Hongera Mahakama kufunguliwa MwanaHalisi

Hongera Mahakama kufunguliwa MwanaHalisi

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,465
Mahakama imeamua. Hizi ni habari njema kwa Tasnia ya Habari nchini.


[h=2]Friday, September 4, 2015[/h][h=3][/h]

kubenea.jpg

Mkurugenzi wa Mwanahalisi Publisher, Saed Kubenea akionesha magazeti ya Mwanahalisi katika moja ya mikutano aliyofanya na wanahabari. Picha ya Maktaba



Na Florence Majani


Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetoa hukumu yake na kulipa ushindi gazeti la Mwanahalisi baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kuwa Waziri wa Habari na Utamaduni, Dk Fenella Mukangara hakufuata taratibu la kukifungia chombo hicho cha habari.



Gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa Julai 30, 2012 kwa amri ya Dk Mukangara kwa kutumia mamlaka aliyopewa na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.


Akitangaza kulifungia gazeti hilo mwaka 2012, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Fabian Rugaimukamu alisema kuwa gazeti hilo limefungiwa kwa sababu limekuwa na mwenendo wa kuandika habari na makala za uchochezi na zinazojenga hofu kwa wananchi.



Lakini leo, Jaji Salavatory Bongole wa Mahakama Kuu ametoa uamuzi huo na kusema kuwa waziri hakufuata hatua za kisheria ambazo alitakiwa kuzifuata kabla ya kulifungia.



Wakili wa Kampuni ya Hali Halisi Publisher , Rugemaleza Mashamala amesema ingawa hawajapewa hukumu mkononi lakini kutokana na ushindi waliopewa na mahakama ni halali na wana haki ya kuendelea na uchapishaji.


Hata hivyo alisema ni lazima upande wa serikali waone uamuzi wa kimaandishi uliotolewa ili kujiridhisha na kuendelea na taratibu nyingine.



CHANZO:
MWANANCHI

 
Source please.

Kwa sababu hili gazeti walilifungia Wizara ya Habari.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Halafu kubenea yupo kwenye kampeni. Nahamu lirudie ile stori ya kumwagiwa tindikali. Lilikuwa janga baya zaidi kuliko kufungiwa!
 
Wameamua kulifungulia maana sasa hivi halitaweza kuandika zile habar maana shut up law ipo.
 
kwanza naomba niombe radhi kwa serikali na cyber crime law kwa hili ninalo lipost kwa sababu natambua uwepo wa ile sheria but hii sio taarifa ni swali nawauliza wadau ili nipate uhakika wa kile nilicho kiskia.

Nimeskia kua gazeti la mwanahalisi limefunguliwa rasmi leo baada ya hukumu ya mahakama.kuna ukweli wowote wadau?
 
Kuna habari zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Gazeti la Mwanahalisi limefunguliwa baada ya hukumu ya Mahakama leo mchana.

Mwenye taarifa zaidi atujuze.

Wasalaam.
 
We subiria tu watakuja humu muda si mrefu, ila nini wasiwasi kama kipindi hiki wanaweza kuruhusu hilo Gazeti likaanza kuingia sokoni, si unajua kuwa huwa linaangaza kila kona!!? Watasubiri hadi uchaguzi upite aisee.
 
We subiria tu watakuja humu muda si mrefu, ila nini wasiwasi kama kipindi hiki wanaweza kuruhusu hilo Gazeti likaanza kuingia sokoni, si unajua kuwa huwa linaangaza kila kona!!? Watasubiri hadi uchaguzi upite aisee.

Kama ni kweli wamekosea timing maana jamaa watakuja na mambo mazito na hata mfumo unaelewa kazi yao hawa
 
Itakuwa poa sanaaa, hivi kumbe jamaa alifungua kesi mahakamani?
 
Natamani limalizie kisa cha Dr. Ulimboka na Ramadhan Ighondu, maana hii ndio ilikuwa makala ya mwisho na ndio simulizi ambayo huenda ilipelekea serikali kulifungia hili gazeti.

Kama sikosei Kubenea alituhaidi angeivua nguo TISS kuhusu namna ambavyo walishiriki kumpa kibano Ulimboka
 
Back
Top Bottom