Hongera sana Diamond lakini kwa hili hapana...

DavidHard

JF-Expert Member
Nov 4, 2011
428
500
Diamond haina haja ya kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na yote yakakosa ubora na ubunifu. Hiyo ni kutengeneza vitu vitakavyo ishi muda mfupi sana. Na ukweli unaujua kuwa watu wanapenda na ku support hivyo vitu vingi unavyovitengeza na kuvianzisha hata kama havina ubora. Si kwa sababu wanavipenda bali ni kwa sababu wanakupenda wewe.

Nitazungumzia kwa uchache hizi Show za Tigo tumewasha. Kwa ukubwa wake na wasanii wake tusingetegemea kuona picha mbovu kama zinazorushwa. Na achilia mbali ubovu wa picha WASAFI TV wameshindwa kurusha live matangazo yao..kwani yanakatika katika kila baada ya sekunde kadhaa.. Sound ni mbovu kupindukia. Swali langu hivi ni kweli bado wewe ni mchanga katika maandalizi ya hizi show kubwa.. ili hali hii ni awamu ya tatu unafanya hivi...tulitegemea kuona matangazo na show bora badala yake imekuwa kinyume.

..Upande wa Tv umekuwa ukikimbizana na watangazaji wakubwa lakini wakifika wasafi ukubwa wao unapotea na wanakuwa wa kawaida na wapiga kelele..utadhani sio watangazaji tunaowajua(Kitenge,joni joo. Kabla ya kuhama,omary tambwe)..Lakini vipindi vimekosa ubunifu hata kama ni tv na redio ya vijana..isimaanishe udaku bali weledi ambao umekuwa adimu hapo kwako.

Kwa ufupi fanya machache ama vitu vichache kwa ubora na ufanisi kuliko mengi yasiyo na ubora na kukosa ubunifu.. Walimu wanajua hili mwanafunzi aliyeandika kwenye karatasi tano mambo mengi yasiyo na maana ..basi atazidiwa na aliyeandika kwenye karatasi moja mambo yaliyo na maana.

Ni hayo kwa uchache.
 
Rukaka2020

Senior Member
Jun 20, 2020
102
500
Kiukeli kabisa mini ni Team Mond ila kwenye uwekezaji wa media zako hadi sasa naona hamna cha maana UBORA WA WASAFI TV ni wa chini sana hasahasa kwenye Live events.
yaani WBC LABELndio inaibeba Wasafi Media badala ya Media kuibeba LABEL,
Tatizo naloliona ni kuwa WAMEKAMIA SANA KUTAKA KUIFUNIKA CLOUDS kwa muda mfupi, sasa inakua too much
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
6,990
2,000

Hapo kwenye ubora wa Live hata Clouds wapo chini,yaani kwa kifupi quality zao zinafanana.

EATV pamoja hawafanyi Live Events nyingi wapo vizuri kuliko hao wawili.
 
BM X6

Member
Nov 24, 2020
43
150
Kiukeli kabisa mini ni Team Mond ila kwenye uwekezaji wa media zako hadi sasa naona hamna cha maana UBORA WA WASAFI TV ni wa chini sana hasahasa kwenye Live events.
yaani WBC LABELndio inaibeba Wasafi Media badala ya Media kuibeba LABEL,
Tatizo naloliona ni kuwa WAMEKAMIA SANA KUTAKA KUIFUNIKA CLOUDS kwa muda mfupi, sasa inakua too much
Uzee huu unatufanya tunapitwa na mengi, Kumbe kuna WBC Label!!!? Wacha nipakue Instagram niji-update kidogo
 
DavidHard

JF-Expert Member
Nov 4, 2011
428
500
Kiukeli kabisa mini ni Team Mond ila kwenye uwekezaji wa media zako hadi sasa naona hamna cha maana UBORA WA WASAFI TV ni wa chini sana hasahasa kwenye Live events.
yaani WBC LABELndio inaibeba Wasafi Media badala ya Media kuibeba LABEL,
Tatizo naloliona ni kuwa WAMEKAMIA SANA KUTAKA KUIFUNIKA CLOUDS kwa muda mfupi, sasa inakua too much
Shida ipo hapo anataka kufika walipofika jirani zake kwa haraka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom