Wafahamu wagombea wanaokwenda kushindana na Dr Tulia katika nafasi ya kuwania Urais wa IPU

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,740
Ndugu zangu Watanzania,

Katika kuelekea uchaguzi wa kumchagua Rais wa 31 wa umoja wa mabunge Duniani yaani IPU katika mkutano wa 147 utakaofanyika nchini Angola katika mji wa Luanda kuanzia Tarehe 23-27 mwezi huu, nimeona nikuletee wagombea watakaochuana na Mh Dr Tulia Acksoni mwansasu ,Nguli wa sheria ,mwalimu wa walimu wa sheria,Dada msomi ,Dada wa Taifa,Fahari ya nyanda za juu kusini na Nembo ya wana Mbeya, kiongozi shupavu,imara na madhubuti.

Katika uchaguzi huo wa kumrithi Rais anayemaliza muda wake mh Duarte Pacheco kutoka Ureno, wagombea wote ni wanawake kutoka bara la Afrika. Na hivyo kutoa nafasi kubwa sana kwa Dada yetu na speaker wetu mh Dkt Tulia kupita kirahisi sana,kutokana na Elimu yake kubwa,uzoefu wake kiuongozi, Ushawishi wa Tanzania kidiplomasia hasa wakati huu wa Rais samia ambaye Ameliheshimisha sana Taifa letu na kuliweka katika Ramani nzuri kidiplomasia pamoja na uungwaji mkono wa mataifa mengine kwa Dr Tulia.

Mgombea wa kwanza ni mh Catherine Gotani Hara,kutoka nchini Malawi. Huyu ni mbunge tokea mwaka 2009,lakini pia ni speaker wa kwanza mwanamke nchini Malawi nafasi aliyoipata na kuishikilia Tokea mwaka 2019, ni msomi wa shahada ya sayansi ya siasa na utawala wa umma yaani PSPA(political science and public administration) Japo amefanya mafunzo ya kozi zingine ndogo ndogo tu.

Mgombea mwingine ni Mh Marwa Abdibashir Hagi,kutoka Somalia. Huyu ni mbunge Tangia mwaka 2022 ,pia ni makamu mwenyekiti wa kamati ya Rasilimali,lakini pia amefanya kazi serikalini kwa muda mrefu. Amesomea Business Administration kutoka nchini Canada, pamoja na mafunzo ya ICT Japo siyo kwa kiwango cha shahada.

Wa mwisho ni Mh Adje Diarra kanoute kutoka Nchini Senegal. Huyu ni mbunge Tangia mwaka 2017, Amesomea masuala ya modern literature Lakini pia ana masters ya Business communication ,lakini pia amesomea masuala ya masoko yaani marketing.

Sasa ukiwaangalia hao wa gombea Elimu zao,uzoefu wao wa kibunge ,ndani ya serikali au hata katika mashirika unaona kabisa kuwa Dr Tulia anayeungwa mkono na jumuiya mbalimbali pamoja na nchi nyingine nyingi anakwenda kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima. Sijaweka CV ya Dr Tulia kwasababu ni ndefu sana iliyo Shiba ,nzito,safi,yenye kutulia, kuvutia na kutoa hamasa sana,hivyo yenyewe nitaiweka humu pekee yake muda mwingine ili kila mtu apate kuisoma vizuri.

Tuendelee kumuombea Dada yetu na speaker wetu katika mchako huu wa kumpata Rais mpya wa IPU yenye wanachama 179 na iliyoanzishwa mwaka 1889 na yenye makao makuu yake Geneva uswisi unaokwenda kufanyika mwezi huu.Tupige magoti kujinyenyekeza mbele za Mungu wetu ili amshindie vita hii Dr Tulia, kiongozi mwenye upendo na huruma kwa watu wote na mwenye moyo wa kusaidia watu wote Bila mipaka.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Tunamtakia kila la kheri, atuwakilishe vyema.
 
Mimi huwa silipwi chochote na yeyote kufanya kazi ya kuandika humu jukwaani Ndugu yangu.
Jitahidi kukithamini kipaji chako Cha uandishi. Hakikisha hufanyi kazi za bure. Ivi unajua kuwa vitu vya bure Huwa watu awavithamini kabisa that's why mtu anaweza akatupa mtoto ila uwezi kusikia mtu katupa nyumba...​
 
Vitu vizuri na bora ni vile vinavyofanywa kwa mioyo ya kujitolea yenye uzalendo isiyohitaji kulipwa au malipo .
 
Back
Top Bottom