Hongera Makonda, umeonesha njia!

Hongera Makonda, umeonesha njia!

SIMBA NYANI

Member
Joined
Dec 8, 2014
Posts
35
Reaction score
25
Wadau,

Baniani mbaya kiatu chake dawa! Pamoja na maneno ya kejeli yalitolewa kwa Paul Makonda wakati anateuliwa kuwa mkuu wa wilaya, lakini ameonesha kuwa ni mweledi na anaijua kazi.

Leo kawaita vijana waliomaliza vyuo na kujadiliana nao kuhusu tatizo la ajira, ambapo vijana wameambiwa wajikusanye katika vikundi vidogo vidogo kulingana na fani walizozisoma, wabuni miradi halafu wataunganishwa katika taasisi za fedha kupewa mikopo. Huu ni mfano mzuri kwa viongozi vijana.

Big up Makonda!
 
Mkuu, idea aliyoitoa ni nzuri lakini wasiwasi wangu asije kuwatumia kisiasa tu maana Makonda anajulikana kwa kutumia fursa. (Kupanda kisiasa kupitia jobless).
 
Wazo liwe endelevu.....isije kuwa kama ile michuano ya coca cola ya watoto ya kuvumbua vipaji
 
asingefanya hivyo mngesema hakuwahi hata kujaribu kuzungumza na vijana, sasa huyu amejaribu mnatoa maneno ya kukatisha tamaa. huenda ana moyo wa kusaidia msaidieni awasaidie na sio mnatoa maneno mengi haliyakuwa ninyi hamna msaada wowote kwa hao vijana...
 
hivi hizo taasisi za fedha zitatoa mikopo bila masharti na yeye makonda atawadhamini na nini maana hakuna taasisi ya mikopo zinazofanya,siasa wapo kwa ajili ya kutengeneza faida kuwakusanya mainjinia kuwaambia waunde mradi Je kuna taasisi itawapa mkopo kwa mradi unaoendana na fani yao kuna mambo mengi hata mama zetu walipoletewa vikoba walikuwa na mitaji yao haikuwa bure
 
Kawasaidia kuwafanya wajitambue, maana wengi wanadhani ajira ni mpaka uajiriwe serikalini...
 
wabongo hawana jema amefanya hivyo wanatoa kasoro je asingefanye hivyo asingedaiwa na mtu naona watu kama Makonda waungwe mkono kiukweli ameonyesha njia....Keep it up DC Makonda
 
Hakuna taasisi ya fedha itakayowapa fedha hao vijana, kamwe!

Makonda anawatumia kisiasa huku akijua hakuna namna wanayoweza kupata fedha kutoka taasisi hizo!
 
Idea yake imekaa vizuri ila kwa hiki kipindi cha mpito wa kuelekea uchaguzi bachela kutuachia katikati ya deep sea tukitamalaki bila kuwa na hata boya la kutuokoa hapo badaee
 
Kinadharia unaweza kufikiri linawezekana ila kivitendo sio jambo jepesi.....
 
Kinadharia unaweza kufikiri linawezekana ila kivitendo sio jambo jepesi.....

Mkuu, nimemwambia taasisi za fedha haziko kisiasa, nani atawadhamini hao vijana watapata wapi pesa za kufungulia account ya kikundi pesa za usajili Wa kikundi na mengineyo bado akuna taasisi ya pesa itakayotoa mkopo kwa kikundi kisichokuwa na uzoefu nani atawadhamini hawa vijana makonda hana Mali za kuwadhamini anataka kuwatumia kisiasa tu na siku zote wapenda sifa ndio wanavyofanya
 
Mkuu, nimemwambia taasisi za fedha haziko kisiasa, nani atawadhamini hao vijana watapata wapi pesa za kufungulia account ya kikundi pesa za usajili Wa kikundi na mengineyo bado akuna taasisi ya pesa itakayotoa mkopo kwa kikundi kisichokuwa na uzoefu nani atawadhamini hawa vijana makonda hana Mali za kuwadhamini anataka kuwatumia kisiasa tu na siku zote wapenda sifa ndio wanavyofanya

Naona ni mandalizi ya ubunge jimbo la Kinondoni...
 
Naona ni mandalizi ya ubunge jimbo la Kinondoni...

Kabisa, hakuna jingine yeye mwenyewe ni mwajiriwa wa serikali anawambiwa watu wajikusanye waandike mradi kwa fani zao atawasaidia kupata mkopo kama mikopo ungekuwa ni kuandika mradi tu watu wengi wangekuwa wanapata yeye afanye siasa zake aache kuwadaha Watanzania
 
Hahaaa! Hawamjui vizuri Makonda hao, Makonda ni bonge la tapeli, Mimi ninamjua vizuri sana Makonda anapenda sana sifa za kijinga na kuwatumia vijana wenzake kama ngazi na mtaji wake wa kisiasa, Very Opportunistic, Double agent na Mnafiki sana.

Kwa mfano
Maonda wakati akiwa pale MUCCoBs(chuo cha Ushirika Moshi) Makonda alijiingiza mpaka kwenye issue za kidini, akijifanya bonge la mlokole na karibu kila baada ya miezi miwili au mitatu akiandaa bonge la Tamasha la Gospel, bahati mbaya sana wachache walimshtukia haswaa baada ya kuhoji anapata wapi pesa za kuandaa hayo matamasha na matamasha yote hayo wageni waalikwa wakuu ni makada wa CCM akiwemo Samwel Sitta, Mwakyembe nk. Baadaye alipogundulika anafanyakazi na TISS na baadhi ya vitengo vya siri vya CCM(chini ya uratibu wa Yusuph Makamba) akafanikisha vyuo vyote vikuu vilivyopo Kilimanjaro vinakuwa na matawi ya CCM, Then akapotea kabisa chuo then akarejea baada ya 2years akiwa amechoka sana kuja kumalizia masomo.

Hao vijana wawe very careful na Makonda, jamaa anatafuta Gear ya kupata Ubunge Hapo Kinondoni nk.
 
Back
Top Bottom