Hongera RC Makonda kwa hili la madawa ya kulevya

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kwenye hili jambo la Madawa ya kulevya vuta soksi, weka pembeni siasa piga kazi maana hii vita si ya kitoto, kuna kitengo cha polisi cha kudhibiti madawa ya kulevya nchinj lakini kiko kimya. Wewe umeamua mwenyewe kufanya kazi pamoja na uwepo wa kikosi hicho.

Kwenye hili binafsi nakuombea dua kwa Mungu kwa kiroho safi kabisa brother, ninakuunga mkono 100% na nikuombe tu uwe makini na usalama wako binafsi maana mtandao wa makundi ya Madawa ya kulevya sio ya watu wadogo, ni watu wenye mapesa mengi machafu.Na ni watu wenye jeuri ya hali ya juu kutokana pesa zao hizo.

Mungu akuongoze vyema usikatishwe tamaa na mtu, jitoe muhanga kuwaokoa Wananchi hasa vijana wanaoangamia na janga hili, nalisema hili kwa uchungu kabisa maana ndani ya familia yetu tumeharibikiwa na vijana tuliowapenda na sasa wapo walishaathiriwa na Madawa ya kulevya yaani wamekua kama si binadamu, utu wao sio Kama wa zamani.

Umelianzisha nadhani kuna wenzako wa mikoa mingine watafanya hivyohivyo! Huku Arusha hakufai vijiwe ni vingi mno na RC Gambo aige mfano kwako.

Kila laheri brother, funga mkanda! Mungu pekee atakulinda.

Tangu kuteuliwa kwa Paul Makonda kuwa Mkuu wa wilaya ya kinondoni na baadae kupandishwa cheo kuwa mkuu wa mkoa wa Dar kijana Paul Makonda ameonyesha kipaji cha hali ya juu sana katika kufanikisha maendeleo na kubuni mambo mbalimbali katika maeneo yake ya utawala.

Makonda akiwa Mkuu wa wilaya ya kinondoni aliendesha zoezi la kutafutia ajira vijana waliomaliza vyuo na kukaa majumbani kwao bila ajira.

Alibuni pia namna ya kushirikiana na wadau mbali mbali katika wilaya ya kinondoni kutatua tatizo la uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa ambapo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kuna wakati flani Paul Makonda akiwa Dc kipindi cha utawala wa Rais mstaafu J.Kiwete alifanikisha kuzima na kutatua kabisa mgogoro wa Madreva nchini.

Juhudi na ubunifu wa Makonda haukuishia hapo ameendelea kubuni mambo mbali mbali ata alipofanikiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es saalam.
Sote ni mashahidi katika hili.

Mara baada ya kuapishwa kuwa Rc wa Dar Makonda alifanya mpango wa kutengeneza magari mabovu katika ofisi yake ( ofisi ya Rc).

Ameendelea kubuni mambo mbalimbali ikiwemo suala la usafiri kwa walimu ,kutafanya mikutano ya ana kwa ana na wananchi na kushughulikia kero zao .
RC MAKONDA ameenda mbali zaidi katika udhubutu wake na kuingilia kati suala la wafanya biashara watumiaji wa madawa ya kulevya.

Katika hili Rc Makonda amedhubutu kuwataja hadharani watu mbali mbali wenye itikadi tofauti tofauti za kiasiasa.wengine wakiwa wana CCM wenzake.

Katika kufanya mambo haya yote Rc Makonda amekuwa mtu wa kusemwa kutukanwa na kudharirishwa mitandao lakini kikubwa uwa ajishughulishi kuwajibu wale wote wanaomfanyia hivi bali yeye amekua akijizatiti kwenye kile alichokianzisha.

Sifa hii ndio sifa kubwa inayomfanya Makonda asonge mbele licha ya kukatishwa tamaa na watu mbalimbali.

Hii ndio sifa ya kiongozi bora.

Usema ukweli nchi yetu ingekua na wakuu wa mikoa karibu wote wa aina ya Makonda nchi yetu ingeamka sana.

Heko heko kwa viongozi wote nchini wakubwa kwa wadogo kuwa wabunifu na kufatilia matatizo mbalimbali ya wananchi katika sehemu zao.

Heko Heko Paul Makonda,Mungu aliekuinua hawezi kukushusha mpaka kusudi lake litimie.
 
Nimejaribu kupitia sehemu mbali mbali mtaani na mitandaoni hasa hii ya kijamii juu ya suala hili la kijasiri la kuwataja watuhumiwa hadharani mh Makonda amepongezwa sana, wengi wameenda mbali na kushauri kuwa apewe wizara kabisa, hata wale wa upinzani wamempongeza na kusema kuwa ni kitendo cha kijasiri sana, Hongera mheshimiwa RC Dar.
 
Nimejaribu kupitia sehem mbali mbali mtaani na mitandaoni hasa hii ya kijamii juu ya suala hili la kijasiri la kuwataja watuhumiwa hadharani mh makonda amepongezwa sana, wengi wameenda mbali na kushauri kuwa apewe wizara kabisa, hata wale wa upinzani wamempongeza na kusema kuwa ni kitendo cha kijasiri sana, Hongera mheshimiwa RC dar,
Hiyo ya watu wote imetoka wapi? Utapongeza usanii na ndo maana kawataja wasanii unataka kusema wauza unga mashuhuri Ni wasanii na baadhi ya maaskali? Ndume zenyewe zipo wasituletee usanii hapa.
 
Nimejaribu kupitia sehemu mbali mbali mtaani na mitandaoni hasa hii ya kijamii juu ya suala hili la kijasiri la kuwataja watuhumiwa hadharani mh Makonda amepongezwa sana, wengi wameenda mbali na kushauri kuwa apewe wizara kabisa, hata wale wa upinzani wamempongeza na kusema kuwa ni kitendo cha kijasiri sana, Hongera mheshimiwa RC Dar.
Na,uunga mkono pia na angefaa kuwa kiongozi endapo angeweza kuheshimu wengine lakin anakosa sifa hiyo pekee,anakiburi cha mamlaka kitu ambacho kinamnyima sifa ya kuwa kiangozi na kupewa madaraka zaidi ya hayo ,labda kama ataendela kujifunza na akafunzika kweli hapo baadae anaweza kutufaa zaid.
 
Nimejaribu kupitia sehemu mbali mbali mtaani na mitandaoni hasa hii ya kijamii juu ya suala hili la kijasiri la kuwataja watuhumiwa hadharani mh Makonda amepongezwa sana, wengi wameenda mbali na kushauri kuwa apewe wizara kabisa, hata wale wa upinzani wamempongeza na kusema kuwa ni kitendo cha kijasiri sana, Hongera mheshimiwa RC Dar.

Big up paul chapa kazi .
 
KWENYE ANAYEPINGA NI MBUYA UNGA TUUUUU
 
Makonda umeshakuwa Mkuu wa mkoa lkn bado una akiri za ki Uvccm.unakuja na Ids gake kujisifu.hakuna mtu anayemsifia Makonda kwa Dar Sisi watu wa Dar Makonda tunamuona kituko hivi kweli Wema yule mtangazaji wa Clouds Chid benz Tid ndio wauza unga kweli?.Makonda usitufanye wajinga sisi mkuu twambie mkoa wako kwa nini una shule 6 za mwisho usiyeyushe acha usanii.hakuna anayekusifu
 
Back
Top Bottom