Hongera nyingi sana kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Amos Makalla, umeweza

Naomba niungane na wana DSM wengine kumpongeza mkuu mkoa kwakweli umeweza unastahili nishani na pongezi ilikuwa sio kazi nyepesi kurudisha jiji katika hali yake baada jiji kuwa ovyo kabisa.

Sasa Dar inawaka Manzese leo unaangusha sindano unaiona kongole kwa timu nzima ya mkoa.

Ila ushauri muwashirikishe ngazi ya chini kama wenyeviti Serikali za Mitaa ili kusimamia kila mtaa wake vibanda visirejee tena maana watanzania tuna mambo ya kujaribu jaribu ataanza mmoja tu wengine wakiona kimya wanarudi kama mwanzo.

Hongera sana RC Makalla

Wako
Mwanadar es salaam
Kwa hili nampongeza sana Mheshimiwa Makala. Jiji lazima liende na hadhi yake.
 
To be honest, nilimbeza Makalla, nilisema hataweza kuondoa wamachinga, smenishangaza kwani zoezi limefanyika kwa amani na upendo na jiji limependeza.

Ushauri wangu;
1. Makalla awaite aongee nao watoe madukuduku yao ili kupunguza mukari usijelipuka baadae..na awasikilize changamoto mpya.

2. Samia naye aitikie wito wao na kukaa nao kama wanawe, awatiw moyo kuvumilia makazi mapya na aahidi kuwasaidia, hapo atawaweza
Kaishawapa 5 bilioni

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Sasa, kama kweli tumedhamiria kutakatisha jiji, na wenye fremu/maduka wapigwe marufuku kusambaza vitu nje ya fremu zao. Kwanza, ni mbaya kiafya. Bidhaa zao nyingi ni zile haziendani na mwanga wa moja kwa moja wa jua (huandikwa, store in a cool dry place). Kuziweka nje ni kuhatarisha maisha ya watumiaji/wateja. Pili, kutaleta muonekano mzuri wa hizo barabara. Wengi wanateka hadi sehemi za kupita.

Kupiga marufuku, kutaonesha wazi zoezi halijalenga kuumiza kundi fulani bali mmedhamiria kurudisha hadhi ya jiji.

sambamba kabisa na kuvunja nyumba duni ndani ya jiji.
IMG_1865.png
 
Back
Top Bottom