The lost
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 2,695
- 8,209
Wakuu taifa letu linatekeleza maadhimio kadhaa kuhusiana na mikataba mbalimbali ya usawa wa kijinsia. Moja ya mikataba hiyo ni pamoja na ule wa kuhakikisha uwepo wa usaa katika vyombo vya maamuzi.
Bunge letu limeridhia kuwepo kwa wabunge wa viti maalum lakini upatikanaji wao umekuwa wa hisani hivyo kupelekea kuwa watu wasio na msimamo dhabiti wa kimaamuzi na kihoja bungeni. Pendekezo langu ni hili;
1. Wabunge viti maalumu wapigiwe kura kwenye majimbo yao kwa uchaguzi utakohusisha wanawake pekee.
2. Wabunge viti maalum wasigawiwe kwa mfumo wa vyama vya siasa ila wagombee kama wagombea wengine kupitia vyama vyao vya kisiasa kwa utaratibu wa wagombea wote katika kundi hili kuwa wanawake.
3. Viti maalumu vitambue uwepo wa walemavu na vijana na wasipungue watu 20 kutoka katika makundi hayo, mathalani katika bunge letu kuna wabunge 113 viti maalumu hivyo angalau wabunge 15 wawe ni kutoka kundi la wenye ulemavu na 15 kutoka kwa vijana na mama wajane, wazee na wafugaji.