Kenya 2022 Hongera Rais wetu mpya, Dkt. William Ruto

Kenya 2022 General Election
Yeah! Moi hakumtaka, if I remember well he fought off the then MP Mr. Chesire, he is a true hustler, my problem with him is that his name has featured in almost every major scandal.
Ikifika ni projects na utendakazi sioni kama Ruto atawahi fikia Uhuru. Jamaa amezungukwa na Ufisadi tupu. We probably won't be able to post mile stone development projects here again. Kila kitu itasimama.
 
Kama Raila mwenyewe alisema ataheshimu maamuzi ya Mahakama wewe ni nani hadi u question Mahakama yao ? Unaishi Dunia nyingine, eti wamuombe Kikwete ungejua hata kumjua siajabu hawamjui wala usingemtaja, hakuna watu Wakenya wanawadharau kama Watanzania hilo labda hamjalijua tu bado vinginevyo msingejipendekeza hivyo kwa kwa watu ambao wanawadharau.

Jinsi ambavyo unavyofikiria sivyo wanavyokuona, unajidanganya sana.

Pigeni magoti tena Ikulu kumuomba na Ruto msamaha!
Kenya wanadharau Watanzania?? bro calm down na upate glass moja ya maji baridii akili itulie. Naona na wewe inaleta mipasho ya TickTok na Twitter humu!
 
Ikifika ni projects na utendakazi sioni kama Ruto atawahi fikia Uhuru. Jamaa amezungukwa na Ufisadi tupu. We probably won't be able to post mile stone development projects here again. Kila kitu itasimama.

Let's be positive and hope for the best, make it easier for him because every decision he will make will impact each one of us in every possible way. I didn't want him, I considered him the most corrupt leader among them all, but he is now at the helm, our president....let's just go through it all, help him where possible for our posterity.
 
Hongera zake Rais wetu mpya Dkt. William Samoei Arap Ruto. Ingawa sikutoa ushirikiano wowote, kwenye azma yake ya kuwa rais wa taifa letu tukufu la Kenya. Wala sikuunga mkono wapinzani wake RAO, Wajackoyah na Mwaure ila mwisho wa siku aliibuka kidedea na jambo hilo linastahili pongezi.

Wakati wa kampeni za uchaguzi nilisikiza hoja za pande zote kwa umakini mkubwa. Nikafuatilia mienendo ya wagombea wote wa kiti cha urais na maamuzi niliyoyafikia ni kwamba wote walikuwa ni matope tu. Hakuna ambaye alinishawishi kwamba alistahili kupata kura yangu na sikutia mguu wangu ndani ya kituo cha kupigia kura.

All in all, the whole exercise was a great illustration that true democracy has come of age in Kenya.
 
Japo sikukupigia kura, na binafsi haujanishawishi ila Wakenya walio wengi walifaulu kukuchagua, inabidi tukubali maamuzi ya wengi ila tulio wachache tusiklizwe pia.

Nakumbuka kitambo nikiwa kijana, nilikua mmojawapo wa vijana tuliokusanyika pale Eldoret kukushangilia siku ya kwanza ulipotangaza kuwaania ubunge kwenye jimbo letu la Uasin Gishu, na umepambana mpaka leo umeukwaa urais, sina budi ila kukupa hongera.

Tawala taifa letu kwa misingi ya haki, heshimu katiba, endeleza miradi yote aliyotanguliza mwenzako, pambana dhidi ya ufisadi (japo hili la ufisadi nina mashaka nalo maana ndio sababu kuu sikukupigia kura, majina yako yametajwa sana kwenye tuhuma za ufisadi).

Wengi tutakuunga mikono, tutasimama na wewe kizalendo na kuendelea kuboresha nchi yetu, huu waraka najua hautausoma ila inawezekana wapambe wako wakapitia humu.

Big up sana William, tusonge mbele kwa mbele!!!!

Na pia shukrani za dhati ziwafikie IEBC kwa namna waliendesha huu uchgauzi, mumeweka rekodi mpya Afrika, tupo kwenye level nyingine, kwamba leo hii hata muungano na EAC kuwa nchi moja itashindikana maana labda tujishushe.

Hatimaye hongera kwa walioshinda viti vingine vyote na hata walioshindwa, sote tuboreshe taifa letu.
Ujumbe wako kwake Mh Ruto ni mzuri sana Mkuu..
HONGERA.
 
Mk 254 naomba unijuze hawa cabinet secretaries wanapatikaje. Je ni lazima wawe wabunge au rais anachagua tu
 
Mk 254 naomba unijuze hawa cabinet secretaries wanapatikaje. Je ni lazima wawe wabunge au rais anachagua tu
kikatiba hawatakiwi kuwa wabunge,...... kule mawaziri sio sehemu ya bunge wala hawatakiwi kuwa wabunge
 
Hongereni sana Wakenya, mnaonyesha njia katika ukanda huu.
 
Wewe naye unaandika upupu mtupu, Watanzania waombe msamha kwa Ruto kwa sababu zipi hasa??
Tanzania ndio inalisha Kenya, Rwanda na Burundi kwa asilimia zaidi ya 70%.
Ngoja tuone Wabongo watakavyonza kujipendekeza kwa Ruto kuanzia utosini mwao mpaka miguuni kama kawaida yao kujipendekeza kwa winners, muda si mrefu watapiga magoti ikulu kumuomba msamaha Ruto full kujidhalilisha, uzuri ni kwamba Ruto hana mpango na Tanzania na sijui hata kama keshawahi kufika, huyo yuko na Uganda.

Anyway laana aliyopigwa Uhuru Kenyata na Mungu itafika Bongo soon, hata huku ana watu wake pia siyo Raila tu, Mungu yuko fair siku zote.

Uhuru nenda zako, pure evil!
 
Wewe naye unaandika upupu mtupu, Watanzania waombe msamha kwa Ruto kwa sababu zipi hasa??
Tanzania ndio inalisha Kenya, Rwanda na Burundi kwa asilimia zaidi ya 70%.

Kwani Uhuru Kenyata aliombwa msamaha ndani ya Ikulu ya Tanzania kwa sababu zipi?
 
Back
Top Bottom