Hongera Mahakama kufunguliwa MwanaHalisi

Hongera Mahakama kufunguliwa MwanaHalisi

Saturday, September 5, 2015Gaeti la Mwanahalisi Lafungulia Rasmi.......Kubenea Ashinda Kesi Mahakama kuuMAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk. Fennela Mkangara hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia gazeti la MwanaHALISI Julai 30 miaka mitatu iliyopita.Jaji Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumiakufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine kutaka maelezo ya utetezi kwa mchapishaji.Katika uamuzi wa shauri lililofunguliwa mara baada ya MwanaHALISI kufungiwa, Jaji Bongole amesema gazetihilo liko huru kuchapishwa kuanzia sasa.Jaji huyo amesema pamoja na uamuzi huo, kampuni iliyolalamika imepewa mafao yote iliyoyaomba katika kufungua shauri hilo la mapitio ya uamuzi wa Waziri ¨C prerogative orders.Miongoni mwa maombi ya faida ni HHPL kulipwa gharama za kesi pamoja na fidia kutokana na hasara iliyopatikana kwa muda wote wa gazti hilo kuwa kifungoni.Wakati Waziri alipofungia gazeti la MwanaHALISI, alieleza kwamba sababuni kuandika habari na makala za uchochezi.Habari hasa iliyoikera serikali hata kujilazimisha kuchukua hatua hiyo katili,ilikuwa ni iliyohusu uchunguzi wa tukio la kutekwa na kuteswa hadi karibu na kifo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (TMA), Dk. Steven Ulimboka.Dk. Ulimboka alikumbwa na mkasa huo mnamo Juni 2012 alipotekwa usiku eneo la Tazara, karibu na viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambako aliitwa na mtu aliyemtaja kuwa ni ofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye alikuwa na mawasiliano ya karibu naye kwa saa kadhaa siku chache na usiku huo siku ya tukio.Daktari huyo aliyekuwa mtumishi wa taasisi ya Marekani nchini, alifika eneo la Tazara akifuatana na daktari mwenzake aitwaye Deo, ambaye mara baada ya tukio hilo, wakati wa alfajiri, alimpigia simu Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa, kumjulishakuhusu kutekwa kwa Dk. Ulimboka.Kufuatia habari za kuachiwa huru kwa MwanaHALISI, Mhariri huyo amesema amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ya Tanzania, kwa kuwa umethibitisha kosa la serikali la kujichukulia maamuzi mkononi chini ya kuvunja sheria ilizoahidi kuzilinda.¡°NImefurahi sana kuthibitishiwa kwamba serikali ilikosea katika kufungia gazeti. Uamuzi wa jaji umesema waziri hakufuata hatua za kisheria alizopaswa kuchukua kabla ya kufungia gazeti, ikiwemo ya kuwapa wamiliki na mhariri nafasi ya kujitetea,¡± amsema Idrissa.¡°Lakini pia uamuzi huu unatakiwa uwe funzo muhimu kwa utawala kwamba hauwezi kudumu na kudumu kwa msisitizo wa kuhifadhi na kufurahia sheria zilizopitwa na wakati ambazo miaka kadhaa nyuma zilishatangazwa kuwa ni sheria kandamizi,¡± alisema.Mhariri amesema anawasiliana na mmiliki na mchapishaji wa MwanaHALISI, kampuni ya HHPL, kukamilisha taratibu za kuchapisha toleo la kwanza haraka iwezekanavyo. Gazeti hilo lilikuwa likichapishwa mara moja kwa wiki siku ya Jumatano.Mpekuzi blogTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )6§86§9HomeView web version
 
kubenea alifanye gazeti la Mwanahalisi liwe linatoka kila siku na Mawio liendelee kuwa la wiki mara moja.

Habari za kiuchunguzi kuziandika daily ni ngumu sana...aendeleze weekly but iwe siku tofauti na MAWIO!
 
nimeweka bajeti ya mwaka mzima kwa ajili ya kununua gazet langu la mwanahalisi kuanzia tu litakapoanza kutoka muda wowote ule kuanzia sasa.
big up mwanahalisi
 
Habari njema saana hii, natumaini sasa tutapata elimu ya kutosha hasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo octoba 25. Niwapongeze Hali Halisi Publishers LTD pamoja na Mwana Halisi gezeti langu nikipendalo Tanzania.
 
Slaa alilisifia juzi akiamini halitafunguliwa tena,tunaomba toleo lake la kwanza,lichunguze na kutupa taarifa za tuhuma za slaa kuhusu kuhongwa
 
Iyo kesi ilifunguliwa lini na lini hukumu imetolewa. Acheni udaku. Mwanahalisi limeshakufa kifo cha mende
 
Mwaka huu lazima uwehuke...!
Mkuu MUSSA ALLAN, njoo uchukue akili yako hapa Lumumba coz tangu umeenda BAVICHA, unashindwa kabisa kujenga hoja. Akili yako imetunzwa vema na hakuna anayeitumia coz imeingiwa na kinyesi
 
Hizi dalili mimi zinanipa uhakika wa lowasa kusikikwa kama raisi wa Tanzania baada oct 25 kweli siasa ni sayansi
 
Iyo kesi ilifunguliwa lini na lini hukumu imetolewa. Acheni udaku. Mwanahalisi limeshakufa kifo cha mende


Kweli wewe kipapa usiyekuwa na akili hata ujazo wa kisoda!!!

Hivi huwa unachangia nini kama huna hakika ya kitu? mbona unatia kinyaa sana?
 
Ukandamizaji sio utatuzi WA matatizo. Hongera Mwanahalisi hongera Kubenea
 
Na bado asubirie kichapo cha JJ MNYIKA. Magamba safari yatapukutika sana.
 
Huu udaku mpelekee mumeo Kubenea

Lizaboni acha gundu!!!! Ebu rejea ukweli mwingine hapa chini.

Dar es Salaam: Na Florence Majani.

Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetoa hukumu yake na kulipa ushindi gazeti la Mwanahalisi baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kuwa Waziri wa Habari na Utamaduni, Dk Fenella Mukangara hakufuata taratibu la kukifungia chombo hicho cha habari. Gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa Julai 30, 2012 kwa amri ya Dk Mukangara kwa kutumia mamlaka aliyopewa na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976. Akitangaza kulifungia gazeti hilo mwaka 2012, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Fabian Rugaimukamu alisema kuwa gazeti hilo limefungiwa kwa sababu limekuwa na mwenendo wa kuandika habari na makala za uchochezi na zinazojenga hofu kwa wananchi. Lakini leo, Jaji Salavatory Bongole wa Mahakama Kuu ametoa uamuzi huo na kusema kuwa waziri hakufuata hatua za kisheria ambazo alitakiwa kuzifuata kabla ya kulifungia. Wakili wa Kampuni ya Hali Halisi Publisher , Rugemaleza Mashamala amesema ingawa hawajapewa hukumu mkononi lakini kutokana na ushindi waliopewa na mahakama ni halali na wana haki ya kuendelea na uchapishaji. Hata hivyo alisema ni lazima upande wa serikali waone uamuzi wa kimaandishi uliotolewa ili kujiridhisha na kuendelea na taratibu nyingine.

CHANZO: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom