Hongereni Mabasi ya Kilimanjaro Express

Hongereni Mabasi ya Kilimanjaro Express

Kwanza kabisa naomba nitoe pongezi kwa kampuni ya mabus ya kilimanjaro kwa kuona thread yangu wiki mbili zilizopita na kuamua kuifanyia kazi

Jumamosi hii ya juzi kilimanjaro express wameanza kufunga ac kwenye bus zao nne ambazo zitaanza kutumia ac siku ya jumatano kesho kutwa,i hope dar express nao watabadilika

Ila sasa nataka niwakosoe kilimajaro express,hivi ni ubahili kiasi gani mlio nao mkaamua kuongeza siti kwenye bus zenu zinazofungwa ac?yaani kwa kifupi haina tofauti na school bus tena za chekechea,mmebana siti ziwe ndogooo hakuna nafasi ya kuweka miguu,yaani ubahili huu umepitiliza,hii yote ni katika kushindana na tahmeed.

Sasa kilimanjaro mmebana siti ili waingie watu wengi,tv moja tu,hakuna wifi,siti sio za ngozi,charging system hakuna,fridge na disposer hakuna,halafu leo hii mnataka kushindana na TAHMEED

Ikumbukwe katika njia ya dar moshi arusha nairobi SUMATRA wamethibitisha ni TAHMEED pekee ndio bus la kifahari kwa kubandika sticker ya blue mlangoni kuthibitisha kuwa ni bus la daraja la juu sana

Mbaya zaidi TAHMEED imeleta mabus mapya zaidi ya 25 yapo yard kufikiria ziende route ipi ,hii imewaletea wamiliki wa mabus wa kaskazini waliozoea kufanya biashara kwa mazoea kitu kinachoitwa TAHMEED fever

Kigoma mbeya mwanza songea kahama singida jiandaeni

Mrejesho:
kilimanjaro express wamefanikiwa kufunga choo ambacho hakitumiki na ac wameghaili kuwawekea wateja wao ila wamekumbuka kuongeza siti kwenye bus zao

so sad
mm binafsi nawapongeza sn TAHMEED kwn wameleta mapinduzi sn ktk industry y usafiri nchi hii kw kiac kikubwa n pia wameleta mabac ambayo yan ubora sn n pia yenye ubora! Hongera sn TAHMEED kw ubora wenu!
 
Tunaangalia usalama tangia nimeanza kupanda kilimanjaro miaka sita sasa sijawahi kusikia limechinja watu hayo mabasi yenu mnayokuja kuyatafutia soko humu hayaishi kumwaga damu za watu kila mwaka

Kwa roure ya Dar-Moshi-Arusha hakuna kampuni ya usafiri wa uhakika na salama kuishinda KILIMANJARO EXPRESS. Hawa jamaa wako vizuri na wanastahili pongezi!! Hongera sana bwana na bi Rowland!!
 
Yote tisa.....kumi ni kwamba kampuni ya BORN CITY iko njiani kuweka mabasi njia ya DAR/ARK.Wanaahidi huduma zilezile na hawatakuwa tayari kumuacha yoyote aliyekosa nauli kumrudisha home...kama zamani
 
Nami nina mpango wa kusafiri na Tahmeed soon...
Hatimaye nimetimiza mpango. Ndani ya Tahmeed sasa, tumefika Korogwe. Safari ni ya kutoka Dar kwenda Nairobi!


Very comfortable sana hawa Jamaa!!


Sidhani kama ana mpinzani, kama yupo aseme..
 
Hatimaye nimetimiza mpango. Ndani ya Tahmeed sasa, tumefika Korogwe. Safari ni ya kutoka Dar kwenda Nairobi!


Very comfortable sana hawa Jamaa!!


Sidhani kama ana mpinzani, kama yupo aseme


Sisi wa Moshi na Arusha hakuna mwingine bali KILIMANJARO EXPRESS.
 
Sisi wa Moshi na Arusha hakuna mwingine bali KILIMANJARO EXPRESS.
uploadfromtaptalk1466067266824.jpg
 
Mbongo ukimpa nafasi akikukosoa siku moja ukafanyia kazi basi next time ata taka akupangie mpaka mboga ya kula
 

Pamoja na maboresho hayo wakumbuke kupiga misasa ndimi za wahudumu wao kila wakati maana muda mwingine wanajisahau sana

Kwa upande wa TV ingependeza kama kila siti ingekuwa na headset zake ili kutompa usumbufu wa kelele msafiri asiye na interest na burudani hizo
Kisayansi siyo salama,utakufa kabla ya muda wako
 
Huo mrejesho tena vepe? Siti ni kweli zinabana sana mpaka ufike mwisho wa safari hasa sisi warefu miguu inakakamaa
 
Toa evidence na uwe mkweli kabisa kwa kumuogopa mungu lini umesikia tahmeed imeanguka au kuwaka moto,halafu nipm namba yako nikutumie mamia ya picha za ajali za kilimanjaro na dar express, mbaya zaidi kwa uongo wako wiki iliyopita kilimajaro imeanguka na kuua wiki iliyopita ikitoka stand arusha

Bro jipange vizuri lasivyo nitakuona hujawahi hata kuipanda hiyo kilimanjaro,maana hapa unatia aibu tu

Tahmeed Imeungua Jana! !
 
Yote tisa.....kumi ni kwamba kampuni ya BORN CITY iko njiani kuweka mabasi njia ya DAR/ARK.Wanaahidi huduma zilezile na hawatakuwa tayari kumuacha yoyote aliyekosa nauli kumrudisha home...kama zamani
Wale waarabu mmh dereva anamuuliza kondakta nikanyage ng'ombe wangapi hapa anasema 3, na anapitia watatu kweli, badala yakusubiri mifugo ipite kwanza, khaaaa
 
Kama zilivyo ajali nyingine
Umewajibu vizuri,mbona hawana subra katika kipindi cha.miaka 15 ndio tahmeed ya kwanza kuungua,kilimanjoro na dar express zimeungua mnoo ndani ya miaka mitatu hii
Pia kwenye tahmeed hakuna mzigo uliopotea wala alieumia lakin watu wameona ajali hiyo ndio sehemu ya kuhukumu na mkasahau hizo zinazoungua kila siku ndio zilipaswa zihukumiwe
 
Yote tisa.....kumi ni kwamba kampuni ya BORN CITY iko njiani kuweka mabasi njia ya DAR/ARK.Wanaahidi huduma zilezile na hawatakuwa tayari kumuacha yoyote aliyekosa nauli kumrudisha home...kama zamani

Aisee umenikumbusha mbali sana enzi za born city Dar - Arusha,enzi hizo tunatoka Arusha saa 12 jioni tunafika dar saa 10 Usiku ,chakula tunakula mombo yaani mombo ukipita usiku ni kama mchana vile kumechangamka balaa,aisee daraja la wami tunapita saa 7 au 8 usiku mnaanza kuamshana daa long time na mpinzani wa born city alikuwa anaitwa SMAA ,enzi hizo za nissan diesel ,enzi za isuzu,leyland,leyland daf
 
Back
Top Bottom