Hongera Dkt. Tulia. Sasa unatosha kuchukua kijiti 2030

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Nianze kwa kukupa pongezi kwa ushindi wako. Umeliwakilisha vyema taifa. Hongera sana

Nimeangalia ulivyojinadi. Kusema kweli umeonesha uwezo wako kama mwanamke mahiri.

Ujumbe wangu kwako Dkt Tulia- Jijenge vizuri kimataifa, jijenge vizuri kuijua Dunia na Siasa zake. Jipe muda kujifunza sana na kwa kila unalojifunza jifunze pia namna ya kulifanyia utekelezaji.

Ujumbe wangu kwa Rais Samia- Naona umemuona Tulia. Najua hata faili lake unaweza kulipata na kulipitia. Kusema kweli mwanamke mwenzako anaweza. Mjenge vizuri, mpe exposure, mjenge aendeleze haya mazuri yote unayoyafanya sana hasa katika kujenga uchumi imara kupitia sekta binafsi pale utakapomaliza uongozi wako. Mpe exposure apate kujifunza vizuri geopolitics. Na mwisho ikikupendeza chama chako kimpe kijiti akapeperushe bendera ya chama 2030.

Kwa CCM- Najua coming 2030 kuna Mwigulu na Makamba. Najua wamejijenga sana na wanajijenga sana. Ila muangalieni vizuri Dkt. Tulia. Mjengeni kichama na kimataifa. Aijue Dunia na siasa zake ili ajifunze kipi tunatakiwa kukifanya kuendana na kasi dunia inayoenda. Msimfundishe udiktekta bali kutumia akili, busara na maarifa kama anavyofanya Rais Samia. Nchi inahitaji consistence ili ipate maendeleo ya kweli.

Mjengeni Tulia afanye haya mazuri anayoyafanya Samia ili kuwe na consistence na mwisho tuwe nchi ya maziwa na asali. Tusirudi tena nyuma.

Kwa wana Mbeya- Mmemuona Tulia. Anaweza na kweli anaweza. Kikubwa mleeni awe kiongozi bora. Mpeni ushirikiano na jifunzeni kulingia watu wenu wenye mafanikio kwa kuwa mafanikio ya watu wenu ni mafanikio yenu. Mbeya ni jiji lenye hali nzuri ya hewa nadhani kuliko mikoa yote hapa Tanzania ila mnahitaji viongozi wazuri muijenge vizuri mbeya yenu. Mmepata Tulia mtumieni vizuri.

Asanteni
Lord Denning
Kigali
 
Unampongeza kwa uwezo upi anaouonesha huko nje kwenye kujinadi, wakati akiwa pale bungeni anageuka mpiga debe wa Samia?

Mtu asiye na msimamo hafai kuongoza popote, na kwa tabia zake kule bungeni, anaonesha wazi hata huko nje alipochaguliwa atakuja kugeuka kituko mbele ya safari.

Tulia ameshaonesha kwa vitendo sio wa kumuamini na wala hajiamini zaidi ya maneno yake matupu, huo ushindi wake ni kwa mbinu za kitapeli tu.
 
Nimeangalia ulivyojinadi. Kusema kweli umeonesha uwezo wako kama mwanamke mahiri...
Imagine 2025 raisi Samia amchague Dr Tulia kuwa mgombea mwenza wa uraisi na baadae awe makamu wa raisi.

Alafu Makonda agombee ubunge na baadae apitishwe kuwa spika wa bunge.

I hope kuna watu watakufa kwa presha ya "wasiempenda kaja" 🤣🤣🤣
 
Unampongeza kwa uwezo upi anaouonesha huko nje kwenye kujinadi, wakati akiwa pale bungeni anageuka mpiga debe wa Samia?

Mtu asiye na msimamo hafai kuongoza popote, na kwa tabia zake kule bungeni, anaonesha wazi hata huko nje alipochaguliwa atakuja kugeuka kituko mbele ya safari.

Tulia ameshaonesha kwa vitendo sio wa kumuamini na wala hajiamini zaidi ya maneno yake matupu, huo ushindi wake ni kwa mbinu za kitapeli tu.
Tupe uthibitisho wa kutokuwa na msimamo kwake?

Ameoneshaje kuwa sio wa kumuamini? Kuna uthibitisho wa mtu kuaminiwa zaidi ya kura 172 alizopata kwenye uchaguzi wa IPU?
 
Nianze kwa kukupa pongezi kwa ushindi wako. Umeliwakilisha vyema taifa. Hongera sana

Nimeangalia ulivyojinadi. Kusema kweli umeonesha uwezo wako kama mwanamke mahiri.

Ujumbe wangu kwako Dkt Tulia- Jijenge vizuri kimataifa, jijenge vizuri kuijua Dunia na Siasa zake. Jipe muda kujifunza sana na kwa kila unalojifunza jifunze pia namna ya kulifanyia utekelezaji.

Ujumbe wangu kwa Rais Samia- Naona umemuona Tulia. Najua hata faili lake unaweza kulipata na kulipitia. Kusema kweli mwanamke mwenzako anaweza. Mjenge vizuri, mpe exposure, mjenge aendeleze haya mazuri yote unayoyafanya sana hasa katika kujenga uchumi imara kupitia sekta binafsi pale utakapomaliza uongozi wako. Mpe exposure apate kujifunza vizuri geopolitics. Na mwisho ikikupendeza chama chako kimpe kijiti akapeperushe bendera ya chama 2030.

Kwa CCM- Najua coming 2030 kuna Mwigulu na Makamba. Najua wamejijenga sana na wanajijenga sana. Ila muangalieni vizuri Dkt. Tulia. Mjengeni kichama na kimataifa. Aijue Dunia na siasa zake ili ajifunze kipi tunatakiwa kukifanya kuendana na kasi dunia inayoenda. Msimfundishe udiktekta bali kutumia akili, busara na maarifa kama anavyofanya Rais Samia. Nchi inahitaji consistence ili ipate maendeleo ya kweli.

Mjengeni Tulia afanye haya mazuri anayoyafanya Samia ili kuwe na consistence na mwisho tuwe nchi ya maziwa na asali. Tusirudi tena nyuma.

Kwa wana Mbeya- Mmemuona Tulia. Anaweza na kweli anaweza. Kikubwa mleeni awe kiongozi bora. Mpeni ushirikiano na jifunzeni kulingia watu wenu wenye mafanikio kwa kuwa mafanikio ya watu wenu ni mafanikio yenu. Mbeya ni jiji lenye hali nzuri ya hewa nadhani kuliko mikoa yote hapa Tanzania ila mnahitaji viongozi wazuri muijenge vizuri mbeya yenu. Mmepata Tulia mtumieni vizuri.

Asanteni
Lord Denning
Kigali
Ni mwizi wa kura, hicho cheo ameshinda maana hakina maana yoyote. Ni sawa na kuona mtoto wako ana uwezo kisa Kawa class monitor. Nimegundua ni cheo kisicho na vetting yoyote, ili mradi mtu kafika na kachukua form, hakuna namna yoyote ya kujiridhisha na uadilifu wake huko atokako.
 
Ujumbe wangu kwa Rais Samia- Naona umemuona Tulia. Kusema kweli mwanamke mwenzako anaweza. Mjenge vizuri, mpe exposure, mjenge aendeleze haya mazuri yote unayoyafanya sana hasa katika kujenga uchumi imara kupitia sekta binafsi pale utakapomaliza uongozi wako. Mpe exposure apate kujifunza vizuri geopolitics. Na mwisho ikikupendeza chama chako kimpe kijiti akapeperushe bendera ya chama 2030.

Asanteni
Lord Denning
Kigali
Mkuu Lord denning , kwanza naunga mkono hoja Dr. Tulia awe mgombea wa urais wa CCM mwaka 2030.

Pili kwa vile Rais Samia alishauri 2025, twende na mgombea Mwanamke, japo wengi wanadhani Mwanamke huyo wa 2025 ni lazima awe Mama Samia, kwasababu ndio awamu yake ya pili, mimi pia Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!, hii maana yake 2025 Rais Samia is most likely but not necessarily ni lazima, yeye!, sio lazima, Mwanamke huyo, anaweza kuwa mwanamke mwingine yeyote, ila ukimuondoa Rais Samia as the No. 1 top lady in Tanzania, Dr. Tulia is the second!, hivyo 2025 anaweza kuwa ni Dr. Tulia!.

Kisha tembelea uzi huu, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke angalia nilichosema kumhusu Dr. Tulia na uchaguzi wa 2030
Na kipindi hicho cha 2025- 2030 ndipo sasa sasa tufanye grooming ya Mwanamke atakaye kuja kugombea urais wa JMT kwa 2030, na kwa maoni yangu, Mwanamke huyu sii mwingine yeyote zaidi ya Dr. Tulia Akson Mwansasu, Spika wa sasa wa Bunge la JMT.
Hivyo kwa hoja yako hii ya Dr. Tulia kuwa mgombea urais wa JMT kwa tiketi ya CCM mwaka 2030, tunafanana!.
P
 
huu mwezi jamaa wa chadema nikushindia panado tuh walahi kule makonda huku tulia hawajakaa sawa uchumi wa blue hua apa DP ndani ya nchi ya asali na maziwa
 
Imagine 2025 raisi Samia amchague Dr Tulia kuwa mgombea mwenza wa uraisi na baadae awe makamu wa raisi.

Alafu Makonda agombee ubunge na baadae apitishwe kuwa spika wa bunge.

I hope kuna watu watakufa kwa presha ya "wasiempenda kaja" 🤣🤣🤣
Kwa akili hizi, ndipo wazungu hutuona wafrika bado tuna undergo evolution!!
 
Imagine 2025 raisi Samia amchague Dr Tulia kuwa mgombea mwenza wa uraisi na baadae awe makamu wa raisi.

Alafu Makonda agombee ubunge na baadae apitishwe kuwa spika wa bunge.

I hope kuna watu watakufa kwa presha ya "wasiempenda kaja" 🤣🤣🤣
Aaahaaaa
 
Back
Top Bottom