Hongereni STRABAG! Dar Rapid Transit imefana mno!


wewe lazima ni wale ambao hata kusimama kwenye zebra crossing mnaona tabu mpaka wapita njia wanawapisha nyinyi na magari yenu.....acheni u selfish mnajifikiria nyinyi tu magari yenu,kaeni kwenye foleni sisi watumia daladala tunahamia kwenye dart hakuna foleni
 
Kweli kazi nzuri sana kwa miji ya kisasa
Kasoro ndogo tu ni kwamba Sio rafiki kwa walemavu wavuka njia.
Fuatilia Kipindi alichorusha Zembwela Jpili iliyopita sehem za kuvukia hasa kwa walemavu ndio utapata jibu.
Kama Amon Mpanju angekuwa anajitambua, angeyapigania haya, badala yake anakazania kusema "Chalinze tumewagaragaza, na Kalenga tumewagaragaza".
 
Naombeni ufafanuzi wa DART na BRT, naona kama ni abbreviations mbili tofauti lakini they're used interchangeably!
 

Lengo ni kuboresha public transport hata nchi za ulaya kama hapa sweden wamefanya priority kwa colectiv transport (public transport) na pia wamefunga badhi za barabara kwa ajili ya mabasi tu na pia kuna ada ya unalipia ya kuingia ndani ya mji na hiyo imefanya magari kupungua sana. Kwahiyo tuombe serikali ya Tanzania ijitahidi kufanya hivyo na wajenge barabara zaidi kwa ajili ya daladala
 
Wewe unauona kama uselfish! Lakini mradi lazima uangaliwe kwa ujumla wake! Yale mabasi yatakuwa yanapita may be kila baada ya dk 5 au 10. Inamaana kila baada ya dk 5 mpaka 10 katika kila kituo kutakuwa na stoppage ya magari! Hapo utakuwa hujapunguza foleni! Wakati lengo kubwa ni hilo! Wenzetu miradi kama hiyo katika vivuko watu wanavukia chini au juuu ya barabara!
 
Kweli kazi nzuri sana kwa miji ya kisasa
Kasoro ndogo tu ni kwamba Sio rafiki kwa walemavu wavuka njia.
Fuatilia Kipindi alichorusha Zembwela Jpili iliyopita sehem za kuvukia hasa kwa walemavu ndio utapata jibu.

Kasoro nyingine kubwa ni kwamba kwenda au kutoka kituo cha Bus katikati ya barabara ilibidi kuwe na njia ya chini au daraja kwa juu. Hii ingefanya magari mengine yaendelee kupita bila bugudha. Huu mpango wa Zebra Crossing nchi yenyewe Tanzania ambapo Zebra Crossing ni hiari ya dereva itakuwa hatari sana. Najua wamekwepa hili kupunguza gharama. Maji walishayavulia nguo ilibidi wamalizie tu. Labda siku za usoni itakuwa "dili" tena la watu wengine.
 
Sehemu zote iliyopita DARTS hakuna daladala Ina operate tena , in short kwenye DART itaondoa daladala na wameshaambiwa waunde makampuni YA hayo mabasi YA mwendo kasi
 

foleni haipunguzwi kwa kutopisha watu wavuke....foleni itapungua iwapo watu kama wewe wataona sense ya kuacha gari na kupanda public transport....daladala ilikuwa hilo haliwezekani kwa jinsi zilivyo ila utaratibu wa DART ulivyo ni standard hivyo atakaeng'ang'ania gari atakuwa limbukeni.
 
Nimekupata kiongozi, kwa hiyo Mwenge-Posta/kariakoo kupitia shekilango route itakufa, buguruni-kawe/masaki nayo itakufa sio?

Nadhani routes nyingi zitakufa au italazimu watu kupanda gari mbili/tatu hadi kufika wanapoenda..!
 
Sehemu zote iliyopita DARTS hakuna daladala Ina operate tena , in short kwenye DART itaondoa daladala na wameshaambiwa waunde makampuni YA hayo mabasi YA mwendo kasi
Manake Ni kuwa biashara ya wamiliki daladala nayo itakuwa ngumu. Coz kimara-posta route imekufa, Na njia ya kinondoni sijui...nayo route imekufa.
 

Comments zako kwenye 1, 2 na 4 zimenifurahisha. Nyongeza
(5) Njia ya kuwezesha kugeuza (Detour) za maana ziko pale Magomeni mwembechai kanisa la Anlican/Ban, na pale Jangwani; kwingine kote ni magumashi. Hata yale matoleo ya Kwa Thomas na Kibo yamekuja kama second thoughts, maana Strabag awali walikuwa wamepaziba, na baadaye wakabomoa.
(6) Fedha zilizowekezwa kwenye ile bara bara ya mwendo kasi ni too much (unene wa zege nchi tisa, nondo mm 19) bila sababu ya maana, au wanapanga baadaye treni au tram litapita juu yake?? Vituo ndiyo usiseme, utafikiri godown za bandarini au kiwanda!!
(7) Mitaro iliyokuwepo awali kuanzia Ubungo hadi Kibo ilikuwa ni ya wazi ili kama kuna takataka zimejazana zinachotwa na kuzolewa. Kwa sasa imerekebishwa kwa kuweka culverts na kufunika, sasa ikiziba sijui wataajiri vijana watambae humo ndani kuzibua.
(8) Nitaaongeza zingine baadaye.......


Vile vile matuita
 
Naombeni ufafanuzi wa DART na BRT, naona kama ni abbreviations mbili tofauti lakini they're used interchangeably!

Ni kweli mkuu kama zinaendana hivi maana DART ni Dar Rapid Transit na BRT ni Bus Rapid Transit
 
Kuboresha tunakubali lakini issue hapa ni ufinyu wa hizo barabara. Hata ukilipia halafu huwezi kuendesha comfortably kutokana na ufinyu wa barabara inakera
 
kweli kazi nzuri sana kwa miji ya kisasa
kasoro ndogo tu ni kwamba sio rafiki kwa walemavu wavuka njia.
Fuatilia kipindi alichorusha zembwela jpili iliyopita sehem za kuvukia hasa kwa walemavu ndio utapata jibu.

umechanganya madesa; ile ya zimbwera ni ya jaica (mwenge -tegeta) sio strabag
 
Kuboresha tunakubali lakini issue hapa ni ufinyu wa hizo barabara. Hata ukilipia halafu huwezi kuendesha comfortably kutokana na ufinyu wa barabara inakera

Nakuelewa ndugu Tulimumu ni shida hapo na hakuna uwezekano wa kuzipanua sababu hakuna nafasi. Cha muhimu ni sisi tunaotumia private cars kufuata sheria za barabara na kutumia akili na busara. Huku ulaya kuna baadhi za barabara mabasi yanasimama katikati ya barabara na wenye magari inabidi wadimame hadi basi litakapo ondoka hakuna wa kuchepua hapo, hiyo ndio heshima ya barabara na sheria zake.
Taratibu tutakuja kuzoea
 
Ni sheeda tup! vibarabara kama vichochoro vya zenji!!! wamekula tu pesa yetu. Kwa ushamba mlionao mtawasifia kwa barabara mpya.... ubora sifuri........ usumbufu 100%
 
Nimekupata kiongozi, kwa hiyo Mwenge-Posta/kariakoo kupitia shekilango route itakufa, buguruni-kawe/masaki nayo itakufa sio?

Nadhani routes nyingi zitakufa au italazimu watu kupanda gari mbili/tatu hadi kufika wanapoenda..!

Upo sahihi kabisa mkuu, kwa mfano mtu anatokea Sinza kwa Remy na anaenda K'Koo au let say Posta, itabidi apande bus mpaka Shekilango ili aweze kuconnect na haya mabus ya kwenye kwa haraka, hii inamaanisha kwamba uchumi wa watanzania inabidi ukue kidogo ili waweze kuafford hizi changes otherwise mtu inabidi atembee tu from Sinza to Shekilango ili apande bus la kwenda kwa haraka, kwa kweli ni changamoto. Buguruni-Kawe/Masaki inaweza kuwepo mpaka pale tu mpango wa barabara ya Kawawa itakapokamilika, lakini hata ikikamilika kumbuka yenyewe inaanzia magomeni Mapipa tu mana yake ni kwamba lazima mtu from Buguruni afanye mchakato wa kupanda bus jingine mpaka Mapipa. Yaani kazi kweli kweli. Kwa ufupi biashara ya coster na hiace bado itaendelea kuwepo baadhi ya sehemu. Kwa mfano route kama K'Koo-Tabata, Magomeni-Sinza kupitia Tandale, Mwananyamala Posta, Mwenge-Posta n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…