Dar: Mapokezi ya ndege ya pili ya ATCL aina ya AirBus A220-300(Ngorongoro) katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere


Roving Journalist

Roving Journalist

Senior Member
Joined
Apr 18, 2017
Messages
199
Likes
1,629
Points
180
Roving Journalist

Roving Journalist

Senior Member
Joined Apr 18, 2017
199 1,629 180
Rais Magufuli leo anatarajia kuongoza watanzania kupokea ndege nyingine ya sita aina ya Airbus A220-300, inayowasili hapa nchini ikitokea nchini Canada, na kufanya idadi ya ndege zilizonunuliwa katika kipindi cha awamu ya tano kufikia 6.

UPDATES; 1520hrs

=> Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 iliyonunuliwa na serikali yatua uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar muda huu. Rais John Magufuli, viongozi waandamizi, viongozi wa dini na wananchi wajitokeza kuipokea.

=> Askofu Kakobe: "Hata ungefanya kitu gani huwezi kusifiwa na Watu wote na MUNGU anasema kama utasifiwa na Watu wote basi ni ole wako, tumekusanyika kwa ajili ya ndege za ATCL ni jambo zito na kubwa lakini usitarajie Watu wote watakusifu, wengine watakusifu ukifa"
fb_img_1547218887609-jpg.991910

“Mheshimiwa mimi huwa ni mbishi kidogo…na ukiona nimekuja mahali kama hapa…ujue umenikosha,” – kauli ya Mchungaji wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe akikiri kukoshwa na Rais

Kakobe amsihi Rais Magufuli alale. “…Umewahi kutuambia unashindwa kulala kwa sababu kitanda kimejaa mafaili…lakini leo tunakusihi…hebu jipongeze ulale…” – kauli ya Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe.

Paul Makonda: Mh. Rais naomba niruhusu kwa leo nikupe salamu tu kwa kuwa furaha yangu imezidi

> Pokea salamu kutoka kwa Mwl. Christopher Mwakasege. Anakupongeza kwa jambo kubwa unalolifanya ila ameshindwa kuja yupo Tukuyu kwa jambo la kifamilia.

Paul Makonda: Nilipotoa tangazo la kuja hapa nilisema waje wale waliowahi kutoa ahadi na wakatekeleza.

> Tumekuja kukuunga mkono kwa kuwa ulitoa ahadi kutoka kwenye ilani ya CCM na unatekeleza ikiwemo elimu bure

Paul Makonda: Hivi ulivyo Rais wetu angekuwa mwingine watoto wake tungekuwa tunagombana nao mtaani lakini wewe umehakikisha hakuna anayeingilia jukumu lako kama baba wa familia. Nikikua nataka niwe kama wewe

Akizungumza katika mapokezi ya ndege aina Airbus A220-300 hapa uwanja wa ndege, RC Paul Makonda amewataka viongozi wa Dini kumuombea juu ya ndoto yake ya kuwa kama Rais Dkt Magufuli.

Serikali imesema Ndege mpya iliyopokelewa leo aina ya AIRBUS A220-300 NGORONGORO itakuwa na safari za kila siku kwenda Dodoma kuanzia January 16 mwaka huu tofauti na ilivyo sasa ambapo ATCL hufanya safari 4 tu kwa wiki kwenda Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji ATCL Ladislaus Matindi: Ujazo wa ndege hizi 2 za Airbus unatuwezesha kutoa huduma kwa Mkoa wa Mtwara na mikoa yenye viwanja vidogo

> Ndege hizi zote zina uwezo wa kubeba tani 19 na tayari tumefanikiwa kuingia kwenye makubaliano ya kusafirisha nyama ya mbuzi

Matindi: Tayari tunashirikiana na ubalozi wa Uingereza ili kuwakutanisha wadau wa usafiri wa ndege kuweza kujadiliana na kukubaliana kuhusu fursa zilizopo kwenye shirika la ndege
fb_img_1547214211302-jpg.991911

Matindi: Baada ya kurudisha kwenye mfumo wa tiketi duniani kazi ya kuunganisha ATCL kwenyw mfumo huo inategemewa kuwa imekamilika Januari hii.

> Tunatazamia pia kutoa huduma kwa wateja kwa saa 24 kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kilichopo kwenye matengenezo

Matindi: Kufika kwa ndege hii kunahitimisha mkataba wa ununuzi wa ndege mbili za Airbus A220-300, ndege hizi zinatuwezesha kuwa na upanuzi wa mtandao wa safari zetu na kutoa huduma za kimkakati katika soko la Kusini mwa Afrika

Ladslaus Matindi: Katika safari ya ndege hii tulikuwa na Kapteni Khamisi, Kapteni Msingi na aliyeiteremsha ndege hapa nchini ni Kampteni Budodi na kiongozi wa safari alikuwa ni Kapteni Patric anayetoka kwenye kampuni iliyotuuzia ndege na atakuwa hapa kwa miezi 3 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana wetu

Waziri Mkuu Majaliwa: Jambo hili ni kubwa sana na tunaamini wafanyakazi mtafanya kazi kwa weledi na kuendelea kuliinua shirika letu na ukitaka usafiri mzuri safiri na Air Tanzania

Mhandisi Isack Kamwelwe: Nakupongeza Rais wangu kwamba uliweka nia na ukaagiza tununue ndege 7 na zimenunuliwa ambapo Oktoba mwaka huu inaingia ndege nyingine na juzi umeniambia tununue ndege nyingine tena

Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson: Sisi kama Bunge tunakupongeza Rais kwa kazi kubwa unayoendelea kuifanya, sote ni mashahidi kwa kinachoendelea, ulipokuja bungeni kusema utanunua ndege hatukuamini lakini kama matani tunazo ndege Sita

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa na ninawashukuru sana viongozi wa dini, wamemaliza maneno mazuri ambayo tulitakiwa kuyazungumza hapa. Endeleni kuliombea taifa hili

Mafanikio ya ndege hizi 6 ni shuhuda tosha wa nguvu za watanzania hivyo watanzania hongereni sana.

Ndege hizi ni zenu, hakuna hata senti 5 iliyotoka kwa mfadhili kununua ndege hizi. Mfadhili ni mtanzania.

Ukangalia nchi zingine utakuta ndege zina "percent" kubwa inayomilikiwa na watu wengine hata kama zina majina ya nchi hizo lakini Tanzania Air Tanzania inamilikiwa na watanzania 100%.

Napenda kutoa wito kama pesa imepangwa ikanunue ndege basi ikanunue ndege

Kwa taarifa yenu kitendo cha ndege hii kuchelewa hiyo kampuni imetulipa hela dola milioni 1.3 na wameandika "cheque" na wanairudisha pesa Wizara ya fedha.

Hiyo ndiyo Tanzania ninayoitaka mimi, Tanzania ya ukweli na uwazi

Na walipokuwa huko niliwaambia hakuna kuacha cheque huko waje nayo ingekuwa miaka mingine hizo pesa zingebaki huko na kuliwa hukohuko

Tunafanya kazi kwa mapenzi makubwa kwenu watanzania na ni kwa watanzania wote, vyama vyote, makabila yote na dini zote maana maendeleo hayana vyama

Nimesikia wito wa Kakobe kwamba wao wanavyokutana na sisi wanasiasa tuwe tunakutana lakini shida kubwa huwezi ukawa unakutana na mtu anakutakana tukana hovyo kwamba uchinjwe ufie huko

Hakuna nchi duniani iliyofanikiwa kwa kupewa misaada. Ninawaambia watanzania wenzangu, itafuteni hamtaipata

Ili nchi ifanikiwe lazima ijitegemee na saa nyingine ukipewa misaada sana inakulemaza.

Tunahitaji misaada sana lakini iwe ya kutufanya tuweze kusimama na tunahitaji ushirikiano kutoka nchi zingine lakini lazima iwe ya kumuwezesha mtanzania kujitegemea

Pia tunahitaji wawekezaji kutoka nchi zingine

Katika kipindi ambacho ndege zimeanza kununuliwa tayari wafanyakazi 380 wameshaajiriwa, hivyo ununuzi wa ndege hizi umegusa maisha ya Watanzania

Ndege hii tuliyoipokea leo sio ya mwisho, mwishoni mwa mwaka huu tunategemea kuleta ndege nyingine aina ya Dreamliner itakayobeba abiria 262

Tunataka baada ya miaka 10 au 20 Tanzania tuwe na ndege hata 100, tushindane na mashirika mengine makubwa duniani,Tanzania tunaweza

Na nyie ATCL punguzeni matumizi mabaya. Kuna wakati ndege ilikuwa inaenda Dubai kuchukua nguo kwa ajili ya maduka ya watu Fulani Fulani

Hizi ndege mmeazimwa. Ni sawa na koti, wameazimwa. Wakifanya ovyo, tunawanyang'anya. Tunaweza hata kuwapa Precision

Nashukuru sana Bunge. Mheshimiwa Spika, Naibu, wenyeviti wa kamati na wabunge kwa kupitisha manunuzi ya ndege hizi. Nawapongeza sana wabunge wa CCM

Napenda sana kukipongeza chama changu hasa Katibu Mkuu Dkt.Bashiru Ally amekuwa muwazi sana

Ndege hizi za Rais ambazo ziko tatu, mbili zitapakwa rangi ya Air Tanzania zikabebe abiria siku ambapo hazibebi huku kwetu zikabebe abiria, Rais kwanza sitembei sana

Kwa miaka 8 tulikuwa hatujapa gawio kutoka Airtel.

Leo amekuja Chairman wa Airtel na kakubali hisa zao zishuke. Wakipiga hesabu vizuri wataanza kutoa gawio

Tanzania itakuwa Ulaya. Niamini. Nawaomba Watanzania kila mmoja aamini hivyo.

Haya yaliyopatikana ndani ya miaka mitatu ni rasharasha. Mvua zinakuja

Nimpongeze kijana huyu Mwenyekiti wa ATCL alikuwa anafanya kazi nchini Senegal alikokuwa analipwa mshahara mkubwa lakini tulipomuambia tunataka kurudisha shirika letu alikubali kurudi kufanya kazi hapa na kuacha mshahara mkubwa huko

Mkuu wa mkoa Paul Makonda ameomba awe kama mimi, na mimi namuombea awe zaidi yangu

Niwapongeze sana Bendi ya TOT mmebadilika sana na leo mmepiga Mziki mzuri mpaka nikatamani kucheza na Mama Majaliwa hapa lakini nikaogopa sababu Majaliwa ana wivu sana

Pia nakupongeza Balozi kwa kuzungumza Kiswahili, sisi Watanzania tumekuwa watu wa 'How are you', 'How are you my son', sasa umewafundisha.

Balozi huyu ana miezi mitatu tuu hapa lakini ameonesha mfano na kuwafundisha wale ambao wanaona aibu

Rais Magufuli: Nimpongeze kijana huyu Mwenyekiti wa ATCL alikuwa anafanya kazi nchini Senegal alikokuwa analipwa mshahara mkubwa lakini tulipomuambia tunataka kurudisha shirika letu alikubali kurudi kufanya kazi hapa na kuacha mshahara mkubwa huko
 
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Messages
2,635
Likes
4,339
Points
280
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2018
2,635 4,339 280
Hahahaaa,nimeishia kucheka!Nikiangalia Dira TBC,aliunganishwa mtangazaji moja kwa moja kutoka airport Dsm!Akaeleza kuwa wageni wanaendelea kuingia kwa wingi na kwamba hakuna jua kutokana na mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya 5!

Mlioko Dar,naomba kujua hali ya hewa ikoje ili twende sawa na huy mtangazaji!
 
kisikiji

kisikiji

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2015
Messages
2,322
Likes
2,116
Points
280
kisikiji

kisikiji

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2015
2,322 2,116 280
Watakua wamepozi chato wapige picha.
Usihofu itafika, umeisubiri sana nini kiongozi? nikuelekeze mahali ukapate maji uwe na sauti ya kuiimbia ndege.
 
U

Undetectable

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Messages
233
Likes
212
Points
60
U

Undetectable

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2018
233 212 60
Inaingia mkoa wa Singida
 

Forum statistics

Threads 1,251,651
Members 481,811
Posts 29,778,891