua sisi ni ma agent wazuri wa mabadiliko ya kweli, tunakumbuka tulipotoka na tuna uchungu, wanaume hamuaminiki ka mnaweza telekeza familia na msiwe na uchungu mioyoni. Wanawake ni ma agent wa mabadiliko ya kweli hatuna uoga ka wanaume wasio na msimamo
 
Wanawake tukiamua ku support kitu huamua toka moyoni. Wanawake tukijitambua sisi ni ma agent wazuri wa mabadiliko ya kweli, tunakumbuka tulipotoka na tuna uchungu, wanaume hamuaminiki ka mnaweza telekeza familia na msiwe na uchungu mioyoni. Wanawake ni ma agent wa mabadiliko ya kweli hatuna uoga ka wanaume wasio na msimamo
Ahsante Cariha, nakubaliana nawe.Kwa kweli, wanawake mmetisha.Big Up.
 
Wanaume wamekuwa waoga zamani tuliaminishwa eti wanaume ni majasiri sasa hawa si wanaweza kuuza hata familia. Sifa ya mwanaume halisi misimamo yake anayo isimamia
Kuhama chama,si sababu ya yote hayo mnayoyasema

Mwanaume ni mwanaume,na itabaki hivyo
Sifa zake timilifu,haziwezi kuondoka kwasababu ya maneno na mfano wake

Lau kama hicho ndio kipimo chetu sahihi cha kuwapima watu,Basi tutalizamisha jahazi
 
Back
Top Bottom