Rashda Zunde
Senior Member
- May 28, 2022
- 199
- 231
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imetangaza kufuta tozo tatu za miamala ya kieletroniki kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu.
Naipongeza serikali kwa kuwa sikivu na kuja na marekebisho yaliyowezesha kufutwa baadhi ya tozo. Aidha, naungana na wasomi na wabunge walioshauri kuangalia namna ya kuongeza wigo wa walipa kodi nchini, kwani ukweli ni wkamba wanaolipa kodi ni wachache kuliko wanaostahili.
Pia kama Watanzania tunapaswa kutambua kwamba hakuna nchi inayoendelea bila kutoza kodi watu wake hivyo tujitahidi kulipa kodi na tozo ili tupate maendeleo tunayoyahitaji.
Hata misaada inayotolewa na nchi washirikia wa maendeleo inatokana na kodi za wananchi wake, hivyo Watanzania wote wanapaswa kujenga utamaduni wa kulipa kodi ili fedha zake zitumike kuwaletea maendeleo.
Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe. Kazi Iendelee kwa sababu Mama Yuko Kazini.