Hongera HALIMA MDEE umeonyesha ukomavu

Hongera HALIMA MDEE umeonyesha ukomavu

Status
Not open for further replies.
usilolijua!!!

wakati mwingine huwa tuna waacha mazuzu na mandondocha ya ccm yasapotiane ujaha wao',lakini sie tunaojua mapungufu yao wala hatuhangaiki,yaache tu hayo mazuzu dada rose wala usihangaike nayo hayajitambui yapo utumwani ccm.
 
Pasco ni gamba, yupo kwenye siasa kwa maslahi, usijiumize kichwa kutaka kumwelewa
Call me what you may, it's not gonna change my status !.
Mtu wa kwanza kumuita JK ni dhaifu ni mimi kupitia uzi huu na wengi mlinipongeza mkiniita bold!.
Mtu wa kwanza kusema CCM imechokwa ni mimi kupitia uzi huu, na wengi mlinipongeza!.
Niliposema Chadema Haijajipanga, hili ndilo likawa kosa, nikaanza kuitwa gamba!.

Kiukweli kutoka ndani ya nafsi yangu sina chama ila kuna ninawakubali sana kwa Chadema ni ZZK, kwa CCM ni EL, na kwa CUF ni Jussa!.
Pasco.
 
Mwalimu J.K.NYERERE """""alieleza kuwa dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu........amin msiamini huu ndo mwanzo wa kutafunana ndani ya CDM na hawatokaa salama milele......., wabunge wote wa CHADEMA kwa namna moja au nyingine tumewajua wapo upande upi! Kimsingi nampongeza Mbunge wa Kawe HALIMA MDEE kwa kukaa kimya, kutotoa neno lolote ambalo kwa namna moja au nyingine lingeendelea kukuza mgogoro! CHADEMA igeni kwa mwana Mama HALIMA MDEE kawashinda busara wanaume wote ndani ya CHADEMA upeo wa kufikiri! Nakushauri usije comment chochote juu ya hili sakata utajijengea heshima kubwa kwa nchi hiii

Unazifahamu 14 Principles of Management? Rudi darasani! Moja ya principle ni Principal of One Boss/Unity of command! Wote hawawezi kuwa wasemaji!
 
Sina shaka kabisa na msimamo wala maamuzi ya cdm juu ya Zitto na ninaunga mkono hilo kwa 100% kumuondoa ndani ya CDM. Shaka niliyonayo ni moja tu, kwamba taratibu na katiba ya kumchukulia hatua zzk huenda zilikuwapo na ndio zinazotugharimu CDM leo na katika kesi hii, lakini pia nna imani hatimae tutashinda. Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu....

Toka awali nimekuwa na imani kubwa sana kwa mwenyekiti na katibu wake, na tukio hili linaidhihirisha imani yangu kwao zaidi kwani yale niloyajengea imani sqasa yanathibitika, vivyo hivyo toka awali nilikua na shak sana juu ya mwenendo thabiti wa zzk na leo hili pia linathibitsha kwangu kuwa zzk si mkweli na hapaswi kuungwa mkono asilani.

Mh. Mbowe, ni mtu ambaye kweli amejitoa kihali na mali kumpigania Mtz ambapo inasikitisha kuwa leo wapo ndani yetu wanaombeza..... of course ni kwawaida kwani mara zote unapoishi duniani lazima wawepo wanaokupenda na wanaokuchukia kinyume cha hapo basi lazima una tatizo. Big up Mh. Mbowe, Big up Mh. Slaa, Big up CC CDM na wengine wote wenye mapenzi mema na wanaotaka ukombozi wa kweli CDM

Kwa tahmini yangu ya haraka haraka juu ya utendaji wa viongozi wangu, ni Mkiti na Katibu amabo utendaji wao unazidi wenyeviti na makatibu wote east and central Africa. Chini yao chadema imepata mafanikio makubwa na kuongeza mizizi yake mpaka kwenye grass root level. Hili linajidhihirisha katika namna mbalimbali, 1. idadi ya wabunge toka 5 - zaidi ya 45 hivi sasa, kuongezeka kwa utawala wa CDM mpaka kiwango cha vitongoji, mabadiliko ya haraka na kazi kama vile CDM kuongoza halmashauri ndogo Arumeru muda mfupi tu toka uchaguzi mkuu lakini pia kwa mtidno uleule kuchukua Jimbo la Arumeru magharibi kwa kishindo kikubwa na kutoa upinzani mkali igunga pamoja na hujuma kubwa zilizofanyika huko, lakini moja kati ya mafanikio ya uongozi huu ni hamasa/ari kubwa nadani ya wananchi hivi sasa Tanzania ya kujua na kudai haki zao, jambo ambalo Mkiti wakati wote amekuwa akiliosema kama moja ya vitu ambavyo anavisimamia kuvijenga, ili hata kama CDM itachukua madaraka isiswaburuze wananchi bali iwajibike kwao. Yapo mengi ya kurejea kama mafanikio ya uongozi huu, wana JF wema hebu sasa tupate muda wa kuyaorodhesha yote ili malumbano haya yasiendelee kwa watu kuzomeana tu ila pia yatoe somo na watu wauone ukweli, nina imani kuwa ukweli huongea vizuri zaidi kuliko matusi au kuzomeana?????, nilichogundua hapa ni kwamba watu hawasomi hata magazeti kujua dhana fulani fulani, ni muhimu sana sasa tuusome waraka ule wa akina zitto wa kutaka mabadiliko ya uongozi na kuu critic kwa hoja bila hivyo tutapoteza muda na kutoka bila elimu wala kupanuana mawazo.

Kuhusu ZZK kwa kweli nimekuwa mfuasi wake bali wa mashaka (Urafiki wa mashaka) nimempenda kwa hoja zake mbali mbali japo mara zote nimekuwa nikikatishwa tamaa na namna ambavyo amekuwa akikosa udhati wa kuonyesha nia halisi ya kushughulikia yale anayodai kuyasimamia, nilimpenda sana kipindi alipotolewa nje ya bunge na kufanya Operesheni sangara, labdas hili ndilo pekee lililonikosha zaidi juu yake. Vinginevyo anaonekana zaidi katika mazingira yenye mashaka mashaka na kwa haraka haraka namuona Zitto Akiwasiliana sana na Mkurugenzi TISS 2010 katika kipindi kigumu CDM ikichakachuliwa juu ya matokeo ya urais/ubunge wakati ambapo Dr Slaa akilalamikia matokeo ya urais; Namuona zzk akitweet haraka sana kwa urahisi wakati wa matokeo kule Igunga akikiri CDM kushindwa eti kwa sababu chama hakijajengeka vijijini (Hata kwa matokeo yale yaliyochakachuliwa usemi wa zzk hauna ukweli na hasa ukizingatia ndio kwa mara ya kwanza CDM ilisimamisha mgombea), namuona zzk akifanya bidii kuahakikisha Pinda, Dewji, Mkono n.k akipambana kukihujumu CDM na wagombea wake ili CCM na maswahiba wake wapite bila kupingwa, namuona zzk akigoma kutoka nje ya Bunge rais alipokwenda kulihutubia eti kwa vile amemjengea barabara nk (Hapa uanaona ubinafsi wa dhahiri wa mbunge ambae leo nataka zugukia sehemu zote tanzania ati Mzalendo), namuona zzk ikulu akigonga glasi na rais kumpongeza kwa baraza jipya la mawaziri wakati M/kiti wake yupo Arusha akilaani kitendo cha katiba kuvunjwa kwa kuchguliwa baadhi ya mawaziri, Mh Mwinyi kushika wizara ambazo si za muungano, namuona zzk akiwa mabli na viongozi wenake nyakati zote - Akijitenga, Namuona zzk akiwa mbele kwenye ajenda ya kutaka uongozi wa juu kwa udi na uvumba bila staha- Urais, uenyekiti, uongozi wa upinzani bungeni (taamaa ya madaraka; namuona zzk akienda Anticlockwise wakati wenzake wakienda clockwise nk. Nabaki mwenye mashaka makubwa juu ya uzalendo na ukweli wake na sasa namuona ni msalitit anaepaswa kufukuzwa chama tu.

Ukweli hapa kulingana na mtazamo wangu ni kuwa zzk kwa kutofautina na uongozi wote amepoteza sifa na hawezi kubaki cdm, this does not need rocket sayansi kulitambua, ni wazi kuwa atatapata wana cdm wanaomuunga mkono lakini wale ambao hwapo uongozini kumbe itakuwa ngumu kwake kuongoza cdm, haiwezekani wewe peke zako ukaongoza chama katika mazingira ambayo cdm imefikia, hilo linawezekana UDP, TLP, UDP etc etc.

Ukweli ni kwamba M/kiti na katibu CDM wamekuwa mwiba kwa CCM kwani wamevaaa sura ya serikali mbadala inyojihidhirisha ndani ya uongozi thabiti wa kutohongeka na kujitolea kwa hali na mali, lakini pia muamko na ari kubwa ya watanzania juu ya CDM uliotokana na uongozi wao. Wote tutakiri jinsi ambavyo watanzania wamekuwa mbele kuichangia cdm hata kwa mpesa mpaka hujuma ya kukata kodi ya mabilioni toka CDM m-pesa ilipotungwa. Mh. Mbowe hakuzivaa combat kwa bahati mbaya au kifasheni zaidi kama ambavyo inaonekana sasa bali vazi lile liliendana fika na mwandani wake, ukweli, nia, thirika na utendaji wake. Niliwahi safiri na dada mmoja ambae aliwahi fanya kazi na mbowe, akanithibitishia hilo, kwamba Mbowe ni mtu ambae akishaamua kufanya kitu akaanza basi ni mpaka akimalize/akikamilishe, akanimabia kwamba wakati akijenga Bilicanas alikesha usiku na mchana site aliondoka asubuhi tu tena kwa muda mfupi kwenda kwa Bfast kubadili nguo na kurudi site kwa mkesha mwingiine, alipokuta mkewe anadunduliza ili ajenge nyumba yao kisiri, aliingilia kati plan hiyo kuanza na kujenga nyumba nadni ya mwezi mmoja nk, hii ilinikumbusha muda wote hata kabla chadema haijafika hapa Mbowe akizunguka kwa kampeni zake za urais akitumia Helikopta kuhutubia vijijini pamoja na kukijenga chama akiibua hamasa ya mabadiliko.
Hakika sura yake na Dr. Slaa katika siasa za tz inatisha ccm ndio maana wanatafuta mamluki ili kile kilichotokea NCCR kijirudie....Tulianza na mungu tutamaliza na mungu.

Wana JF, mkakati wa zzk, kitila na Mwigamba haupaswi kuungwa mkono kwa namna yeyote sio tu na CDM au wanachama wake bali wanamageuzi wote Tz. Ni kweli katka chama au jamii kwa ujumla hakukosekani makundi lakini makundi hayo yasiwe ya mafungate au kimtandao bali ya hoja na yenye afya kwa chama kwa maana watu watafungama na hoja sio mtu fulani. Hili ndilo linalowasumbua ccm hata leo, ndio maana wanashindwa kuwajibishana, kujivua magamba nk. Raisi Kikwete alipokutana na makatibu wa Wilaya/Mikoa dodoma aliongea kama analia tu hana meno kwa ajili ya mtandao ndani ya ccm akaishia kuwalalamimikia kwamba mtindo wao wa kuchukua posho za simu kila mwezi wa laki mbili kila mwezi utakiua chama, haya ndio matokeo ya Mitandao. Katika mtindo wa mitandao watu hawatahoji CDM imesema nini bali nani kasema ndani ya cdm, kiwe cha ujinga au busara ili mradi kasema zzk sawaaaaa!!!! akasema mbowe holaaaaaaa!!!!!!!! Slaa mjinga!!!!!!!!!!!!!, tusifike hukoooo hakuna maslahi ya taifa hili.

Mh. Mbowe & Slaa, zzk na waheshimiwa wote wenye nia nzuri, ukiona unapingana na wengi ndani ya CDM its time to quit, ndio taratibu za siasa!!!! Mwl. Nyerere aliwahi kumshangaa Mh. Kawawa kwamba anadai hwezi toka ccm!!! yeye akaweka bayana kabisa kuwa ccm sio babake wala mama kwamba huwezi mbadili na kwamba kwamba ccm haitatekeleza kile anachoamini ataondoka....!!! Lyatonga Mrema laifanya hivyo mara kadhaa na wakati wote wafuasi wake walimfuata. Mh zzk ni wazi kwangu wewe unapingana na wenzako na kwa hali hii nakushauri utoke na wafuasi wako watakufuata tuu...... Vinginevyo hisia za watu kwamba --------- na ccm zitaongezeka kwani itakuwa kama vile kukimbia kazi ambayo umeshalipwa kumbe uanang'ang'ania ili kuikamilisha...... Tazama Damu za watu zimeshamwagika kuipigania CDM na ukombozi wa taifa hili sehemu nyingi, kkwa mzalendo halisi angekubali kupoteza maslahi yake ili chama hiki kifike mahali kutoa heshima ya damu iliyomwagika, na mungu afurahie hilo, usikatize mapango wa mungu laana itakufuata kwani damu ya wanyonge hawa bado inalia juu ya taifa hili

Aluta Continua CDM

Mungu ibariki CDM... Mungu ibariki TZ

Tulianza na mungu.... Tutamaliza na Mungu, Amen.
Mkuu Njopa, mtu unapoamua kujikomba komba kwa viongozi wabovu, huna haja ya kuandika posti ndeefu, maneno machache tuu yangetosha mfano uliposema utendaji wao unazidi wenyeviti na makatibu wa vyama vyote East and Central Africa,, ingetosha!.
Kiukweli kuna baadhi ya mashabiki wa Chadema sijui wanatumia nini kufikiri?!.

Pasco
 
Wekeni threads za kujenga chama sio kutupotezea muda wa kujadili indivisual issues
 
Mnyika hakupaswa kujiingiza kwenye hili.hakuwa na sababu ya kujiweka kwenye level ya akina Lema,Msigwa na Sugu.Ni kujidharirisha.

Bila kujua,amejishushia heshima katika hili.

Kwa hiyo mlitaka afanye nini? Akae kimya wakati yeye ni msemaji wa chama? Au mlitaka apingane na maamuzi ya chama ili tu awafurahishe nyie? Ametumia haki yake na busara kama kiongozi kuunga mkono maamuzi ya chama. Hivi hamjui maana ya collective responsibility kwenye maamuzi ya kama hayo?

Wamarekani weusi wanapenda kusema "when you're with your N....a and he starts war you are supposed to roll with him even if he's wrong, you will tell him later that he was wrong"
 
Call me what you may, it's not gonna change my status !.
Mtu wa kwanza kumuita JK ni dhaifu ni mimi kupitia uzi huu na wengi mlinipongeza mkiniita bold!.
Mtu wa kwanza kusema CCM imechokwa ni mimi kupitia uzi huu, na wengi mlinipongeza!.
Niliposema Chadema Haijajipanga, hili ndilo likawa kosa, nikaanza kuitwa gamba!.

Kiukweli kutoka ndani ya nafsi yangu sina chama ila kuna ninawakubali sana kwa Chadema ni ZZK, kwa CCM ni EL, na kwa CUF ni Jussa!.
Pasco.

Zito ni Mbunge wa Mahakama
 
kama baraza kuu litashidwa maamuzi ya kawaida kama haya ,,,basi CDM itakua ni tawi la CCM,,,kama washidwa kuamua kwa umoja dhidi ya kibaraka, msaliti, basi CDM itakuwa si chama makini,,,,,kama watashidwa kufanya maamuzi mepesi kabisa kwa sababu ya kuhogwa je KURA 2015 wataweza kulinda......Kama mimi mwanachama wa kawaida nahasira hivi je mtu ambaye ni baraza kuu itakuaje,,,,,Mimi ningekuwa huko baraza kuu si kumfukuza tu mimi hata MAKOFI angeyapata

Wewe naona unatafuta bwana, humu JF sio mahali pake ni bora ukaenda facebook huko utampa bwana!:A S wink:
 
Kwa wanaojua msimamo wa Mdee, tunaelewa kwa nini yuko kimya!. Pia ameisha jua madhambi ya Chadema kufanya fault finding cherry picking za kuwahukumu watu kwa makosa yao tuu regardless wameifanyia nini Chadema. Anajijua aliingiaje Chadema, what was her inspiration hadi kujoin Chadema. Wewe umemuona Halima tuu?!. Hujiulizi mbona Prof. Safari yuko kimya?.
Pasco

Je Prof Safari ni member wa CC ya CHADEMA? Kwa kawaida huwa sio mtu wa kuongea.....hata kwenye suala la ushindi wa Kashinje mahakamani alikataa kuongea.....kwenye vipindi vya kiswahili TBC mpaka mtangazaji humuuliza Profesa mbona kimya?
 
Mijitu imekariri,kuona mtu ameliongelea hili mlitaka mpaka aje JF???? ubongo kama wa kuku'
 
kimya KINGI HUWA KINA MSHINDO MKUU. lazima halaima anaegemea kwa kamati kuu ambayo naye si mjumbe walakini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom