- BOB, unakwenda mbaali sana ambako mimi sijafika, haya ni maoni yako ambayo ninayaheshimu sana, lakini na mimi nina ya kwangu regardless of what I hear kutoka kwa anybody, ninazo akili za kunitosha kuchuja ninachosikia kabla ya kukisema, ninaikubali analysis ya Slaa kwa 100% kwamba kama angeingia mapema kwenye uchaguzi uliopita, ageitesa sana CCM kuliko ilivyokuwa! Ya kumalizana mapema to me ni fear zaidi kuliko ukweli kwa sababu kama umeamua unataka urais, basi hakuna cha kuogopa, ndio maana ninashangaa sana kwamba mpaka leo hatujui officiallly nani wanataka kugombea urais ni kwa sababu wagombea wengi wana fear ya kujulikana uozo wao mapema, ndio maana hili taifa tumedumaa na fear kila kitu ni fear tu! Watu wanaona ukweli wanaogopa kusema kwa sababu ya fear ya kukosa this, fear ya kuonekana that, tujifunze kusema ukweli people! na timing is everything, saa ya kuambiana ukweli kuhusu uchaguzi wa 2015 ni sasa!
- Kuhusu maneno ya kupandikizwa ubaguzi, mimi kwanza siyaamini sana isipokuwa kwa kawaida kwenye siasa kuna mengi sana ya nyuma ya pazia ambayo sio rahisi kufahamika na wengi, for some reasons I know a lot huko behind the curtain ya Chadema na vyama vingine ambayo siwezi kuyaweka hapa! na hasa the reason behind Slaa kuingia dakika za mwishoni as opposed na what was said, So siasa ni mchezo mchafu lakini some of us tutaendelea kuzifuatilia kwa undani na kujaribu kuweka uwazi as much as we can, tunajua siku zote sio rahisi kupokelewa kwa urahisi, lakini somebody has to do it!
- Kuna wakati CCM, walidai kwamba maneno ya ufisadi ni ya kupandikizwa tu hayana substance, lakini matokeo uchaguzi uliopita ukawaumbua Mwalimu alikuwa anasema hivi: "Mficha maradhi, kilio kitamuumbua" so niliyosema kuhusu Viongozi wa kaskazini ambayo ina-cover sehemu kubwa sana kuliko unavyofikiri na kuamini, ni maneno yangu binafsi na nimeyasema seriously!
Willie @ NYC, USA.
Mkuu wangu labda hujanipata kabisa.. Naheshimu sana mawazo yako lakini nachokisema mimi ni kutokana na habari ulizosimuliwa ukaziamini, nikiwa na maana hayakutoka kichwani mwako bali unakubaliana na mawazo uliyolishwa..
Kama unaamini Dr.Slaa angewapa taabu CCM sijui kuna taabu gani zaidi ya ile alowapa tayari au una maana Chadema wangeshinda uchaguzi?.. kama ndivyo basi nakwambia isingewezekana kwa njia yeyote ile CCM kukubali matokeo yoyote dhidi yao - Hilo futa katika akili yako kwa sbaabu Dr.Slaa na Maalim Seif hamad wote walishinda uchaguzi na hawakupewa ushindi.. That is a fact!
Pili, Dr. Slaa hakufichwa na ndio maana nakwambia achana na havari za simulizi kwa sababu ilichukua muda kumrubuni Dr.Slaa kusimama kama mgombea wa chama. Na pengine hukupitia sana JF wakati wanachadema wakipiga mbiu na kukisisitiza chama kimsimamishe Dr.Slaa.
Na labda nikwambie tu kwamba Chadema ilifikia kukiuka utaratibu wa uchaguzi wa mgombea kwa kulazimisha Dr.Slaa agombee bila ushindani ndani ya chama kwa sababu ambazo wewe huwezi kuziona...Kwa hiyo Dr.Slaa hakuogopa kugombea isipokuwa aliombwa kugombea nafasi hiyo na uongozi wa chama.
Kitu kingine ujue pia kwamba ktk mashatri ya kampeni za kugombea dr.Slaa hakuchelewa balli jina lake lilitajwa kabla ya muda wa kampeni hviyo angekuwa kajificha tu kama kungekuwepo na uchaguzi ndani ya chama. Hivyo sioni mantiki yeyote ya kutaja jina la dr.Slaa ikiwa hairuhusiwi kuanza kampeni za kumtangaza zaidi ya kuwapa nafasi CCM kumbomoa..
Hadi majuzi tulikuwa hatujui ni kina nani wagombea wa Republican wakati umebakia mwaka mmoja tu wa uchaguzi halafu hata ikija tokea mshindi upande wa Republican itakuwa ni ktk wakati unaoruhusiwa kampeni za uchaguzi wa kiti cha Urais kuanza. Kwa hiyo huwezi kusema Republican wanaogopa kutaja mgombea leo kwa sababu wanafanya uchaguzi wa ndani kwanza, Laa! kinachotakiwa ni mgombea atangazwe kabla ya siku iliyowekwa na kabla ya kampeni kuanza..
Swala la Ukaskazini, mkuu wangu uongozi wa chama ni uongozi wa kiimani, sio swlaa la kuongoza nchi hata kidogo na nadhani viongozi wote wa sekretariet ya CCM hawapo ktk uongozi wa nchi sana sana labda wapo wawili..
Kwa hiyo, mfumo wa muundo wa chama hauwezi kuathiri utawala wa nchi hata kidogo kwani hakuna kati yetu anategemea Mnauye awe waziri au huyo Mukama hatuvutii kwa lolote zaidi ya kuzungumzia mazuri ya itikadi za chama chake.
Nitarudia kusema tena kwamba Chama ni kama kanisa, haijalishi kanisa hilo wanaingia sana wachagga au lina mkusanyiko wa mataifa mengi ali mradi kinachokupeleka kanisani ni imani ya Biblia na mafundisho yake. Padre awe mzungu au Mchagga haina maana kanisa ni la Wachagga, wewe unakaribishwa na ukiweza kuisoma dini na ukabobea ktk injili utaweza kushika wadhifa lakini sio tu upewe wadhifa kwa sababu wewe ni wa kabila jingine au rangi nyingine.
Na kesho ukimfukuza Padre kwa sababu ni Mchagga, basi utakuwa umejenga profiling ya Wachagga hivyo hao wachagga hawatakuwa na imani tena na kanisa ingawa wanaikubali dini.
Labda ungezunguzia haya kama Chadema ingekuwa haipokei wanachama wa makabila mengine lakini hawawezi watu kuvamia chama na kuanza kudai uongozi wakati hawajajengeka kiimani. Haya ndio yatakuwa ya kina Mukama na Nnauye ambao hawajui hata kukitangaza chama isipokuwa siasa za majitaka.
Believe me, leo hii ukiniuliza Mukama na huyo Nnauye wanasema nini kuhusiana na itikadi ya chama, dira na malengo ya chama mkuu wangu suwezi kujibu swala hilo kwa sababu sijawasikia wala sijui kama wanajua kazi kazi gani wamekabidhiwa kama si kujenga majungu na chuki...
Kwa hiyo kwetu sisi wanaChadema, hatubabaiki na Uchagga wala Ukaskazini kwa sababu tunaelewa mafundisho na msahafu wa chama unasema nini na tunachotaka ni hao viongozi wetu kuwakilisha msahafu huo. Haijalishi yeye ni Mchagga, Muislaam ama Mkaskazini kama nondo zinapanda weka ngoma, pandisha mizimu tunacheza wote kama Mdundiko ngoma ya Kizaramo!