yeriko na wengine wamelitaja jina la Mungu kwa usahihi katika siasa za Chadema. Mungu hajamkimbia mtu Kalenga.
kama unayo Biblia, au kama kuna jirani yako anayo, nakuomba--hapo nimetumia neno nakuomba--fungua Kitabu cha Biblia kinachoitwa Mhubiri kwenye eneo hili: MHUBIRI 3:1-16.
CHADEMA ni mpango wa Mungu kwa wakati alioupanga yeye Mungu. Sio mpango wa Mungu kwa wakati alioupanga Mingoi, Ifwero na Yeriko Nyerere. Na ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kila jambo linalotokea katika nchi yetu ni Mpango wa Mungu. Hata wizi wa kura ni mpango wa Mungu kulifikisha taifa kwenye maamuzi sahihi yaliyopo katika mpango wake huyo Mungu.
Yatafikiwa maamuzi sahihi katika taifa hili kama alivyopanga Mungu kwa kuwa kila jambo lina wakati wake. Soma kifungu hicho katika Biblia takatifu kujua kwanini CHADEMA ni mpango wa Mungu. Mungu ndiye anayechagua wakati sahihi kwa kila jambo! Kila linapotokea tofauti na fikra zako huo huwa tu ushahidi kuwa wakati wa Mungu kuruhusu jambo linalokusudiwa na roho ya Mwanadamu haujafika. Kila jambo lina wakati wake katika mpango wa Mungu.