Uenezaji wa ushoga waweza kuwa mbinu mojawapo ya maangamizi ya kimbari

T Kaiza-Boshe

Member
May 27, 2013
20
39
Kwa wiki kadhaa sasa, Watanzania wamekuwa wakisikia mengi ya kushangaza, kusikitisha, na kukasirisha kuhusu wimbi la ushoga nchini na kwingineko. Mbali na kinachoonekana kuwa kukithiri kwa matendo haya machafu; yasiyokubalika kijamii, kitamaduni, kidini, na kisheria; kinachoshangaza na kutisha zaidi, ni wimbi hili la ushoga kutandawaa nchini na kwingineko Afrika kwa kufadhiliwa na kuchochewa na mashirika yenye makao makuu nchi za Magharibi, hususan Marekani.

Kingine kinachotisha ni weledi na mbinu zinazotumika kueneza na kuratibu matendo haya yaliyokwisha kuadhibiwa na kulaaniwa na Mwenyezi Mungu tangu zama za kale; na haya yakifanyika katika nchi ambayo wananchi walio wengi ni wafuasi wa dini zinazokataza ushoga na yenye sheria za kukataza mapenzi ya jinsi moja tangu 1934. Hivyo uenezaji huu wa ushoga unaendeshwa kama vuguvugu la kimataifa (international movement). Kama haya hayatoshi, vuguvugu hili limeunganishwa na harakati za kimataifa za kudai haki za binadamu na demokrasia, na hivyo kufanywa suala la siasa za kimataifa na nchi. Na hapa ndipo panaonekana kuwa pachungu kwa nchi zinazoendelea; kwa maana kupitia siasa hizo, nchi za Magharibi zinatumia kete ya misaada kurubuni nchi maskini kuukubali ushoga, hata kama siyo waziwazi.

Japokuwa tayari kumeishajitokeza waziwazi rais wa Kiafrika wa kusema kama hivyo hatuhitaji misaada yenu; kunatakiwa ujasiri mkubwa sana mkuu wa nchi maskini kukataa ushoga kwa jinsi nchi hizo za Magharibi zinavyotumia vitisho. Hivyo ni jambo la ujasiri na fahari kwa Rais Yuweri Museveni wa Uganda kujitoa mhanga na kuwa mstari wa mbele kukataa ushoga; na hata Bunge la nchi hiyo kupitisha sheria kali ya kukataza ushoga nchini mwake.

Watanzania walio wengi wamebakia kushangaa, kuchukizwa, na kulaani; wasijue la kufanya. Wengi wanadhani harakati za kueneza ushoga ni mbinu za nchi za Magharibi kuharibu vijana wetu, na hatimaye taifa kwa ujumla. Hawa wanaliona wimbi hili la ushoga kama vile linalenga kubadili tabia na mtindo wa maisha. Wasiloliona wengi harakaharaka, ni kwamba kwa mtindo huu wa uenezaji ushoga, na kasi iliyodhihirishwa na takwimu zilizosomwa na Mheshimiwa Harrison Mwakyembe na mwandishi wa habari za kiuchunguzi Catherine Kaabi kwenye semina ya viongozi wa dini mbalimbali hivi karibuni, ushoga sasa ni baa linalotishia kuangamiza jamii (mbari) ya Watanzania na watu weusi Barani Africa; kama hazitachukuliwa hatua thabiti na za haraka kukabiliana nao.

Yamkini ushoga wa wanaume unatumiwa kama mbinu ya kupunguza watu kizazi hadi kizazi kwa kasi kubwa bila madhara yanayombatana na mbinu nyingine za kimbari (genocide), mathalani, vita. Mbinu hii ni sawa na mbinu inayotumiwa na wataalamu wa uhifadhi wa wanyamapori kuangamiza mbung’o. Kwa mbung’o na wadudu waharibifu wengineo, kinachofanyika ni kuwafanya madume wasiweze kurutubisha mayai ya majike (sterilization). Mtindo huu umewahi kufanyika kwa binadamu pia. Mathalani, inasemekana kuwa watumwa waliopelekwa Arabuni zama zile walihasiwa, na matokeo ni kwamba hakuna watu weusi Arabuni kutokana na watumwa hao, tofauti na ilivyo Marekani, ambako weusi ni takribani asilimia 13 ya Wamarekani.

Mfano mwingine ni wa Argentina. Tunasoma katika maandiko kuwa zama za utumwa, weusi waliwahi kufikia theluthi ya wananchi wa nchi hiyo. Leo Argentina watu weusi ni wachache sana kutokana na kupunguza wanaume weusi kwa kuwatumia kwenye vita, pamoja na mtindo wa ndoa au maisha ulioitwa ‘whitening’. Mtindo huo ulihamasisha ndoa baina ya wanawake weusi na wanaume weupe, na hapo hapo wakawa wakihamasisha wahamiaji weupe kutoka Bara la Ulaya. Aidha mbinu hiyo iliweza kufifisha kuwepo kwa vizazi vya wanaume weusi kwa kuwapandisha hadhi kijamii wanawake weusi walioolewa na wanaume weupe pamoja na watoto wao mashombe. Utaratibu huo uliwahakikishia wanawake hao na watoto wao ustawi zaidi na kuwapunguzia maradhi na vifo kuliko ilivyokuwa kwa familia za wanaume weusi. Kutokana na maisha duni na uchache wa wanaume weusi, jamii ya weusi waliendelea kufa na kupungua kizazi hadi kizazi.

Kuna mambo matano makuu yanayofanya wimbi la ushoga la sasa kuwa tishio kubwa kwa kuwepo kwa Watanzania na hata weusi kwingineko kulikoathiriwa nalo Barani Afrika. Mosi, ni kwamba wanaume wanapoingia mahusiano ya ushoga wanakuwa wameondoa wanaume wawili kwenye uendelezaji wa vizazi vya jamii ya Watanzania au watu weusi kwa mpigo. Katika hali ya kawaida kila moja wao angeendeleza jamii hiyo kwa kuzaa watoto, mathalani watatu hadi watano, kwa wastani.

Pili, katika jamii za kiislamu na wapagani, ambao ni sehemu kubwa ya jamii ya Tanzania na kwingineko Afrika, mwanaume mmoja anaweza kuoa wanawake kadhaa na kila moja akazaa watoto watatu hadi watano. Hii ni kwa wastani tu; bado wapo wanawake wengi wanaozaa watoto zaidi ya watano. Kwa Waislamu kikomo ni wanawake wanne. Kwa wapagani, hakuna kikomo. Hivyo kwa mwanaume mmoja kuwa shoga anapunguza watoto wengi katika kizazi kinachofuata, kati ya 12 na 30. Ila kwa vile siyo kila Mwisilamu ataoa wanawake wanne, na kuna Waislamu na Wapagani wenye mke mmoja, ama wawili, tuchukulie wastani ya chini kabisa kuwa watoto 12.

Tatu, wimbi hili la ushoga lina msukumo wa vuguvugu, nguvu ya pesa, nguvu ya mataifa makubwa, nguvu ya mashirika makubwa, na ushawishi wa wanaharakati mbali mbali wenye mbinu za kila aina.

Nne, walengwa ni vijana; ambao ndiyo sehemu kubwa ya idadi ya Watanzania, sehemu kubwa ya wananchi wasiokuwa na elimu, sehemu kubwa ya wananchi wasiokuwa na ajira, na wengi wao wana uhitaji mkubwa wa mahitaji ya msingi. Aidha, vijana pia ni kundi linaloshawishika kirahishi kwa mambo ya anasa kama mziki, pombe, starehe, matamasha, na matumizi ya dawa za kulevya, mambo ambayo yanatumiwa kutengeneza mazingira ya kuwatengeneza vijana kuwa mashoga kwa urahisi bila hata wao kutarajia.

Tano, kwa mujibu wa taarifa za mitandaoni Tanzania imeteuliwa kuwa makao makuu ya mtandao wa ushoga AfriKa Mashariki, kati, na Kusini.

Katika makala hii naangazia zaidi wanaume, siyo kwa kupendelea jinsi moja na kudhalilisha nyingine; bali ni matakwa ya uhalisia wa tatizo ulivyo. Kwa vile lengo ni kuonesha ukubwa wa tishio, inakuwa sina budi kuangazia jinsi ya kiume kwa vile wao ndio tatizo kubwa zaidi.

Hata hivyo sina budi pia kwanza kueleza kwa nini wanawake mashoga (wasagaji) si tishio kubwa katika kuangamiza jamii ya Watanzania au jamii ya weusi kwingineko Afrika. Sababu kuu ni kwamba mwanamke anazaa mtoto mmoja baada ya miezi tisa ya mimba na kumlea kwa takribani mwaka mmoja. Kupata mapacha ni jambo la nadra sana. Hivyo tunachukulia wastani wa mama kuhitaji miaka miwili kwa mimba na kumlea mtoto mmoja. Hivyo mwanamke anapokuwa msagaji hapotezi watoto wengi kama ilivyo kwa mwanaume kuwa shoga. Isitoshe mwanamke bado anaweza kupata mimba kwa kupandikizwa mbegu za kiume bila kujamiiana.

Tofauti na wanawake, wanaume wana uwezo wa kuwapa mimba wanawake kadhaa katika mwaka, na hata katika siku moja; kama siyo kuzuiwa na dini, jamii, dhamira, na kipato. Idadi ya watoto anaowezakupata mwanaume katika maisha yake ndiyo idadi ya watoto wanaopotea katika kizazi cha mwanaume anayeamua kuwa shoga. Hata kwa nchi za magharibi ambako mashoga wa kiume wameweza kuruhusiwa kuasili watoto, idadi ya watoto hawa ni ndogo sana, maana ni jambo gumu sana kijamii, kidini, na kisheria. Hata hivyo, watoto hao wa kuasili wanakuwa hawana nasaba na shoga aliyemuasili. Hivyo bado hao mashoga wanakuwa hawajaongeza watoto wa nasaba zao kwenye kizazi kinachofuata.

Ili kuweza kuona athari za ushoga wa wanaume kwa vizazi vya jamii husika, tazama takwimu hizi hapa chini zinazoonesha watoto (watu) wanaopotea kizazi hadi kizazi kutokana na ushoga wa wanaume.

Kama shoga ni Mkristo, tukichukulia wastani wa watoto 4 kwa kila mwanaume kwa kila kizazi, katika Vizazi 3 mwanaume mmoja atapoteza watoto 64 kama ifuatavyo: Kizazi cha kwanza 4, cha pili 16, na kizazi cha 3 watoto 64.

Kwa shoga asiyekuwa mkiristo, kwenye jamii ya Waisilamu na wapagani wanaooa wanawake wengi, tukichukulia wastani wa watoto 12 kila mwanaume kwa kila kizazi, katika vizazi vitatu mwanaume mmoja atapoteza watoto 1,728 kama ifuatavyo: kizazi cha kwanza watoto 12, cha pili 144, cha tatu 1,728.

Tukichukua idadi ya kukisia kutokana na idadi za mashoga wa kiume waliotengenezwa mwaka 2016 kwa mujibu wa wasilisho la Mhe. Mwakyemba kuwa imepita 100,000, tunaweza kutumia idadi ya 100,000 tukiwa na Imani kuwa hatujazidisha idadi yao kwa mwaka 2023. Kwa hesabu hizo hapo juu, ina maana wanapokuwa wametengenezwa mashoga 100,000 wa Kikristo watakuwa wamepoteza watoto 6,400,000 katika vizazi vitatu. Kwa wasiokuwa Wakristo watakuwa wamepoteza watoto 172,800,000 katika kipindi hicho. Takwimu hizi ni za wanaume wanaotengenezwa kwa utaratibu rasmi; bado wapo wengi wanaokuwa mashoga kwa mbinu nyingine shuleni, mitaani, na majumbani. Hizi mbinu nyingine tunaweza kuziweka kwenye makundi mawili kutegemea na zinakofanyiwa. Zipo mbinu zinazotumiwa zaidi shuleni na mitaani (majiani), na pia zipo za majumbani.

Mbinu za kueneza ushoga shuleni ni pamoja na za kuwapandikiza watoto wa kiume homoni za kike kwa kuwagawia na kuwaelekeza kutumia dawa za mswaki zenye homoni kwenye shule za bweni (boarding), biskuti zenye homoni, na vitu kama hivyo. Hapa wanatengenezwa wasenge. Mbinu nyingine za shuleni ni sawa na za mitaani na majumbani. Hizi zinatengeneza mashoga mchanganyiko, wasenge na mabasha. Hizi ni pamoja na kufundishwa, kushawishiwa, kurubuniwa, na hata kubakwa. Kama tunaona takwimu za Mheshimiwa Mwakyembe kuhusu mashoga wanaotengenezwa kupitia vyama au mtandao zinatisha, takwimu za watoto na vijana wanaofanywa mashoga kwa mafunzo na kulishwa homoni zingepatikana zingetisha zaidi. Mathalani, kwa mujibu wa Waziri mwenye dhamana ya watoto na jinsia nchini, uchunguzi uliofanywa na serikali umebaini kuwa asilimia 60 ya kesi za ulawiti wa watoto zinatoka majumbani!

Kinachotia hofu zaidi kuhusu jamii ya Watanzania, ama watu weusi, kupoteza mchango wao kinasaba katika vizazi vijavyo, ni kwamba, mbali na ushoga wa wanaume, kuna na mambo mengine yanayosemwa na wanasayansi kuwa yanapunguza uzazi wa mwanaume. Mambo haya ni pamoja na makelele na bidhaa za vyakula zinazosemekana kuwekewa vinasaba vinavyopunguza uzazi kwa watu weusi. Japokuwa siwezi kuthibitisha suala la vinasaba kulenga kupunguza uzazi wa watu weusi, ni jambo ambalo limekuwa linazungumzwa na wanasayansi wa nchi za Magharibi, na kwa vile kukosa uzazi ni tatizo linaloonekana kuongezeka nchini, ni muhimu kuliweka maanani.

Kwa kuhitimisha, ni kwamba, mbali na ueneaji wa ushoga kuwa na athari kubwa kijamii na kiuchumi, ushoga wa wanaume unatishia kupoteza jamii husika, hususan Watanzania. Aidha, ushoga wa wanaume wa Kiafrika ukiiunganishwa na mbinu mbalimbali za nchi za Magharibi zinazosemekana kulenga kupunguza uzazi wa watu Weusi, kwa pamoja zinaweza kusababisha maangamizi ya kimbari. Na kwa sababu hii natoa rai kwa serikali kuchukulia ushoga kama janga la maangamizi ya kimbari na kukabiliana nalo kwa uzito huo. Hivyo pamoja na kuipongeza Serikali kwa hatua zilizochukuliwa kuwalinda watoto wa shule za awali na msingi dhidi ya ushoga, na kuhimiza kazi iendelee; nashauri Serikali ipambane na mtandao wa ushoga na washirika wake mithili ya vita ya kimbari hadi kuuondoa kabisa nchini.

Na Theonestina Kaiza-Boshe
Email: tkaiza@gmail.com
 
Uzi kama huu utakosa wachangiaji, mkuu umeongea point sana.

Serikali, na jamii kwa ujumla watambue kuwa wimbi la ushoga ni vita kubwa. Mikakati iwekwe, sheria zitungwe na zitekelezwe.

Nilipoona video ya askari wa zanzibar nikawaza sana. Imagine miaka ijayo mnaingia vitani alafu jeshi nusu ya jeshi ni wanaume mashoga. Kuna kushinda vita kweli hapo?

Mbali na vita, idadi ya watu inapungua nchini. Watu ni muhimu sana katika taifa lolote. Bila watu hakuna nchi hakuna taifa.

Watu wakichukulia poa itafika wakati Tanzania watabaki watu 12.

Ushoga, punyeto, usagaji, ni vitu vya kupingwa vikali sana. Zote ni silaha za kivita kupunguza watu nchini.

Wachezaji wa Video za ngono wanalipwa pesa ndefu sana, yet kuangalia hio video hulipii chochote ni wewe na MB zako download basi. Huwazi? Huwazi kwanini watu waingie gharama kutengeneza hizo video alafu wewe uangalie bure tu?

Ukiomba kazi mashirika ya kimataifa alafu ukajielezea kwamba wewe ni shoga unapewa kipaumbele kikubwa hata kama una uwezo mdogo wa kiutendaji. Anaweza kuachwa mtu anayestahili ukachukuliwa wewe kwasababu ni shoga.

Kwanini wanafanya hivyo?

Kuna mashoga wanadai wao waliumbwa hivyo. Hivi kweli Mungu anaekataza ushoga alafu huyo hiyo Mungu aumbe mtu shoga? Atakuwa ni Mungu wa namna gani?

Watu wanahisi wameumbwa hivyo kumbe ni chanjo walizochomwa tangu wadogo, kumbe ni pampas walizovaa wakiwa wadogo, kumbe vyakula imported walivyokula wakiwa wadogo, cartoons, movies yaani majamaa wanatumia pesa nyingi na njia nyingi sana kusukuma ajenda yao.

HII NI VITA TENA SIO YA KITOTO. TANZANIA TUAMKE
 
Kusema kweli katika kuishi kwangu huwa nahisi ushoga unatokana na kupagawa na roho chafu,,na zaidi sio jambo lililo katika mipangilio yoyote ya binadamu,,,ni kama kuwa na kichaa either cha kuzaliwa nacho ama cha kurogwa,,,yaani niliuwaza ushoga ktk superstition tu.

Ila katika huu uzi nimepata kitu kingine kwamba ushoga kutumika kwa faida za kimkakati wa kitaifa kwa mataifa makubwa ya kidunia.

Jambo lingine nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini taifa la marekani kuwa na wazo la kupunguza watu??kwani wingi wa watu unawaathiri nini?? ni nini kimejificha ndani ya ajenda zao kuhusu kila taifa,,,mbona wanaharibu hadi taifa lao wenyewe??

Basi nikajiridhisha kwamba either na wao kuna anaewamiliki na kuwaongoza au wana mkono ktk kila mali za mataifa mengine hivyo wanaogopa wasiwe wengi ili wapate umiliki wa mali za wengine...Nikiangalia kuanzia chanjo za watoto mahospitalini napata wasiwasi sana,,maana hizo chanjo wanajua siri yake na hatujawa tayari kukabiliana nao.

Suala la ushoga lipo ila nikajiuliza pia usalama wa taifa hawana wajibu wa kulinda raia au hakuna kitengo ndani ya wizara ya mambo ya ndani kulinda nchi zidi ya madhara ya watalii wanayoweza kuyaleta kwa wananchi, au kitengo hicho kifuatilie wageni wanafanya nini humu nchini hata kama ni ndani ya vyumba vyao (hasa wale walioamua kuishi hapa Tz) Ninahisi kama ushoga umekuwa silaha ya vita ya kiuchumi na sisi tumelala hivi,,basi tumeshafeli maana kama tz kunaweza kuwa na mashoga laki moja basi hio ni colateral damage.

Tutaanza kuwa wateja wa vilainishi na dawa za fangas sugu za mashoga na pampasi zao.Sijui mashoga wanatumia pampasi ngapi kwa siku.

Na wakiwa labda elfu 50 tayari kiwanda cha pampasi kinakuwa kinasuply kontena hata 30 kwa tz,,na usikute yule kimara haris (mliberali) aliingia hata ubia wa kutengeneza kiwanda hapa hapa cha pampasi na vilainishi,,maana tunawapenda sana wawekezaji kutokana na kuwa na viongozi dhoofu na ruber stamp ya waliberali.

Nakushukuru mtoa mada kwa kuniongezea elimu.
 
You have think in a big picture ,Hii vita ni ngumu sana tuendako bila Mungu hatutoboi miaka mitatu ijayo unaeza ambiwa usiporuhusu usenge nchini mwako basi utawekewa economic sanctions .Kwa nchi zetu za kiafrika ni ngumu sana kutoboa
 
Hao mabahasha na mashoga wanalipwa wapi?haya mambo yapo kitambo tokea nipo primary Kuna watu walikuwa wanatatuliwa marinda,Kuna jamaa mmja alikuwa anamtatua mbaba mtu mzima mwenzake,paka Sasa hao wazee wapo na mmja alikuwa mwenyekiti wa chama Cha siasa
 
Nmekuwa nikichukizwa na hili swala kwa kipindi kirefu sababu kubwa ni Kuwa sitaki Kizazi changu kipitie hili janga.

ila kupitia huu uzi na fact ulizoziongea nmepata sababu nzuri ya kupinga hili janga lisikute na vizazi vya watu wengine.
 
Aisee uzi huu umenifumbua
macho hasa kuhusu hasara zinazotokea endapo mwanaume atakuwa shogo
kweli tunapoteza vizazi sababu ya
ushoga
 
Una kitoto chako unajua kitaendeleza Mbegu yangu duniani....siku moja unagundua sivyo unavyofikir kitoto kinaliwa nyuma na imechelewa Ile ya mnara kufa kabisa inaumaje?... Wewe unakula watoto wa wenzako ushawahi kuwaza ungejisikiaje wa kwako akiliwa hiyo kitu? .......Kuna vitu vinauma sana humu duniani basi tu
 
Kwa shoga asiyekuwa mkiristo, kwenye jamii ya Waisilamu na wapagani wanaooa wanawake wengi, tukichukulia wastani wa watoto 12 kila mwanaume kwa kila kizazi, katika vizazi vitatu mwanaume mmoja atapoteza watoto 1,728 kama ifuatavyo: kizazi cha kwanza watoto 12, cha pili 144, cha tatu 1,728
Duh hizi estimations mbona ni exagerated sana. Mkuu hao mabeberu mbona Wana mbegu za kupandikiza siku hizi, yaani baba mmoja anaweza uza mbegu kwa wanawake hata 100 so uzazi sio issue sana kwamba ni lazima dume ampandie jike.

Sisi tujikite tu kwamba ushoga sio sawa KIIMANI na KIMAADILI ila kutafuta back up sijui ni genocide sijui kupoteza watoto nadhani ni kupanua mjadala kiasi kwamba mtawapa justifications wanaotetea ndoa hizi.

Kumbuka mapendekezo ya sheria mfano ya Uganda inasema shoga akikamatwa auwawe au kwa Tanzania afungwe miaka 30. Ina maana hata akifungwa si hatoweza kuzaa? Sio sababu ni shoga pekee ila sababu amefungwa au amenyongwa na serikali?

Nadhani unaona jinsi mnavyopanua mjadala hapo.
 
Una kitoto chako unajua kitaendeleza Mbegu yangu duniani....siku moja unagundua sivyo unavyofikir kitoto kinaliwa nyuma na imechelewa Ile ya mnara kufa kabisa inaumaje?... Wewe unakula watoto wa wenzako ushawahi kuwaza ungejisikiaje wa kwako akiliwa hiyo kitu? .......Kuna vitu vinauma sana humu duniani basi tu
Tatizo linaanza kwa wewe mzazi mpaka hapo, na sio tu mtoto wa kiume hata wa kike kubebeshwa mimba n.k. maadili yanaanzia nyumbani Sasa unakuta nyumbani vigodoro, miziki inayopigwa ni ya kina Mondi, unategemea maadili yatakuwepo?

Kingine Kila kitu kina tiba hata kama kazaliwa na hormone za kike Kuna supplements za kumuongezea testosterone so interest kwa wanaume inakufa.

Ila ukifuatilia wengi waliingiliwa wakiwa wadogo na ndugu au majirani so na hapo jukumu ni la mzazi kumchunga mtoto. Sio Kila siku anaenda sijui kwa mjomba sijui shangazi au analala na wageni n.k
 
Hata hivyo sina budi pia kwanza kueleza kwa nini wanawake mashoga (wasagaji) si tishio kubwa katika kuangamiza jamii ya Watanzania au jamii ya weusi kwingineko Afrika. Sababu kuu ni kwamba mwanamke anazaa mtoto mmoja baada ya miezi tisa ya mimba na kumlea kwa takribani mwaka mmoja. Kupata mapacha ni jambo la nadra sana. Hivyo tunachukulia wastani wa mama kuhitaji miaka miwili kwa mimba na kumlea mtoto mmoja. Hivyo mwanamke anapokuwa msagaji hapotezi watoto wengi kama ilivyo kwa mwanaume kuwa shoga
Una hoja nzuri mkuu ambayo unaweza ifanyia tafiti ukapata mabilioni na ukajengea hoja kwenye jumuiya za dini na serikali kupinga ushoga.

However takwimu zako na nadharia ziwe na uhalisia. Mfano unaposema Shoga ana madhara kuliko usagaji ilihali wanafanya Yale Yale inakua understatement sana.

Kama msagaji anaishi na msagaji mwenzake huyo mwanaume atamzalisha nani?

Ni hivi unapopinga ushoga lazima upinge na usagaji pamoja na anal sex. Maana yote yakiwa addictive issue hiyo hiyo ya genocide inatokea yaani kama wanaume hawatakua mashoga ila wanawake ni wasagaji au wanawake wanafanya anal sex then Bado watoto wengi watapotea pengine hata kuliko wanaume wakiwa mashoga ila wanawake sio wasagaji.

TLDR; Nguvu ya kupinga ushoga iende sambamba na kupinga usagaji na ngono kinyume na maumbile.
 
Hao wazee wa upinde wamejipanga kwelikweli sidhani kama tutatoboa kwa staili hii ya kupenda vya bure na misaada maana inakuja na hizo condition za kichoko
 
Hao mabahasha na mashoga wanalipwa wapi?haya mambo yapo kitambo tokea nipo primary Kuna watu walikuwa wanatatuliwa marinda,Kuna jamaa mmja alikuwa anamtatua mbaba mtu mzima mwenzake,paka Sasa hao wazee wapo na mmja alikuwa mwenyekiti wa chama Cha siasa
Bora usemee wee hapa.
 
Uzi mrefu lakini ulicho kiandika ni uzushi, dhahania, uongo na propaganda tupuuu.

Kafanye utafiti afu urudi upyaa hapa tena.
 
Back
Top Bottom