Zama za Kilimanjaro Express zimeisha

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
6,515
12,602
Juzi kati nikawa na kijisafari cha kuelekea mikoa ya huko kaskazini mwa Tanzania. Nikasema ngoja nipande Kilimanjaro express, duh kwa kweli nilijuta sana kupanda lile basi.

Cha kwanza tulidanganywa kuwa basi ni luxury hivyo tukakatishwa nauli kubwa ila kiuhalisia hakuna luxury bus pale, bus siti zake zimechakaa, ndani linatoa harufu kama ya uvundo flani hivi, hakuna cha AC wala TV ndani ya basi. Basi lilikuwa limejaza kiasi kwamba abiria wengine wakawa wamekaa pale mbele kwa dereva na tulikuwa tukifika karibu na mizani wanawashusha baadhi ya abiria wanawachukulia bodaboda then tunawakuta mbele ya safari tukishavuka mizani.

Wahudumu wa basi ni kama wamekata tamaa yaani hawana mwamko na kazi yao, wanaongea lugha mbaya kwa abiria, badala yake muda wote wa safari walikuwa wamekaa tu kule mbele wanapiga story pasipo kusikiliza abiria pia bus lilikua linavuja.

Kwa kweli Kilimanjaro express niliyoipanda miaka mitano huko nyuma ina tofauti kubwa sana na hii ya leo. Wakati narudi Dar nikasema ngoja nijaribu kupanda BM coach, kwa kweli nimeinjoy sana kusafiri na BM, huduma nzuri sana na wahudumu wao wakarimu mno.

Kilimanjaro express msipobadilika na kufanyia kazi hizi kero za wateja wenu basi naweza kusema huu ndiyo mwisho wa zama zenu.
20220710_082718.jpg
20220710_082957.jpg
 
Hiyo kampuni hata kama hapo katikati ilikuwa inatoa huduma nzuri, niseme tu kwa sasa hiyo huduma wanayotoa sasa hivi ndio level zao. Kwa sie wahenga tuliosafiri mwanzoni mwa miaka ya 2000 tulikuwa tunaikwepa maana mnaweza kuishiwa mafuta njiani....enzi hizo kampuni ilikuwa inajulikana kama Kilimanjaro trucks au Sawaya

N.B. Kama taarifa ya kweli lakini maana kwa gari za Arusha kwa Kilimanjaro Express sio mbaya sana
 
Kuna hizi G7 kama sijakosea T 163 DMH ,T 165 DMH, T 622 DPT ...kama wangezitunza vyema ni bus kali sana kwa ndani na pia mwendo.

Niliwahi pata T 163 DMH mwaka jana.. Same tulifika saa Tano na robo na tukakalishwa hapo na Askari mpaka saa Saba.

Kuna huo uchuro wa AQN zile Marcopolo za miaka ile.. na wana uchuro mwingine wa BVN Yutong ya miaka ili siti fupi vibaya mno.
 
Tatizo la nchi yetu bado ni lilelile la kwenda na ulimwengu wa Analogia wakati dunia iko Digitali.

Mi nadhani wizara ya uchukuzi ingeanzisha utaratibu wa Application au vipeperushi ambavyo vinakuwa vinaonyesha mikoa husika na aina ya ma-bus yanayoelekea huko.

Kwa mfano:

MKOA WA KILIMANJARO

LUXURY BUSES NA HUDUMA NDANI YA BUS

1.TILISHO - AC,WI-FI, etc.

2.BM - AC,WI-FI,VINYWAJI VYA AINA ZOTE.......etc

3.KIMBINYIKO -..........................

SEMI LUXURY BUSES

1.TILISHO - AC,HAKUNA WI-FI etc.

2.BM - WI-FI,HAKUNA AC WALA VINYWAJI

3.KIMBINYIKO - ....................

Huo ni mfano tu nimetolea na hivyo nisieleweke vibaya.

Sasa nadhani hii itaondoa ukakasi wa wale wapiga debe ambao huwa wanawajaza maneno mengi ya faraja abiria na ukiingia kwenye bus unakuta ni vice vesa,pia serikali kupitia wanaosimamia hayo ma-bus au usafirishaji abiria,unapoenda kukata tiketi kuwe kuna ulazima yule mkata tiketi akupe kitabu kitakachoonyesha aina ya bus na huduma zitolewazo na wewe unapaswa kulipia kile utakachokipenda.
Ili ukishalipa hiyo tiketi na ukapandishwa gari isiyokuwa na hizo huduma basi urudishiwe pesa yako na pesa ya kufidia muda wako.

Kinachotugharimu abiria wengi ni kwasababu hakuna mahali ambapo naweza kuona maelezo au taarifa zinazohusu hayo makampuni ya buses na huduma zitolewazo.
Kumbuka hakuna abiria anayependa kusafiri kwenda umbali wa kilometa nyingi kwa usumbufu na kero.

Taarifa ziwepo kuhusu hayo ma-bus na gharama husika ili kila abiria ajikadirie kwa uwezo wa mfuko wake,siyo nakuja stendi kukata tiketi nakuta bus limeandikwa ubavuni "luxury" na ukishapanda unakuta ni vice vesa.

Hebu tubadilike,tuache huu ubabaishaji wa kipumbavu.

Wao ngoja waendeleze huu ujinga na waendelee kuomba SGR isikamilike,lakini ikikamilika na ikafanya kazi kama tunavyoaminishwa,kiukweli ruti za ma-bus zitapungua,kwasababu siwezi kukaa kwenye bus kutoka Dar kwenda Mza kwa saa 17 wakati treni ni masaa 8 mpaka 10 tu.
 
Back
Top Bottom