kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,746
Sina budi kumpongeza Mbowe kwa namna ambavyo amekuwa akieendesha Chadema kama kampuni yake.
Katika kipindi cha uchaguzi zipo habari zilinea kwenye baadhi ya vyombo vya habari ikisemekana kwamba Mbowe amepokea sh. 12 bilioni kutoka kwa Lowasa
Ili kumruhusu Lowasa agombee nafasi ya rais kupitia chama cha Chadema na bila ya shaka yeyote na wote tunafahamu Lowasa aligombea urais kupitia chama hicho cha Chadema.wala hakuna aliyehoji.
Baadaye kidogo zikaenea habari zingine kwamba Mh. Mbowe amehamisha mamilioni ya pesa kutoka Dubai kwenda kwenye kampuni zake ambazo zipo China.
mara hii tena hakuna aliyehoji.
Tukiwa katikati ya kampeni chama chetu Chadema kikaitisha harambee ya kuchangia pesa za uchaguzi pale Mlimani City na kukusanywa pesa nyingi tu ambazo hatukuambiwa idadi yake. Pia hakuna aliyehoji.
Pamoja na matukio haya yote Mh. Mbowe hakukanusha wala kutoa ufafanuzi juu ya taarifa za matumizi mabaya ya pesa ya chama.
Hapa naanza kupata mashaka hivi Chadema ni chama cha wananchi kweli au ni mali Mbowe? Maana kila analolitaka hakuna anayeweza kupinga.
Naomba kuwasilisha jamvini.
Yaani nchi kuwa na mijitu kama wewe ndio maana hatuendelei ebu tafakari kwanza ulichokiweka na matukio kama haya ninayoya orodhesha hapa chini halafu uniambie hilo la Mbowe na haya ni yepe yaliyosababisha hali hii tuliyonayo
1. Wizi kupitia KAGODA na MEREMETA
2. Wizi kupitia RICHMOND ambayo hadi leo TANNESCO wanalipa fedha baada ya ukoo fulani kubadilisha kampuni hiyo kutoka RICHMOND kuwa DOWANS na sasa SYMBION POWER huku mkuu wa kampuni hiyo akimpokea kwa mbwembwe Obama na kumpeleka kukagua mitambo hiyo na kuisifia.
3. Wizi kupitia ESCROW
4. Wizi kupitia utoroshaji wa makontena bandarini na tumesikia hadi Meri nzima zilipotezwa
5. Gesi kuuziwa waCHINA na kuichimba kwa kipindi cha miaka 7 huku wakiiuza kwa wazalishaji umeme na wao kuuza umeme huo kwa TANNESCO na hao TANNESCO kutuuzia sisi.
Yaani wewe hayo mambo ya kubuni na majungu juu ya mbowe ndio umeona mambo ya msingi na kuyaacha haya ambayo yanakuangamiza wewe moja kwa moja na vizazi vyako NYAMBAAFUU!