Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Yes ataondoka na kila mtu ataondoka, hakuna atakayeishi milele. Hoja yangu hapa ni watu watuhumiwe kwa tuhuma za haki, na ikibidi waondolewe, then, waondolewe kwa haki kwa tuhuma za ukweli na sio waondolewe kwa kupikiwa majungu.
P
Mwendazake zake wakati anaondoa watu bila hata sababu za msingi, mlikuwa mnademka mitandaoni kumsifia na kumuabudu,,
We ndio ulikuwa mmoja wanaodemka kufurahia watu wakitumbuliwa enzi za mwendazake, wakati Nape anapigwa chini ulikuwa mmoja wa watu waliofurahia Sana
 
Kwa hiyo tukiambiwa Watu8 ni fisadi jambo la kwanza ni kuamini uambiwaji / maelezo huo/hayo bila hata ushahidi.

Kama msimamo ndiyo huo kama taifa, basi tufute dhana ya ushahidi.

Mkuu anza kwanza kusoma mstari wa kwanza kwamba katika nchi zetu hizi za kiafrika kuna mstari mwembamba mno kati ya mtu fisadi na mtu safi...

Kwa mantiki hiyo, ndipo mimi binafsi maamuzi yangu huegemea kuamini mtuhumiwa wa ufisadi kwa asilimia kubwa kama zote huwa ni kweli...

Hii mifumo ya kisheria haiathiri maamuzi yangu kwa kuwa sheria zipo, mahakama zipo na bado tunaendelea kufisadiwa huku tukiendelea kukusanya ushahidi...

Hizi nchi zetu kuna tabaka la watu lipo juu ya sheria, na jambo hili hatuwezi kulibadilisha katu, labda tubadilike na tusiwe Waafrika...
 
Wanabodi,
Nimekutana na bandiko hili
lenye tuhuma lukuki dhidhi ya kiongozi huyu..

Ukisikia majungu ndio haya. Ukituhumu humu, leta na uthibitisho.
Hapa umevurumisha tuhumu lukuki dhidi ya Biteko-
Tuhuma zenyewe ni hizi
  1. Dotto Biteko ameiba kiasi kikubwa cha pesa, kiasi gani?-Ni tuhuma tuu, hakuna uthibitisho!.
  2. Dotto Biteko ni mshirika usafirishaji madini ya Tanzanite kwa njia za panya kwa kushirikiana na wafanyabiashara. How?. Ni tuhuma tuu hazina uthibitisho wowote?.
  3. Dotto Biteko anaiba madini mengi, ameibaje, ameiba wapi, madini yapi, - Ni tuhuma tuu, hakuna uthibitisho wowote.
  4. Dotto Biteko ana percentage kwenye migodi kibao, percentage ngapi, migodi gani?-Ni tuhuma tuu hazina uthibitisho wowote!.
  5. Dotto Biteko ni jangili wa mwendazake!. Ujangili gani?, unamtukana marehemu na kumsingizia ujangili?!, hii ni dhambi!.
  6. Doto Biteko kila siku anashinda kwa waganga, waganga gani?, hili la mtu kushinda kwa waganga pia linaingilia the right to privacy ya mtu, kama watu wanaoshinda hospitali, makanisani, nyumba za ibada a makanisa ya walokole, haya ni mambo ya imani, Tanzania tuko huru kuamini lolote, waumini wa Mungu washinde makanisani, waumini wa tiba za kizungu washinde mahospitalini, waumini wa dini za asili, tushinde kwa mizimu na waganga wa kienyeji, tusiingilie privacy za watu!.
Mode: JF tuweke standards za kulinda heshima na majina ya watu, dhidi ya mtu kuchafuliwa jina kwa chuki binafsi. Iongezwe kanuni, mtu ukileta tuhuma za mtu yoyote au kiongozi yoyote kwa jf as a whistleblower, lazima tuhuma hizo ziandamane na uthibitisho, ndipo jina la mtuhumiwa litajwe, kumtuhumu mtu kwa kumtaja kwa jina, bila ya uthibitisho wowote, ni kuchafua tuu bure majina ya watu.

Najua JF as a whistleblower, imefanya kazi nzuri na inaendelea kufanya kazi nzuri, lakini na sisi sasa ni lazima tubadilike, kwenye tuhuma, lazima tufanye a due diligence kwa kuhakikisha tunafuata sheria, taratibu na kanunu, "the one who alleges, must prove", ukileta tuhuma zozote za hearsay bila uthibitisho, yes zilete, as a whistleblower, but don't mention names without proof. Yaani leta tuhuma, lakini usitaje majina bali taja tuu cheo na indications zote ambazo zita point kwa mhusika bila kumtaja jina na kumchafua bila uthibitisho wowote!.

Nimetokea kumfahamu mtuhumiwa huyu kupitia kazi yangu ya uandishi, kwa mambo anayoyafanya hadharani, huyu ni mmoja wa wazalendo wa kweli wa taifa hili.
Msikilize Dotto Biteko kwenye video hii.

Ukimzikiliza Biteko, utakubaliana na mimi, huyu ni mzalendo wa kweli wa nchi hii, kumtuhumu kwa tuhuma lukiki bila ushahidi wowote au uthibitisho wowote, sio kumtendea haki.

Hongera sana wana jf kwa kwa kazi kubwa nzuri ya Whistleblowing, ila sasa tubadilike, tukitoa tuhuma, tulete na uthibitisho kuepuka kuchafua bure majina ya watu.

Paskali.
Ndiyo umepewa kazi ya kumsafisha?

Wangapi humu wametuhumiwa kwa namna hii hii aliyotuhumiwa Doto Biteko, mbona hukuwahi kuweka bandiko?

Ukisikia unafiki, ndiyo huu uliouweka hapa.

January anawekewa tuhuma humu kila siku. Mara sijui anataka mafisadi wauze majenereta, kuna uthibitisho?

Tundu Lisu, mara amehongwa na Acacia, kuna uthibitisho?

Rais Samia, mara amehongwa na mabeberu, kuna uthibitisho?

Zito mara amehongwa, kuna uthibitisho?

Dr. Slaa alihongwa na Serikali, kuna uthibitisho?

Lipumba anatumiwa na Serikali, kuna uthibitisho.

Mbowe ni wakala wa mabeberu, kuna uthibitisho?

Mabeberu wanatuibia, kuna uthibitisho?

Tupo kwenye vita vya kiuchumi, kuna uthibitisho?

Hak wote hatujawahi kumsikia mnafika Pascal Mayala akikemea ila tu tuhuma dhidi ya Biteko, tena kwa kiasi kikubwa ni tuhuma ambazo zina maelezo yanayojitosheleza namna uovu anavyoutenda.

Wewe ukiamua kumsafisha, kumpamba au kumtetea, endelea, lakini usiwapangie wanaomtuhumu. Ukweli ni kuwa hakuna kitakachofanywa dhidi ya Doto kwa vile tu watu wametuhumu. Kama kutakuwa na hatua, ujue ni baada ya wanaomchukulia kujiridhisha na tuhuma hizo.¹
 
Naounga mkono hoja. Moyo wa mtu ni kichaka, hata siku moja usimsemehe mtu. Hivi Kuna kiongozi tz akikaa sehemu nyeti yenye mavumba asifanye ubadhilifu?? Tatizo bongo hakuna system inayowashughulikia wabadhirifu ipasavyo, watu wanaanza kwa kuteuliwa na wanaishia kutenguliwa

Yahani adhabu kubwa wanayopata ni kutumbuliwa
Very affordable adhabu. Mtu wakati huo keshajinufaisha na mabilioni yaliyotakiwa yakafanye maendeleo yanayogusa maisha ya watu.
 
Nadhani zile story kuwa kuna chuki imepandikizwa- hii ndiyo maana yake.
Kwani kama si chuki ni nini basi?

Sad kwamba hakuna anayejaribu kuangalia kama kuna ukweli katika hili isipokuwa kuna ubishi juu ya hizi chuki zinazosemekana kuwa zimepandwa.

Pengine imeachwa ijisolve naturally.
Hivyo tusubiri.
 
QUOTE="Pascal Mayalla, post: 40859523, member: 17813"]
Wapenda haki wakiona mtu yoyote hatendewi haki, hujitokeza kumtetea, kwasababu kiukweli kabisa kuna baadhi ya tuhuma, sio tuhuma za kweli, ni chuki binafsi tuu.

Ndio maana nimeshauri, ukituhumu, leta na uthibitisho. Ukipata tuhuma za hearsay tuu zisizo na uthibitisho, then zilete as Whistleblow lakini usiweke majina ili kuepuka kuwachafua watu bure.
P
BITEKO siyo mtu safi hata kidogo.

Nenda kafanye utafiti kwa kuongea na wafanyabiashara wakubwa wa migodi wakueleze namna Dotto anavyokusanya bongo bila aibu kutoka kwao.

Vilevile, upendeleo wa wazi na tuhuma zilizo bayana kuwa ana maslahi na kampuni ya usafirishaji mafuta ya mitambo katika mgodi wa GGM ni uchafu kwake na inamuondolea kabisa heshima yake kwa jamii.[/QUOTE]Mimi binafsi, siyo kwa kusikia kwa watu wa pembeni, bali wahusika wenyewe waliolazimika kutoa pesa kwa Biteko ili wapate eneo la kuchimba ambalo lilikiwa ni eneo la kampuni moja. Walimpa akichotaka na leo wanachimba. Mwenye eneo anaendelea kupambana kuona kama atarudishiwa, sijui kama atarudishiwa. Ninao mfano mwingine vivyo hivyo, wahusika wenyewe wanaeleza walivyolazimika kutoa pesa ili wapate maeneo ambayo hayakuwa yao.

Uthibitisho hauwezi kupatikana hapa, huwezi kuweka majina ya watu waliotoa pesa hapa, ila vyombo vinavyohusika vifanye kazi, vimchunguze Waziri Biteko. Kwa hakika, bila chuki wala nia ya kisasi chochote, Biteko siyo msafi. Kwenye vyombo vya uchunguzi, watu waliolazimika kutoa pesa, wataweka wazi. Uchunguzi ufanyike.
 
Wapenda haki wakiona mtu yoyote hatendewi haki, hujitokeza kumtetea, kwasababu kiukweli kabisa kuna baadhi ya tuhuma, sio tuhuma za kweli, ni chuki binafsi tuu.

Ndio maana nimeshauri, ukituhumu, leta na uthibitisho. Ukipata tuhuma za hearsay tuu zisizo na uthibitisho, then zilete as Whistleblow lakini usiweke majina ili kuepuka kuwachafua watu bure.
P
Umeongea la maana sana sijui kwa sababu home boy ndio anasakamwa?

Kuna video clip ya sekunde chache tu inasambazwa, watu wenye akili timamu kila ukiitazama video hiyo ni vigumu kumtambuwa muhusika, lakini kuna kundi la watu wanatulazimisha tuamini huyo ni Kabwili ya Yanga anatuhumiwa ushoga, hivi kwa ushahidi kama huo ni haki kweli kumpa mtu tuhuma nzito? Au ndio bullying?
 
Mkuu Watu8 , kwanza nakubaliana na wewe, the dividing line between mtu safi na fisadi is very thin, kwasababu ufisadi hufanywa sirini, hivyo with naked ayes, kuna watu wanaonekana clean, kumbe ni mafisadi kichinichini au sirini, lakini kwa kutumia jicho la tatu, jicho la rohoni, unamuona fisadi ni fisadi hata kama amevaa mavazi meupe kama malaika au vazi la askofu, na mtu safi alivalia kaniki.
P
Kumtetea Doto na kumtangaza kuwa ni mzalendo, hukustahili kufanya. Aheri ungenyamaza tu, kwa vile hujui kama ni msafi au corrupt. Lakini nakuhakikishia ukifanyika uchunguzi, utajilaani kumtetea mtu wa namna hiyo. Hujui hata anavyotoa pesa kwa watu mbalimbali ili wamsafishe kutokana tuhuma nyingi nzito, na nyingine hazijawahi kuandikwa hata humu? Sasa hivi anahangaika sana, kwa kuwatumia watu mbalimbali kutoka kwenye ofisi kubwa za uongozi, ili wamsafishe dhidi ya uchafu ambao amekuwa akiufanya.
 
Paskali una angalizo zuri, lakini watu wanaona bora waweke hizo hearsay humu mitandaoni, maana taasisi za uchunguzi na kutoa haki nazo zinafanya kazi nje ya weledi kabisa. Mifano mirahisi kabisa, kuna nyumba ilikamatwa ikiwa imejiunganishia bomba la mafuta hapa Dar, waziri mkuu na IGP wakasema ndani ya siku 7 watatoa ripoti ya jambo lile, lakini mpaka leo kimya.

Hata watu wakiamua kwenda mahakamani, bado mahakamani kwa sasa sio sehemu ya uhakika ya kwenda kupata haki, mfano hii kesi ya Mbowe kama kuna documents zimewafikia mashahidi kinyume na utaratibu na bado jaji anakoroga unategemea nini? Kuna mashahidi unaona kabisa wanatoa ushahidi wenye kutia shaka lakini wanaachwa.

Kwa mifano hiyo ya wazi wa taasisi za kufanyia kazi tuhuma ziko chini ya weledi, unategemea watu waache kuja kuanika huku mitandaoni. Fuatilia vizuri hicho unachosema ni kuchafuana, utakuta zaidi ya nusu ni kweli kwani ni watu wanaojuana na machafu yao. Watu waliopo madarakani kwa uchaguzi wa kishenzi vile watakuwaje wasafi?
"Mifano mirahisi kabisa, kuna nyumba ilikamatwa ikiwa imejiunganishia bomba la mafuta hapa Dar, waziri mkuu na IGP wakasema ndani ya siku 7 watatoa ripoti ya jambo lile, lakini mpaka leo kimya"

Hivi hii habari iliishia wapi? Iliishaje?
 
BITEKO siyo mtu safi hata kidogo.

Nenda kafanye utafiti kwa kuongea na wafanyabiashara wakubwa wa migodi wakueleze namna Dotto anavyokusanya bongo bila aibu kutoka kwao.

Vilevile, upendeleo wa wazi na tuhuma zilizo bayana kuwa ana maslahi na kampuni ya usafirishaji mafuta ya mitambo katika mgodi wa GGM ni uchafu kwake na inamuondolea kabisa heshima yake kwa jamii.
Wewe tuambie ni mfanyabiashara yupi na yupi kaombwa pesa ili tumface direct.otherwise haya uliyoandika bado ni majungu.[/QUOTE]Upo sahihi sana. Jana tu niipata nafasi ya kuongea na mwanafamiia wa huyu aliyepewa tenda ya kupeleka mafuta GGM kwa msaada wa Biteko. Mimi mwenyewe nilikuwa siamini. Nilishangaa huyu mwanafamiia alipotamka kuwa ni kweli.

Kukifanyika uchunguzi na taarifa ikawekwa wazi, wengi watashangaa jinsi huyu bwana alivyofanya tangu kifo cha Magufuli. Anatafuta pesa kwa namna isivyo halali kwa kiwango cha ajabu na kushangaza.
 
Yes ataondoka na kila mtu ataondoka, hakuna atakayeishi milele. Hoja yangu hapa ni watu watuhumiwe kwa tuhuma za haki, na ikibidi waondolewe, then, waondolewe kwa haki kwa tuhuma za ukweli na sio waondolewe kwa kupikiwa majungu.
P
Ebu eleza, ni tuhuma ipi dhidi ya Biteko ni majungu? Kukosekana kwa kielelezo cha kuthibitisha hapa JF, haimaanishi taarifa hiyo ni majungu, sawa na ilivyo kama mtu akaleta tuhuma hapa, si lazima tuhuma hiyo iwe ni jambo la kweli. Ndiyo maana inaitwa tuhuma.
 
"Mifano mirahisi kabisa, kuna nyumba ilikamatwa ikiwa imejiunganishia bomba la mafuta hapa Dar, waziri mkuu na IGP wakasema ndani ya siku 7 watatoa ripoti ya jambo lile, lakini mpaka leo kimya"

Hivi hii habari iliishia wapi? Iliishaje?
Limepotezewa tayari wakiamini tumesahau.
 
Wanabodi,
Nimekutana na bandiko hili
lenye tuhuma lukuki dhidhi ya kiongozi huyu..

Ukisikia majungu ndio haya. Ukituhumu humu, leta na uthibitisho.
Hapa umevurumisha tuhumu lukuki dhidi ya Biteko-
Tuhuma zenyewe ni hizi
  1. Dotto Biteko ameiba kiasi kikubwa cha pesa, kiasi gani?-Ni tuhuma tuu, hakuna uthibitisho!.
  2. Dotto Biteko ni mshirika usafirishaji madini ya Tanzanite kwa njia za panya kwa kushirikiana na wafanyabiashara. How?. Ni tuhuma tuu hazina uthibitisho wowote?.
  3. Dotto Biteko anaiba madini mengi, ameibaje, ameiba wapi, madini yapi, - Ni tuhuma tuu, hakuna uthibitisho wowote.
  4. Dotto Biteko ana percentage kwenye migodi kibao, percentage ngapi, migodi gani?-Ni tuhuma tuu hazina uthibitisho wowote!.
  5. Dotto Biteko ni jangili wa mwendazake!. Ujangili gani?, unamtukana marehemu na kumsingizia ujangili?!, hii ni dhambi!.
  6. Doto Biteko kila siku anashinda kwa waganga, waganga gani?, hili la mtu kushinda kwa waganga pia linaingilia the right to privacy ya mtu, kama watu wanaoshinda hospitali, makanisani, nyumba za ibada a makanisa ya walokole, haya ni mambo ya imani, Tanzania tuko huru kuamini lolote, waumini wa Mungu washinde makanisani, waumini wa tiba za kizungu washinde mahospitalini, waumini wa dini za asili, tushinde kwa mizimu na waganga wa kienyeji, tusiingilie privacy za watu!.
Mode: JF tuweke standards za kulinda heshima na majina ya watu, dhidi ya mtu kuchafuliwa jina kwa chuki binafsi. Iongezwe kanuni, mtu ukileta tuhuma za mtu yoyote au kiongozi yoyote kwa jf as a whistleblower, lazima tuhuma hizo ziandamane na uthibitisho, ndipo jina la mtuhumiwa litajwe, kumtuhumu mtu kwa kumtaja kwa jina, bila ya uthibitisho wowote, ni kuchafua tuu bure majina ya watu.

Najua JF as a whistleblower, imefanya kazi nzuri na inaendelea kufanya kazi nzuri, lakini na sisi sasa ni lazima tubadilike, kwenye tuhuma, lazima tufanye a due diligence kwa kuhakikisha tunafuata sheria, taratibu na kanunu, "the one who alleges, must prove", ukileta tuhuma zozote za hearsay bila uthibitisho, yes zilete, as a whistleblower, but don't mention names without proof. Yaani leta tuhuma, lakini usitaje majina bali taja tuu cheo na indications zote ambazo zita point kwa mhusika bila kumtaja jina na kumchafua bila uthibitisho wowote!.

Nimetokea kumfahamu mtuhumiwa huyu kupitia kazi yangu ya uandishi, kwa mambo anayoyafanya hadharani, huyu ni mmoja wa wazalendo wa kweli wa taifa hili.
Msikilize Dotto Biteko kwenye video hii.

Ukimzikiliza Biteko, utakubaliana na mimi, huyu ni mzalendo wa kweli wa nchi hii, kumtuhumu kwa tuhuma lukiki bila ushahidi wowote au uthibitisho wowote, sio kumtendea haki.

Hongera sana wana jf kwa kwa kazi kubwa nzuri ya Whistleblowing, ila sasa tubadilike, tukitoa tuhuma, tulete na uthibitisho kuepuka kuchafua bure majina ya watu.

Paskali.

Ila Mkuu,kwamba vyanzo vyangu vimeniambia kwamba kijana wangu anakwapua mazao na kuuza shambani nikae kimia mpaka kudhibitisha, na KAZI ya vyombo wa uchunguzi kuoji KAZI yao ni ipi?

Binafsi nitatoa malalamiko ,na vyombo husika vinisaidie kudhibitisha Kama kweli au la,
 
Huyu ni mtusi pandikizi, na wamejana huko Geita,Mwanza, Kagera, Ukerewe, na sehemu za mkoa wa Mara.
 
Hawa wanaleta kelele tu zisizo na mashiko. Hivi kable ya Dotto na Magu kuingia madarakani Tanzania ilisifika kwa uuzaji wa Tanzanite? Au tulibaki kusikia India, South Africa na Kenya ndio wauzaji wakubwa.

Magufuli na serikali waliwabana sana watorosha madini ndio maana wapo hapa kulalamika. Tanzanite one mlichukulia kinyemela na kujilia kiulaini, vipi hamtaki mbanwe ili kutoa fursa ya serikali kukusanya mapato halisi?
Ukiniambia kuwa Magufuli alijitahidi kuwabana wanaotorosha madini, nakubaliana na wewe kwa 100%. Inaonekana Biteko alilisimamia hilo, siyo kwa sababu ndicho alichokiamini, bali ni kwa sababu ndicho kilichomhakikishia kuendelea kuwa Waziri. Kama ingekuwa hicho ndicho alichokuwa akikiamini, asingebadilika kwa kiwango hiki cha sasa, mara tu baada ya marehemu Magufuli kuondoka Duniani.

Hii inaonesha mawaziri na watendaji wengi wa marehemu, waliyokuwa wanayafanya ni kwa sababu ya kumwogopa marehemu, lakini kiasili kwenye mioyo yao, wengi ni corrupt kupindukia, Biteko ni miongoni. Nazungumza nikiwa na uthibitisho wangu moyoni. Ukihitajika panapostahili na palipo salama, tutapeleka.
 
Back
Top Bottom