Hong Kong yaendelea kuwa tulivu, imara na yenye neema miaka 25 baada ya kurudi China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111385197304.jpg
Ni miaka 25 sasa imepita tangu China irudishe mamlaka yake kwenye mkoa wa Hong Kong baada ya kuwa chini ya utawala wa Uingereza wa miaka 100. Ilikuwa ni Julai Mosi mwaka 1997, wakati wakosoaji walikuwa wakijenga picha mbaya kuhusu mustakbali wa Hong Kong, na kuitaja hatua hiyo kuwa ni mwanzo wa mwisho wa Hong Kong. Baadhi walifikia hatua ya kutabiri kuwa neema waliyokuwa nayo watu wa Hong Kong ingetoweka. Ni miaka 25 sasa, hali ya Hong Kong ikoje?

China kurudisha mamlaka yake kwenye mkoa wa Hong Kong ni jambo lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu na watu wa China, lakini pia ni jambo ambalo waingereza hawakulipenda hasa kwa kuwa walikuwa wananufaika sana kiuchumi baada ya kuutawala mkoa huo kwa zaidi ya miaka 100. Hata hivyo Uingereza ililazimika kukomesha utawala wake kwa kuwa makubaliano yaliyosainiwa mwaka 1898 kati ya Uingereza na China, yalitoa ruhusa kwa Uingereza kuvitumia visiwa hivyo kwa miaka 99.

Miaka michache kabla ya Hong Kong kurudishwa China kulikuwa na maswali mengi. Swali kubwa lilikuwa ni kuhusu mfumo gani utafuatwa na Hong Kong. Katika kipindi cha miaka 100 chini ya utawala wa Uingereza, Hong Kong ilikuwa inafuata mfumo wa kibepari lakini China ilikuwa inafuata mfumo wa kijamaa, na siasa za ndani zilikuwa ni siasa za kiliberali. Hali hii ilianza kuwatia hofu watu wa Hong Kong na hata nje ya Hong Kong kuhusu mustakbali wake kiuchumi na kisiasa baada ya kurudi kwa China. Hofu hii iliondolewa baada ya China kuweka sera ya “Nchi moja, mifumo miwili” yaani iliruhusu mfumo wa kibepari uendelee kufanya kazi China, na pia iliweka “sheria ya kimsingi” ambayo ni sawa katiba ya Hong Kong ambayo inasema Hong Kong iliyo chini ya mamlaka kuu ya China, itafuata utaratibu wake wa kisiasa na kuruhusu wakazi wa mkoa huo kuwa na uhuru mkubwa wa kujiamulia namna ya kuendesha mambo yanayohusu mkoa huo.

Tukiangalia matokeo ya utekelezaji wa mfumo huo katika kipindi cha miaka 25, ni wazi kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa. Takwimu zinaonesha kuwa pato la ndani (GDP) la Hong Kong la mwaka 1997 ilikuwa dola za Marekani bilioni 177, na pato la mtu mmoja moja (Per Capita Income) lilikuwa dola za Marekani elfu 24. Lakini katika kipindi chote hasa kuanzia mwaka 2003 baada ya serikali kuu ya China na mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong waliposaini makubaliano ya ushirikiano wa karibu wa kiuchumi (CEPA) pato la Hong Kong liliendelea kukua kwa mfululizo na kufikia dola za kimarekani bilioni 360, na pato la mtu mmoja mmoja limekuwa zaidi ya dola za kimarekani elfu 40, na kuna wakati hata lilifika dola za kimarekani elfu 46.

Kwa upande mmoja mafanikio haya yalithibitisha uzuri na manufaa ya sera ya “Nchi moja, mifumo miwili”, lakini kwa upande mwingine hayakuwafurahisha baadhi ya watu waliokuwa wanataka kuona sera hiyo inashindwa. Kutokana na kutofurahia hali hiyo, baadhi ya watu walianza kutumia mianya iliyopo kwenye “Sheria ya Msingi” ya Hong Kong na kuleta uchokozi wa kisiasa.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2014 kulikuwa na maandamano ya wanafunzi yaliyoitwa “Maandamano ya Miavuli”, na maandamano mengine ya mwaka 2019 yaliyoitwa maandamano ya rangi, yalijaa vitendo vingi vya kichochezi vyenye lengo la kukiuka “Sheria ya Msingi”, na hata kujaribu kufanya harakati ya kuitenga Hong Kong kutoka China. Vitendo hivyo vilikomeshwa baada ya sheria mpya ya usalama kupitishwa na kuanza kutekelezwa.

Wakati China inaadhimisha miaka 25 tangu irudishe mamlaka yake kwa Hong Kong, busara ya “Nchi moja, Mifumo miwili” imeonekana kuwa na mafanikio na kudumisha neema waliyokuwa nayo watu wa Hong Kong, na hata kuhimiza maendeleo na kufanya Hong Kong iwe na neema mara mbili kuliko ilivyokuwa chini ya utawala wa waingereza.
 
Kwanini wachina hampendi kuongelea siasa za nchi yenu mkiwa nchini kwenu!??,,juzi nilikuwa na mchina fulani Dodoma nikamuuliza kuhusu suala la Taiwan na mainland China nikamuuliza kuna sababu gani ya kutaka kutwaa eneo ambalo lilishajitangazia uhuru na wananchi wake wapo willing na suala hilo!? Aisee alipanick vibaya sana aksema kwa msisitizo nakwambia kwa sababu tu nipo Tz ila hili suala huwa haliojiwi ukiwa china hapo nikajua kumbe nyie mkiwa kwenu ni Kunguru tu kwa uoga wenu hata watanzania wana afadhali
 
Nchi ya jirani inaweza kukuangusha vibaya mno. Maadui zako huwa wanaanza na jirani zako ndio maana tunaona Russia inatumia gharama kubwa kujenga heshima. Leo hii unaona jinsi hata wakenya wanavyothujumu watanzania; inafikia sehemu hata wanazuia magari yetu yasipite nchini kwao. Njia rahisi ya kuwashinda ni kuwagawanya. .
 
Back
Top Bottom