Hongera Mahakama kufunguliwa MwanaHalisi

Hongera Mahakama kufunguliwa MwanaHalisi

Wangefungia hata miaka 100,mwanahalisi online bado ilikuwa inatupa uhondo.wanadhani huu ni mwaka 47 mpaka mtu uende kununua gazeti.mambo online
 
nalikubali kwa kuandika habari za kweli km hizi
 

Attachments

  • 1441389573287.jpg
    1441389573287.jpg
    41.6 KB · Views: 465
Kwa uonevu huu na double standards za serikali ya CCM sijui kwanini wanataka tuendelee kuwachagua....
 
[h=2]Friday, September 4, 2015[/h][h=3][/h]

kubenea.jpg

Mkurugenzi wa Mwanahalisi Publisher, Saed Kubenea akionesha magazeti ya Mwanahalisi katika moja ya mikutano aliyofanya na wanahabari. Picha ya Maktaba ​



Na Florence Majani​


Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetoa hukumu yake na kulipa ushindi gazeti la Mwanahalisi baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kuwa Waziri wa Habari na Utamaduni, Dk Fenella Mukangara hakufuata taratibu la kukifungia chombo hicho cha habari.



Gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa Julai 30, 2012 kwa amri ya Dk Mukangara kwa kutumia mamlaka aliyopewa na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.


Akitangaza kulifungia gazeti hilo mwaka 2012, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Fabian Rugaimukamu alisema kuwa gazeti hilo limefungiwa kwa sababu limekuwa na mwenendo wa kuandika habari na makala za uchochezi na zinazojenga hofu kwa wananchi.



Lakini leo, Jaji Salavatory Bongole wa Mahakama Kuu ametoa uamuzi huo na kusema kuwa waziri hakufuata hatua za kisheria ambazo alitakiwa kuzifuata kabla ya kulifungia.



Wakili wa Kampuni ya Hali Halisi Publisher , Rugemaleza Mashamala amesema ingawa hawajapewa hukumu mkononi lakini kutokana na ushindi waliopewa na mahakama ni halali na wana haki ya kuendelea na uchapishaji.


Hata hivyo alisema ni lazima upande wa serikali waone uamuzi wa kimaandishi uliotolewa ili kujiridhisha na kuendelea na taratibu nyingine.



CHANZO:
MWANANCHI​





 
Watanzania acheni kuwa na ubongo wa kuku,hamjiulizi kwa nini hukumu ya kulifungulia gazeti hili imekuja wakati wa uchaguzi mkuu unaotikisa taifa? Tafakari.
 
Back
Top Bottom