Wakati mwingine nahisi kama kuzaliwa tu mtanzania tayari unakuwa na matatizo!! Sehemu ya ubongo inakuwa dormant. Hivi inaingia akilini kweli mtu apewe bilioni 12 kwa ajili ya kumruhusi agombee uraisi kupitia CDM? Wewe ungekuwa na mashine ya kufyatulia hela nyumbani kwako ungetoa hela zote hizo kirahisi hivyo? Ok, Mbowe amepewa bil 12, Dr. Kapewa ngapi? au amekataa ngapi?. Labda Kidogo ingeingia akilini kama ningemsikia Slaa akinena alipewa bil 1 au 2 amekataa. Hivi huoni kama ilikuwa muhimu hiyo hela hata bil 2 tu angenyamazishwa Slaa? Slaa alipokuwa anahoji Lowasa kaja na nini angeambiwa kaja na hela, kwani asset manake nini? Hivi inawezekana kufanya dili kubwa kiasi hiki na mtu 1 tu?. Hebu tujiulize, afisa wa ikulu katumbua pesa na demu hotelini Arusha laki 8 kutekenywa lisiti za malipo tumeziona, ufisadi unaotokea na marisiti yanaanikwa? Huyu Lowasa alimpia Mbowe pesa kwenye kitunga? Malisiti ya serikali yaonekane, masandarusi Escrow na mikokoteni, vikatuni vilichorwa ya Escrow tumeyaona, kwanini ya Mbowe yasionekane?