Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,442
- 113,452
Wild Card,Pasco,
Sikatai unachokiongea hapa. Nifahamishe zaidi yafuatayo:
-Kwa nini taaluma hizi hadi leo hazina boards za kitaaluma kama vile NBAA ya wahasibu, ERB ya wahandisi,...
-Kwa nini mpangilio wa vyeo na madaraka haufati elimu ya mtu? Kwa mfano, AG au CJ alipaswa kuwa PhD holder ambao Tanzania hii tunao wengi tu.
Kutoa mfano wa watu kama Arnold Kileo haututendei haki Watanzania. TBL sasa hivi iko mikononi mwa nani? Aliisimamia hadi ikauzwa kwa bei ya kutupa kama NBC yetu kisha naye akajigawia hisa. Nadhani pia unaelewa mikataba mbalimbali tuliosaini kama NCHI ilikotufikisha.
Utaratibu wa kuupata uwakili, ndio professsional body ya taaluma ya sheria kwa mawakili, baada ya kuhitimu, huwi wakili hivi hivi tuu ndio maana inachukua muda kuupata, hili batch waliopata juzi, walimaliza UD, 2006. Mawakili wakifanya visivyo, pia huchukuliwa hatua za kunyang'anywa uwakili kama ambavyo baadhi wamesha vuliwa.
Hili la proffesionalism ni subjective, requirement ya kuwa wakili, jaji, mwanasheria mkuu, sio academic execelence, possession ya LL.B tuu pre-requisite na inatosha kumaliza kila kitu.
Hii ni sawa na bodi za kitaaluma za madaktari, kupata sifa ya kuitwa daktari, ni kupa MD tuu, hizo specialization ni ziada na sio lazima.
Wanasheria wazuri na waliobobea wanahitaji zaidi burasa na uzoefu tuu na sio mavyeti ya taaluma za juu, hivyo sio ajabu kukuta pale mlimali, wanasheria vichwa wenye 1st Class kama Prof. Kabudi, ambao ni mabingwa waliobobea kwenye sheria, ndani nje, kamsimamishe Kabudi Mahakamani!, matokea ndio yale ya ushauri kuhusu mgombea binafsi alioutoa na CJ kuukubali na kuufuata na matokeo ndio yale.
Kuwa mwanasheria mzuri, hakuhitaji masters, kwa maoni yangu, hapa Tanzania, bado hatajapata wakili mahiri kwa kiwango cha Murtaza Lakha, huyu alijipatia LL.B tuu kwisha biashara, arguments zake na reasoning power yake ilikuwa juu sana. Ndiye alisimamia zile kesi za Mauaji Mwanza. Mauaji Shinyanga na Kesi ya Uhaini ya 1982 akiwatetea mshitakiwa wa kwanza , Pius Lugangila na Mshtakiwa wa Pili, Hatty McGhee, japo walitiwa hatiani, cha moto serikali ilikipata. Hata wakili mwenye mafanikio makubwa kabisa kuliko wakili mwingine yoyote Tanzania in terms of resources, Nimrod Mkono, alipata just a Pass na hana Masters ya sheria mpaka kesho, and is doing fine, wakati Ma Ph.D sheria, wanajaza tuu masheflf pale mlimali na mareaseach yao yasiyofanyiwa kazi.
Tukubali tukatae, sheria ni fani adhimu ukiwaondoa wendawazimu wachache wanaotaka kuichafua.