Hongera Mahakama kufunguliwa MwanaHalisi

Sheria inasemaje,huyo waziri alielifungia gazeti hawezi kushitakiwa na akalipa fidia?kampuni imeingia hasara kiasi gani kwakutofanya sales kumbuka kuna capital waliinvest kwa kazi hiyo...
 
Halafu waziri aliyelifungia eti ni Dokta. Kumbe hajui taratibu za kazi yake na sasa eti anagombea ubunge. Ifike mahali mawaziri kama hawa wawe ndio wanaolipa fidia kutokana na uzembe wao. Serikali iwe inalipa halafu inawafilisi mawaziri wazembe kama huyu ndio watajifunza kufanya kazi kwa kufuata taratibu.
 
Hongera sana kubenea 👏👏
 
Weraweraaaaaaa! Nitaanza kusoma magazeti tena!
 
Lile gazeti maarufu la habari za kiuchunguzi lililokuwa mwiba kwa serikali limeshinda kesi mahakamani na kuruhusiwa kuanza kuchapishwa tena.
Gazeti lile lililkuwa tishio kwa serikali kwa kufukua habari nyeti zilizojificha bila ya woga, jee hapa tunapoelekea uchaguzi mkuu litaweza kuweka mambo mbalimbali hadharani na kubadili upepo wa uchaguzi?
 
Mahakama imelifungulia gazeti la Mwanahalisi.

Chanzo:Tanzania Daima
 
Kubenea awe makini sana na hili gazeti.
Siku akiandika habari za kichochezi anapelekwa gerezani mazima na masaburi anapita bila kupingwa.
Aachane nalo hadi uchaguzi upite.
 
Kwa hilo hakumsaidii kupata MO Ibrahim prize anayoiwida; utawala wake wa miaka 10 umekuwa wa kifisadi.
 
Saturday, September 5, 2015
Gaeti la Mwanahalisi Lafungulia Rasmi.......Kubenea Ashinda Kesi Mahakama kuu

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk. Fennela Mkangara hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia gazeti la MwanaHALISI Julai 30 miaka mitatu iliyopita.

Jaji Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumia kufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine kutaka maelezo ya utetezi kwa mchapishaji.

Katika uamuzi wa shauri lililofunguliwa mara baada ya MwanaHALISI kufungiwa, Jaji Bongole amesema gazeti hilo liko huru kuchapishwa kuanzia sasa.

Jaji huyo amesema pamoja na uamuzi huo, kampuni iliyolalamika imepewa mafao yote iliyoyaomba katika kufungua shauri hilo la mapitio ya uamuzi wa Waziri – prerogative orders.

Miongoni mwa maombi ya faida ni HHPL kulipwa gharama za kesi pamoja na fidia kutokana na hasara iliyopatikana kwa muda wote wa gazti hilo kuwa kifungoni.

Wakati Waziri alipofungia gazeti la MwanaHALISI, alieleza kwamba sababu ni kuandika habari na makala za uchochezi.

Habari hasa iliyoikera serikali hata kujilazimisha kuchukua hatua hiyo katili, ilikuwa ni iliyohusu uchunguzi wa tukio la kutekwa na kuteswa hadi karibu na kifo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (TMA), Dk. Steven Ulimboka.

Dk. Ulimboka alikumbwa na mkasa huo mnamo Juni 2012 alipotekwa usiku eneo la Tazara, karibu na viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambako aliitwa na mtu aliyemtaja kuwa ni ofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye alikuwa na mawasiliano ya karibu naye kwa saa kadhaa siku chache na usiku huo siku ya tukio.

Daktari huyo aliyekuwa mtumishi wa taasisi ya Marekani nchini, alifika eneo la Tazara akifuatana na daktari mwenzake aitwaye Deo, ambaye mara baada ya tukio hilo, wakati wa alfajiri, alimpigia simu Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa, kumjulisha kuhusu kutekwa kwa Dk. Ulimboka.

Kufuatia habari za kuachiwa huru kwa MwanaHALISI, Mhariri huyo amesema amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ya Tanzania, kwa kuwa umethibitisha kosa la serikali la kujichukulia maamuzi mkononi chini ya kuvunja sheria ilizoahidi kuzilinda.

“NImefurahi sana kuthibitishiwa kwamba serikali ilikosea katika kufungia gazeti. Uamuzi wa jaji umesema waziri hakufuata hatua za kisheria alizopaswa kuchukua kabla ya kufungia gazeti, ikiwemo ya kuwapa wamiliki na mhariri nafasi ya kujitetea,” amsema Idrissa.

“Lakini pia uamuzi huu unatakiwa uwe funzo muhimu kwa utawala kwamba hauwezi kudumu na kudumu kwa msisitizo wa kuhifadhi na kufurahia sheria zilizopitwa na wakati ambazo miaka kadhaa nyuma zilishatangazwa kuwa ni sheria kandamizi,” alisema.

Mhariri amesema anawasiliana na mmiliki na mchapishaji wa MwanaHALISI, kampuni ya HHPL, kukamilisha taratibu za kuchapisha toleo la kwanza haraka iwezekanavyo. Gazeti hilo lilikuwa likichapishwa mara moja kwa wiki siku ya Jumatano.

Mpekuzi blog

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

‹
›
Home
View web version
 
Kodi za wananchi k utumika kulipa fidia kwa maamuzi ya kijinga
 
kubenea alifanye gazeti la Mwanahalisi liwe linatoka kila siku na Mawio liendelee kuwa la wiki mara moja.
 
"Mnyika huko Kibamba" nadhani utakuwa umenielewa, siwezi kuandika kwa kuwa natii sheria ya mitandao bila shuruti
 
Ifike wakati mtu akifanya maamuzi yakijinga alipe fidia kwa pesa zake na si kodi za watanzania
 
Hapa ndipo nazidi kupata kigugumizi cha ''kwanini serikali ya CCM bado inataka kuendelea kubaki madarakani?
 
Back
Top Bottom