Hongera HALIMA MDEE umeonyesha ukomavu

Hongera HALIMA MDEE umeonyesha ukomavu

Status
Not open for further replies.
@Njepo if wishies were horses' CDM to U could have been history!!
Bahati mbaya kwenu CDM inazidi kupata nguvu!!
Wewe njoo vijini uone ukweli, wacha kujidanganya kwenye keyboard!!

hili ndo lililonifurahisha na linalonifurahisha
 
ukimya nao una tafsiri nyingi sana, inawezekana moyoni ana fukuto kubwa lakini akiwaza na kuwazua anaona atapoteza so she decided to stay quite
 
Mmbeya na wewe BABU SLAA na JOSEPHINE mnaofanya fitna za kumuondoa HALIMA MDEE KAWE ,ili JOSEPHINE agombee mnafikiri hatujui mambo yenu, kaa kushoto wewe choko wa tandale.

hivi kwa nini josephine mushumbuzi analitaka sana jimbo la halima mdee,kwani hakuna majimbo mengine mpaka jimbo la kawe tu
 
Wewe kweli kilaza,unawajua wasemaji wa cdm wewe? ulitaka kila mtu aongee bila itifaki kuzingatiwa? mnyika ni msemaji wa chama kwa kukusaidia! div 5 kweli majanga.

anafijiri cdm ni km ccm ambako kila mtu anaongea tu na kutoa tamko, itifaki lzm izingatiwe
 
Unaonyesha ulivyo juha zaidi ya JUHA KALULU,Mnyika ni mkurugenzi wa habari wa chama kwa mawazo yako asiyasemee maamuzi ya chama?Kumbuka anaweza kuwa hayaungi mkono lkn ndio yameshapitishwa hanabudi kutujuza na kuyatetea la sivyo hafai kwa nafasi ya uongozi
kuna tofauti ya kutoa taarifa na kuwa shabiki wa taarifa unayoitoa...angeishia kutoa taarifa maelezo yako yangejaa mantiki.
 
ukimya nao una tafsiri nyingi sana, inawezekana moyoni ana fukuto kubwa lakini akiwaza na kuwazua anaona atapoteza so she decided to stay quite
busara inakutaka usikilize zaidi kuliko kusema..so hata kama amesema au atakuja kusema,,ni wazi ametumia busara kusikiliza zaidi.
 
Kwa wanaojua msimamo wa Mdee, tunaelewa kwa nini yuko kimya!. Pia ameisha jua madhambi ya Chadema kufanya fault finding cherry picking za kuwahukumu watu kwa makosa yao tuu regardless wameifanyia nini Chadema. Anajijua aliingiaje Chadema, what was her inspiration hadi kujoin Chadema. Wewe umemuona Halima tuu?!. Hujiulizi mbona Prof. Safari yuko kimya?.
Pasco

Huwa sikuelewi kabisa.
 
kama baraza kuu litashidwa maamuzi ya kawaida kama haya ,,,basi CDM itakua ni tawi la CCM,,,kama washidwa kuamua kwa umoja dhidi ya kibaraka, msaliti, basi CDM itakuwa si chama makini,,,,,kama watashidwa kufanya maamuzi mepesi kabisa kwa sababu ya kuhogwa je KURA 2015 wataweza kulinda......Kama mimi mwanachama wa kawaida nahasira hivi je mtu ambaye ni baraza kuu itakuaje,,,,,Mimi ningekuwa huko baraza kuu si kumfukuza tu mimi hata MAKOFI angeyapata

Hizi tabia za kupiga wake zenu halafu mnajiona mnaweza kupiga kila mtu zitawtokea puani
 
Are you Zitto?
Nimekuuliza hivyo kwa sababu unamsema mnyika,
Mimi nilisema kama mimi kuwa Mnyika disapointed me.
Wewe umemsemea Mnyika kwamba mimi nimem'disapoint Mnyika.
 
kinachochekesha kwenye siasa ni kumkuta mfuasi anasema kwa niaba ya yule anayemfuasia, unawapata wapi hiyo mamlaka wewe shabiki tu?
 
Mwalimu J.K.NYERERE """""alieleza kuwa dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu........amin msiamini huu ndo mwanzo wa kutafunana ndani ya CDM na hawatokaa salama milele......., wabunge wote wa CHADEMA kwa namna moja au nyingine tumewajua wapo upande upi! Kimsingi nampongeza Mbunge wa Kawe HALIMA MDEE kwa kukaa kimya, kutotoa neno lolote ambalo kwa namna moja au nyingine lingeendelea kukuza mgogoro! CHADEMA igeni kwa mwana Mama HALIMA MDEE kawashinda busara wanaume wote ndani ya CHADEMA upeo wa kufikiri! Nakushauri usije comment chochote juu ya hili sakata utajijengea heshima kubwa kwa nchi hiii

Hawo kina Halima Mdee ndio akina Mama wa vifaranga ambao ndugu Zitto alikuwa anawataka waje Kortini alisema hapendi kupigishana kelele na vifaranga anamtaka mama yao ndio akina Halima Mdee na Dr slaa baba wa vifaranga.,
 
Wewe mleta maada una lako jambo cyo bure,unamtaka halima aseme nini na ili iwe nini????????????????????????/.
 
Sasa PhD nikisema wewe ni mchochezi utakataa??
Hayo mambo ya Mzee Slaa, Josephina eti wamtoe Halima Kawe umeyatoa wapi??
Dar majimbo ya ubunge yamekwisha???
Wacha kupandiza ujinga, hata feri huwezi kuuza huo upuuzi!!

Subiri nije niweke nyaraka na audio clips za uthibitisho, huu sio uchochezi HALIMA MDEE kushalalmika kwa uwazi kabisa kuwa SLAA anamuandalia KAWE JOSEPHINE
 
Mwalimu J.K.NYERERE """""alieleza kuwa dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu........amin msiamini huu ndo mwanzo wa kutafunana ndani ya CDM na hawatokaa salama milele......., wabunge wote wa CHADEMA kwa namna moja au nyingine tumewajua wapo upande upi! Kimsingi nampongeza Mbunge wa Kawe HALIMA MDEE kwa kukaa kimya, kutotoa neno lolote ambalo kwa namna moja au nyingine lingeendelea kukuza mgogoro! CHADEMA igeni kwa mwana Mama HALIMA MDEE kawashinda busara wanaume wote ndani ya CHADEMA upeo wa kufikiri! Nakushauri usije comment chochote juu ya hili sakata utajijengea heshima kubwa kwa nchi hiii


kwa vile bado una nafuu kidogo wahi mirembe ukalazwe mapeeema kabla hujapelekwa ukiwa umefungwa kamba miguu na mikono na hujaanza kuokoteza makopo.
 
Sina shaka kabisa na msimamo wala maamuzi ya cdm juu ya Zitto na ninaunga mkono hilo kwa 100% kumuondoa ndani ya CDM. Shaka niliyonayo ni moja tu, kwamba taratibu na katiba ya kumchukulia hatua zzk huenda zilikuwapo na ndio zinazotugharimu CDM leo na katika kesi hii, lakini pia nna imani hatimae tutashinda. Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu....

Toka awali nimekuwa na imani kubwa sana kwa mwenyekiti na katibu wake, na tukio hili linaidhihirisha imani yangu kwao zaidi kwani yale niloyajengea imani sqasa yanathibitika, vivyo hivyo toka awali nilikua na shak sana juu ya mwenendo thabiti wa zzk na leo hili pia linathibitsha kwangu kuwa zzk si mkweli na hapaswi kuungwa mkono asilani.

Mh. Mbowe, ni mtu ambaye kweli amejitoa kihali na mali kumpigania Mtz ambapo inasikitisha kuwa leo wapo ndani yetu wanaombeza..... of course ni kwawaida kwani mara zote unapoishi duniani lazima wawepo wanaokupenda na wanaokuchukia kinyume cha hapo basi lazima una tatizo. Big up Mh. Mbowe, Big up Mh. Slaa, Big up CC CDM na wengine wote wenye mapenzi mema na wanaotaka ukombozi wa kweli CDM

Kwa tahmini yangu ya haraka haraka juu ya utendaji wa viongozi wangu, ni Mkiti na Katibu amabo utendaji wao unazidi wenyeviti na makatibu wote east and central Africa. Chini yao chadema imepata mafanikio makubwa na kuongeza mizizi yake mpaka kwenye grass root level. Hili linajidhihirisha katika namna mbalimbali, 1. idadi ya wabunge toka 5 - zaidi ya 45 hivi sasa, kuongezeka kwa utawala wa CDM mpaka kiwango cha vitongoji, mabadiliko ya haraka na kazi kama vile CDM kuongoza halmashauri ndogo Arumeru muda mfupi tu toka uchaguzi mkuu lakini pia kwa mtidno uleule kuchukua Jimbo la Arumeru magharibi kwa kishindo kikubwa na kutoa upinzani mkali igunga pamoja na hujuma kubwa zilizofanyika huko, lakini moja kati ya mafanikio ya uongozi huu ni hamasa/ari kubwa nadani ya wananchi hivi sasa Tanzania ya kujua na kudai haki zao, jambo ambalo Mkiti wakati wote amekuwa akiliosema kama moja ya vitu ambavyo anavisimamia kuvijenga, ili hata kama CDM itachukua madaraka isiswaburuze wananchi bali iwajibike kwao. Yapo mengi ya kurejea kama mafanikio ya uongozi huu, wana JF wema hebu sasa tupate muda wa kuyaorodhesha yote ili malumbano haya yasiendelee kwa watu kuzomeana tu ila pia yatoe somo na watu wauone ukweli, nina imani kuwa ukweli huongea vizuri zaidi kuliko matusi au kuzomeana?????, nilichogundua hapa ni kwamba watu hawasomi hata magazeti kujua dhana fulani fulani, ni muhimu sana sasa tuusome waraka ule wa akina zitto wa kutaka mabadiliko ya uongozi na kuu critic kwa hoja bila hivyo tutapoteza muda na kutoka bila elimu wala kupanuana mawazo.

Kuhusu ZZK kwa kweli nimekuwa mfuasi wake bali wa mashaka (Urafiki wa mashaka) nimempenda kwa hoja zake mbali mbali japo mara zote nimekuwa nikikatishwa tamaa na namna ambavyo amekuwa akikosa udhati wa kuonyesha nia halisi ya kushughulikia yale anayodai kuyasimamia, nilimpenda sana kipindi alipotolewa nje ya bunge na kufanya Operesheni sangara, labdas hili ndilo pekee lililonikosha zaidi juu yake. Vinginevyo anaonekana zaidi katika mazingira yenye mashaka mashaka na kwa haraka haraka namuona Zitto Akiwasiliana sana na Mkurugenzi TISS 2010 katika kipindi kigumu CDM ikichakachuliwa juu ya matokeo ya urais/ubunge wakati ambapo Dr Slaa akilalamikia matokeo ya urais; Namuona zzk akitweet haraka sana kwa urahisi wakati wa matokeo kule Igunga akikiri CDM kushindwa eti kwa sababu chama hakijajengeka vijijini (Hata kwa matokeo yale yaliyochakachuliwa usemi wa zzk hauna ukweli na hasa ukizingatia ndio kwa mara ya kwanza CDM ilisimamisha mgombea), namuona zzk akifanya bidii kuahakikisha Pinda, Dewji, Mkono n.k akipambana kukihujumu CDM na wagombea wake ili CCM na maswahiba wake wapite bila kupingwa, namuona zzk akigoma kutoka nje ya Bunge rais alipokwenda kulihutubia eti kwa vile amemjengea barabara nk (Hapa uanaona ubinafsi wa dhahiri wa mbunge ambae leo nataka zugukia sehemu zote tanzania ati Mzalendo), namuona zzk ikulu akigonga glasi na rais kumpongeza kwa baraza jipya la mawaziri wakati M/kiti wake yupo Arusha akilaani kitendo cha katiba kuvunjwa kwa kuchguliwa baadhi ya mawaziri, Mh Mwinyi kushika wizara ambazo si za muungano, namuona zzk akiwa mabli na viongozi wenake nyakati zote - Akijitenga, Namuona zzk akiwa mbele kwenye ajenda ya kutaka uongozi wa juu kwa udi na uvumba bila staha- Urais, uenyekiti, uongozi wa upinzani bungeni (taamaa ya madaraka; namuona zzk akienda Anticlockwise wakati wenzake wakienda clockwise nk. Nabaki mwenye mashaka makubwa juu ya uzalendo na ukweli wake na sasa namuona ni msalitit anaepaswa kufukuzwa chama tu.

Ukweli hapa kulingana na mtazamo wangu ni kuwa zzk kwa kutofautina na uongozi wote amepoteza sifa na hawezi kubaki cdm, this does not need rocket sayansi kulitambua, ni wazi kuwa atatapata wana cdm wanaomuunga mkono lakini wale ambao hwapo uongozini kumbe itakuwa ngumu kwake kuongoza cdm, haiwezekani wewe peke zako ukaongoza chama katika mazingira ambayo cdm imefikia, hilo linawezekana UDP, TLP, UDP etc etc.

Ukweli ni kwamba M/kiti na katibu CDM wamekuwa mwiba kwa CCM kwani wamevaaa sura ya serikali mbadala inyojihidhirisha ndani ya uongozi thabiti wa kutohongeka na kujitolea kwa hali na mali, lakini pia muamko na ari kubwa ya watanzania juu ya CDM uliotokana na uongozi wao. Wote tutakiri jinsi ambavyo watanzania wamekuwa mbele kuichangia cdm hata kwa mpesa mpaka hujuma ya kukata kodi ya mabilioni toka CDM m-pesa ilipotungwa. Mh. Mbowe hakuzivaa combat kwa bahati mbaya au kifasheni zaidi kama ambavyo inaonekana sasa bali vazi lile liliendana fika na mwandani wake, ukweli, nia, thirika na utendaji wake. Niliwahi safiri na dada mmoja ambae aliwahi fanya kazi na mbowe, akanithibitishia hilo, kwamba Mbowe ni mtu ambae akishaamua kufanya kitu akaanza basi ni mpaka akimalize/akikamilishe, akanimabia kwamba wakati akijenga Bilicanas alikesha usiku na mchana site aliondoka asubuhi tu tena kwa muda mfupi kwenda kwa Bfast kubadili nguo na kurudi site kwa mkesha mwingiine, alipokuta mkewe anadunduliza ili ajenge nyumba yao kisiri, aliingilia kati plan hiyo kuanza na kujenga nyumba nadni ya mwezi mmoja nk, hii ilinikumbusha muda wote hata kabla chadema haijafika hapa Mbowe akizunguka kwa kampeni zake za urais akitumia Helikopta kuhutubia vijijini pamoja na kukijenga chama akiibua hamasa ya mabadiliko.
Hakika sura yake na Dr. Slaa katika siasa za tz inatisha ccm ndio maana wanatafuta mamluki ili kile kilichotokea NCCR kijirudie....Tulianza na mungu tutamaliza na mungu.

Wana JF, mkakati wa zzk, kitila na Mwigamba haupaswi kuungwa mkono kwa namna yeyote sio tu na CDM au wanachama wake bali wanamageuzi wote Tz. Ni kweli katka chama au jamii kwa ujumla hakukosekani makundi lakini makundi hayo yasiwe ya mafungate au kimtandao bali ya hoja na yenye afya kwa chama kwa maana watu watafungama na hoja sio mtu fulani. Hili ndilo linalowasumbua ccm hata leo, ndio maana wanashindwa kuwajibishana, kujivua magamba nk. Raisi Kikwete alipokutana na makatibu wa Wilaya/Mikoa dodoma aliongea kama analia tu hana meno kwa ajili ya mtandao ndani ya ccm akaishia kuwalalamimikia kwamba mtindo wao wa kuchukua posho za simu kila mwezi wa laki mbili kila mwezi utakiua chama, haya ndio matokeo ya Mitandao. Katika mtindo wa mitandao watu hawatahoji CDM imesema nini bali nani kasema ndani ya cdm, kiwe cha ujinga au busara ili mradi kasema zzk sawaaaaa!!!! akasema mbowe holaaaaaaa!!!!!!!! Slaa mjinga!!!!!!!!!!!!!, tusifike hukoooo hakuna maslahi ya taifa hili.

Mh. Mbowe & Slaa, zzk na waheshimiwa wote wenye nia nzuri, ukiona unapingana na wengi ndani ya CDM its time to quit, ndio taratibu za siasa!!!! Mwl. Nyerere aliwahi kumshangaa Mh. Kawawa kwamba anadai hwezi toka ccm!!! yeye akaweka bayana kabisa kuwa ccm sio babake wala mama kwamba huwezi mbadili na kwamba kwamba ccm haitatekeleza kile anachoamini ataondoka....!!! Lyatonga Mrema laifanya hivyo mara kadhaa na wakati wote wafuasi wake walimfuata. Mh zzk ni wazi kwangu wewe unapingana na wenzako na kwa hali hii nakushauri utoke na wafuasi wako watakufuata tuu...... Vinginevyo hisia za watu kwamba --------- na ccm zitaongezeka kwani itakuwa kama vile kukimbia kazi ambayo umeshalipwa kumbe uanang'ang'ania ili kuikamilisha...... Tazama Damu za watu zimeshamwagika kuipigania CDM na ukombozi wa taifa hili sehemu nyingi, kkwa mzalendo halisi angekubali kupoteza maslahi yake ili chama hiki kifike mahali kutoa heshima ya damu iliyomwagika, na mungu afurahie hilo, usikatize mapango wa mungu laana itakufuata kwani damu ya wanyonge hawa bado inalia juu ya taifa hili

Aluta Continua CDM

Mungu ibariki CDM... Mungu ibariki TZ

Tulianza na mungu.... Tutamaliza na Mungu, Amen.

Mwalimu J.K.NYERERE """""alieleza kuwa dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu........amin msiamini huu ndo mwanzo wa kutafunana ndani ya CDM na hawatokaa salama milele......., wabunge wote wa CHADEMA kwa namna moja au nyingine tumewajua wapo upande upi! Kimsingi nampongeza Mbunge wa Kawe HALIMA MDEE kwa kukaa kimya, kutotoa neno lolote ambalo kwa namna moja au nyingine lingeendelea kukuza mgogoro! CHADEMA igeni kwa mwana Mama HALIMA MDEE kawashinda busara wanaume wote ndani ya CHADEMA upeo wa kufikiri! Nakushauri usije comment chochote juu ya hili sakata utajijengea heshima kubwa kwa nchi hiii
 
Mnyika hakupaswa kujiingiza kwenye hili.hakuwa na sababu ya kujiweka kwenye level ya akina Lema,Msigwa na Sugu.Ni kujidharirisha.

Bila kujua,amejishushia heshima katika hili.

Sasa John Mnyika angefanyaje nwakati ye ndie msemji wa chama? Naye pia hatupaswi kumlaum directly. Ila hongera sana MDEE.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom