Hongereni Mabasi ya Kilimanjaro Express

Hongereni Mabasi ya Kilimanjaro Express

Overtaking hiyo umeiona halafu mtu anakuja hapa na kusifia gari za namna hiyo, ikitokea ajali dereva nae anasema barabara nyembamba!!
Huyo falcon mombasa kashaishiwa pumzi. Kaonyeshwa basi lao likiungua na sasa hii ya udereva uso makini kakimbia. Na kazi anaenda kuacha huko Tahmeed. Kwanza alikimbia falcon na spider huyu
 
Kwanza kabisa naomba nitoe pongezi kwa kampuni ya mabus ya kilimanjaro kwa kuona thread yangu wiki mbili zilizopita na kuamua kuifanyia kazi

Jumamosi hii ya juzi kilimanjaro express wameanza kufunga ac kwenye bus zao nne ambazo zitaanza kutumia ac siku ya jumatano kesho kutwa,i hope dar express nao watabadilika

Ila sasa nataka niwakosoe kilimajaro express,hivi ni ubahili kiasi gani mlio nao mkaamua kuongeza siti kwenye bus zenu zinazofungwa ac?yaani kwa kifupi haina tofauti na school bus tena za chekechea,mmebana siti ziwe ndogooo hakuna nafasi ya kuweka miguu,yaani ubahili huu umepitiliza,hii yote ni katika kushindana na tahmeed.

Sasa kilimanjaro mmebana siti ili waingie watu wengi,tv moja tu,hakuna wifi,siti sio za ngozi,charging system hakuna,fridge na disposer hakuna,halafu leo hii mnataka kushindana na TAHMEED

Ikumbukwe katika njia ya dar moshi arusha nairobi SUMATRA wamethibitisha ni TAHMEED pekee ndio bus la kifahari kwa kubandika sticker ya blue mlangoni kuthibitisha kuwa ni bus la daraja la juu sana

Mbaya zaidi TAHMEED imeleta mabus mapya zaidi ya 25 yapo yard kufikiria ziende route ipi ,hii imewaletea wamiliki wa mabus wa kaskazini waliozoea kufanya biashara kwa mazoea kitu kinachoitwa TAHMEED fever

Kigoma mbeya mwanza songea kahama singida jiandaeni

Mrejesho:
kilimanjaro express wamefanikiwa kufunga choo ambacho hakitumiki na ac wameghaili kuwawekea wateja wao ila wamekumbuka kuongeza siti kwenye bus zao

so sad
Kwanini tahmeed wasianzishe ruti ya nairobi kupitia rombo bonge la safari.
 
acha uwongo Kilimanjaro haijapata ajali wiki iliyopita ni magari pekee yanayoaminika kwa wengi ndo mana real Madrid walipokuja bongo walitoka dar-moshi kwa Kilimanjaro kwenda kupanda mlima
Alafu Kilimanjaro haifikagi stand ya mabasi Arusha, ina ofisi zake
 
Hawa jamaa ila Konda na Suka wao wana rugha ambazo sio kabisa, sijajua kama ni mabasi yote, ila kuna basi moja la Dar to Arusha kwa kweli konda sio kabisa plus Dereva wao
I agree with U.
Wanashida sana kwenye hili.
Lugha zao mbovu mno
 
Back
Top Bottom