Hongera CCM

Hongera CCM

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache WanaCHADEMA mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.

Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.

Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.

Pili napenda kutoa himizo kwa wanaCCM na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.

Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na CHADEMA tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua CHADEMA 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.

Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.

Tatu napenda kuwapa hongera na pole CHADEMA kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 CHADEMA kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.

Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama Watanzania kwamba kuna nini kati ya CHADEMA na Arusha? ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine CHADEMA ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.

CHADEMA ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaCCM, kubeza viongozi wa CCM walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.

Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa CHADEMA Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.

Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.

Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.

CCM umoja ni ushindi.

Viva CCM
 
Umeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.
 
Hivi wewe hiyo degree uliipataje? Hilo bandiko lako ni kama vile limetayarishwa na kijana aliyemaliza darasa la saba. Hebu tuwekee takwimu hapa zinazoonyesha kwamba katika uchaguzi wa 2010 CCM ilipata kura kidogo katika hizo kata nne lakini katika uchaguzi wa juzi imepata kura nyingi zaidi. Ukizungumzia uchaguzi kwa ujumla, nashangaa wewe unaishi dunia ya wapi ambaye hujui kwamba CCM ilipoteza viti katika baadhi ya kata kwa CHADEMA? Acha kutujazia server kwa post zisizokuwa na vichwa wala miguu.

Kuna kitu ningesema, lakini naogopa ban.

Tiba
 
Wewe ni mmoja wa watu waliokuwa arusha mkiipigia debe chadema kwa raslimali za CCM. Na kujishaua kote mkapigwa vituo vyote. Eti makapi ya CHADEMA ndio keki za CCM. Dada wa watu nakuhakikishia, mwaka huu hautakwisha bila ya nyinyi kutolewa kwenye reli. Eti hata mbuyu ulianza kama mchicha. CCM ilikuwa mbuyu wakati mwigulu anawasajili. Wewe na wenzako ndio mnaifanya iwe mchicha. Vipi lakini, sombetin Mwigulu ataenda?
 
Juliana Shonza umeandika mambo mengi sana... Lakini unaonekana huna kumbukumbu, kwamba kwenye uchaguzi huu mdogo wa nchi nzima CCM walipoteza kata nne kwa CHADEMA.
Pia huna kumbukumbu CCM walipata kura ngapi hapa Arusha.
Uchaguzi wa juzi ungetangazwa ingelikuwa aibu yenu.
Tena walioichagua CHADEMA walikuwa watu walioletwa na CCM kwenye vituo vya kupiga kura, wakidhani wangeichagua CCM!

Chezea CHADEMA weweeee!!!!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Katika mantiki ya kutafakari baada ya uchaguzi ana haki ya kuandika alichoandika. Ni jukumu letu sisi tumjibu ipasavyo.

Tatizo la CCM ni kulazimisha ushindi kwa lazima! Acheni wananchi wachague viongozi wanaridhika nao.
 
Binti Juliana, bado uko mdogo na mrembo kiasi fulani! Nakushauri ujipe likizo kidogo kwenye siasa ukafanye shughuli nyingine mpaka akili yao ipoe kwanza! Kama una nia kweli ya kufanya "siasa" kuwa "wito wako wa maisha", basi kina Nnape, Mwigulu & Co sio Model wazuri/sahihi kwako! Tafakari!
 
Umeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.

Excuse me!! sema 'ameandikiwa vizuri'...Juliana hana hata chembe ya brain cells za kutosha kuandika huo upuuzi anaodai kaandika hapo juu!
 
Naona baada ya kumalizia chenji ya fungu mlilotengewa na Mwigulu sasa umerudi tena, najua huna uchungu wowote na CCM kugaragazwa vibaya katika uchaguzi huu kwani inamaanika kwamba ulienda CCM kwa maslahi yako binafsi yaani mahusiano ya mazuri na Mwigulu Nchemba pamoja na kutafuta fursa za kuongeza kipato ambapo baadhi ya vijana wa UVCCM wakiwemo viongozi wa mkoa wa Singida walikaririwa wakisema umeziba njia za vijana waliokuwa waaminifu kwa CCM huku ukiwa na faida ndogo. Huna uchungu wowote na CCM, umekuwa ukiwapotosha vijana wa CCM kwa kuwapa matumaini yasiyokuwepo.Mfano, uliwaaminisha kwamba CCM ingeshinda kata zote 4 huko Arusha lakini baadae ukakimbia sambamba na Mwigulu Nchemba huku mkimwacha Katibu Mwenezi,Nape Nnauye akishindwa kuamini na kukosa cha kuongea. Huna uchungu na CCM kwakuwa wewe ni mchumia tumbo tu, wenye uchungu na CCM hawajipongezi Chama dola kushindwa kukomboa walipopoteza 2010.
 
Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.

Binti Juliana Shonza najua hii thread umeianzisha kwa maelekezo ya bosi wako. Pamoja na hayo na kwa faida ya vilaza wa hesabu wenzako hapo lumumba ngoja nikusaidie kufanya hesabu ya darasa la kwanza. Kwa akili yako ndogo unashindwa kujua kwamba kama ccm ilishinda kata 16 na Chadema imeshinda kata 8 basi jumla ya kata zilizofanya uchaguzi ni 24 (16+8=24!hesabu ya darasa la kwanza hii)sasa sijui kata 2 umezipeleka wapi!!??

Jumla ya kata zilizopaswa kufanya uchaguzi tarehe 16/06/2013 ni kata 26.
Kata zilizofanya uchaguzi tarehe hiyo 16/06 zilikuwa kata 22 (baada ya policcm kulipua bomu mkutano wa Chadema na hivyo NEC kuahirisha uchaguzi katika kata 4 za Arusha).
Katika kata 22 zilizofanya uchaguzi awali ccm ilishinda kata 16 na Chadema ikashinda kata 6 (Chadema ilirudisha mikononi kata zake 2 na kuchukua 4 kutoka kwenu ccm).
Katika uchaguzi uliofanyika Arusha juzi tarehe 14/07/2014 Chadema imewagaragaza vibaya ccm kwa kujinyakulia kata zote 4.

Kwa ujumla msimamo wa ushindi wa kata kwa ujumla ni kwamba Chadema 10 ccm 16. Lakini pia kwa uwiano wa wingi wa kura Chadema ina 46% huku ccm ikiwa na 49%. Sasa nataka uanzie hapo uniambie kama ccm imeongeza idadi ya wapiga kura toka 2010 au imeporomoka? sitarajii kwamba mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dsm unaweza kushindwa hata kuunga unga hesabu ndogo kama hizi, unless uniambie hiyo degree uliipata kwa mlango wa dharura.
 
Kama vyama vyote vikiheshimu sanduku la kura...tutaenda mbele sana.
 
Kabla ya matokeo kutanganzwa mkatoka NDUKI -- wewe na Kamanda wa Green Guards.sijui mlikimbilia wapi maana dar mmeonekana jana.
 
Unatoa hongera kwa CCM kwa achievement ipi haswa?

Nimejaribu kusoma bandiko lako naona umetoa tu highlights za namna uchaguzi ulivyokuwa, na sehemu nyingine kukandia CDM.
 
Hata wenzako wanakuzodoa.
Shonza umeleta kiwingu tu ndani ya CCM. Unaleta mkanganyiko kama umetumwa na CDM au ndo uwezo wako ni mdogo hivi? Ndo maana CDM walikutimua

Umeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.
 
Hivi wewe hiyo degree uliipataje? Hilo bandiko lako ni kama vile limetayarishwa na kijana aliyemaliza darasa la saba. Hebu tuwekee takwimu hapa zinazoonyesha kwamba katika uchaguzi wa 2010 CCM ilipata kura kidogo katika hizo kata nne lakini katika uchaguzi wa juzi imepata kura nyingi zaidi. Ukizungumzia uchaguzi kwa ujumla, nashangaa wewe unaishi dunia ya wapi ambaye hujui kwamba CCM ilipoteza viti katika baadhi ya kata kwa CDM? Acha kutujazia server kwa post zisizokuwa na vichwa wala miguu.

Kuna kitu ningesema, lakini naogopa ban.

Tiba

Mimi pia kutokana na ujengaji hoja wake napata wasiwasi na hiyo digrii. Lakini vilevile anapaswa kufahamu kuwa katika chaguzi zilizopita CCM ilipoteza kata kwa Chadema and thi is not a credit. Kata za Arusha zilikuwa za Chadema. Wao wameweza kurejesha kata zao zote tofauti na CCM wanaopoteza zao kila uchwao. Haihitaji digrii ya chuo kikuu kulitambua hili Shonza.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hata wenzako wanakuzodoa.
Shonza umeleta kiwingu tu ndani ya CCM. Unaleta mkanganyiko kama umetumwa na CDM au ndo uwezo wako ni mdogo hivi? Ndo maana CDM walikutimua

Unaposema hata wenzako wanakuzodoa unamaanisha nini? Hembu jipange kabla ya kuongea wewe.
 
Back
Top Bottom