Kaka Pekee
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 336
- 559
Bwana mdogo wangu Aslay, ni wazi kuwa unajitahidi sana kufanya kazi nzuri kimuziki na unashika nafasi mbalimbali za music chat hapa nchini.
Tungo zako na Matumizi ya sauti yako yanaonyesha ni jinsi gani unazidi kukomaa kmuziki ingawa inabidi ufanye mazoezi ya ziada way too far kwenye live performance sababu kwenye Valentine ulizingua kwa kweli ( Kutawala Jukwaa) ubunifu zaidi unahitajika.
Katika ziara yake hapa Mkoani Mbeya Mkurugenzi mkazi wa Usaid Bw. Andy Karas (Huyu ni boss wa USAID nchini- Mmarekani aliyeishi miaka mingi Afrika) nilimuuliza ni mwanamuziki yupi anayempenda nchini...Jibu lake likawa kwa Muziki wa Kale anampenda Remmy Ongala Sura mbaya, Marijani Rajab, na wengine wakongwe wa kale.....Kwa upande wa Muziki wa sasa hakuwa na list kubwa zaidi ya kutaja jina lako “ Muziki wa sasa ninamkubali Mwanamuziki anaitwa ASLAY” basi.
Sasa mdogo wangu Hiyo ni fursa sababu USAID wana miradi mingi ya kimaendeleo nchini. Kuna mradi wa Boresha Afya, Boresha Habari, Tusome Pamoja nk. Hebu fanya kama unatembelea Ubalozi wa marekani pale Msasani Dar es Salaam Uombe kuonana na huyu Mzee wa kimarekani, huenda ukapata zali la kuwa Balozi wa USAID kwa mradi mmoja wapo ukala shavu zaidi mdogo wangu.
Hiyo ni fursa mimekupa kwa kukung’ata sikio kidogo Kazi kwako.