Hon. Kagasheki hii ni bongo

Hon. Kagasheki hii ni bongo

Nduka Original

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
1,012
Reaction score
817
Moja ya mawaziri waadilifu katika Cabinet ya JK ni huyu mzee wa watu, anajitahidi sana kuweka transparency katika wizara yake ile namuonea huruma sana kwani wasaidizi wake ni wasanii wote.

Nimeshakaa na huyu Mh kwa kweli anakerwa na uozo wa taasisi zake kama NGORONGORO, WILDLIFE DIVISION, TANAPA ila inafika sehemu anakwama kutokana na support ndogo anayoipata. Mh kazi unayo kwani umezungukwa na wasanii watupu kuanzia msaidizi wako Nyalandu na ukija hao ma CEO wa taasisi zako nyeti ndio balaa kabisa. Unae bwana Kijazi wa TANAPA yani huyo ni balaa kabisa ni msanii, tapeli, mwongo etc, Ukija huyu bwana wa TTB Nzuki yule wala hajui anafanya nini pale kwani angalia tangu aingie TTB ni kitu gani amekwishakufanya sana sana mimi naona ana diary tu yenye list ya tradefairs nikimalizia ndugu yangu Kawasange yeye wala hajui yuko pale kufanya nini mana shrika limeshikwa na Vero ambaye ni manager wake wa utalii.

Na Mh usifikiri labda mkulu hajui huo usanii ni kwamba hii ndio Serikali yetu bwana hivyo mzee we nenda tu mdogo mdogo ukisubiri 2015.
 
Mkuu nakubaliana nawe kwa kila kitu, Wazara yake haitofautiani sana na Wizara ya Dr.Mwakyembe, kuna baadhi ya viongozi walio kaa muda mrefu bila ya kubadirishwa/kuhamishwa hivyo kujijengea himaya ya aina fulani vile wanashirikiana na wafanya kazi wa ngazi za chini ambao si waminifu, sasa kuweza kusafisha Wizara hiyo ni kazi sana na ukiongezea kwamba nafasi nyingine Rais ndiye anahusika katika utehuzi kwa hiyo Waziri hana mamlaka ya moja kwa moja ya kumwajibisha Kiongozi aliye teuliwa na Raisi kwa mfano.

Cha kufanya pale ni Rais kumpa mamlaka kamili Waziri kusafisha Wizara bila ya kujali kama kuna baadhi ya Viongozi waliteuliwa na Rais au la, nafasi zote nyeti zinatangazwe na Consultant kutoka nje ahusike vile vile katika kuwafanyia interview - watakao shinda ndio wapewe nafasi hata kama watakuwepo wale wa zamani, cha muhimu ni kufanyishwa interview na an Independet Consultant, Waziri akifanikisha hilo ataondokana na urasimu uliho kubuhu - Vile vile ambadirishe BOARD kama hajafanya hivyo - Ma board Members nao waombe na kuwa-veted na ma Consultants sio kutehua watu tu kwa kujuana. Mimi ndio ushauri wangu.
 
Angekuwa muadilifu angekataa suala la kuchukua ardhi ya wamaasai Loliondo na kusingizia uhifadhi wa mazingira.
 
Angekuwa muadilifu angekataa suala la kuchukua ardhi ya wamaasai Loliondo na kusingizia uhifadhi wa mazingira.

I am telling you the Loliondo SAGA is very controversial with too much politics, lile swala lina miaka zaidi ya 20 an he can never solve it. Na ndio maana nakuambia kuna vitu vingi ambavyo yeye Kagasheki havijui na anataka kuvitafutia ufumbuzi ikiwemo loliondo.
 
kwa suala la kuchukua ardhi ya wamaasai Loliondo na kusingizia uhifadhi wa mazingira.huyu bwana nimemchukia kuliko watu wote tukianza na zakia meghji
 
Mkuu nakubaliana nawe kwa kila kitu, Wazara yake haitofautiani sana na Wizara ya Dr.Mwakyembe, kuna baadhi ya viongozi walio kaa muda mrefu bila ya kubadirishwa/kuhamishwa hivyo kujijengea himaya ya aina fulani vile wanashirikiana na wafanya kazi wa ngazi za chini ambao si waminifu, sasa kuweza kusafisha Wizara hiyo ni kazi sana na ukiongezea kwamba nafasi nyingine Rais ndiye anahusika katika utehuzi kwa hiyo Waziri hana mamlaka ya moja kwa moja ya kumwajibisha Kiongozi aliye teuliwa na Raisi kwa mfano.

Cha kufanya pale ni Rais kumpa mamlaka kamili Waziri kusafisha Wizara bila ya kujali kama kuna baadhi ya Viongozi waliteuliwa na Rais au la, nafasi zote nyeti zinatangazwe na Consultant kutoka nje ahusike vile vile katika kuwafanyia interview - watakao shinda ndio wapewe nafasi hata kama watakuwepo wale wa zamani, cha muhimu ni kufanyishwa interview na an Independet Consultant, Waziri akifanikisha hilo ataondokana na urasimu uliho kubuhu - Vile vile ambadirishe BOARD kama hajafanya hivyo - Ma board Members nao waombe na kuwa-veted na ma Consultants sio kutehua watu tu kwa kujuana. Mimi ndio ushauri wangu.

Shida ya mfumo wetu waziri hana autonomy ya ku act
 
Angekuwa muadilifu angekataa suala la kuchukua ardhi ya wamaasai Loliondo na kusingizia uhifadhi wa mazingira.

Kwa hiyo kuhifadhi mazingira hakuna umuhimu wowote kwa ustawi wa binadamu, yaani Watu wa magharibi/Ulaya wanafikia hatua ya kutoa motisha wa watu wanaoishi kwenye equatorial belt na Savannah waifadhi miti - sisi tunaona hawajui lolote including Waziri anaye tetea uhifadhi wa mazingira!! Sisi wabantu ni binadamu wa aina gani lakini?
 
Angekuwa muadilifu angekataa suala la kuchukua ardhi ya wamaasai Loliondo na kusingizia uhifadhi wa mazingira.

Angeanzia wapi kukataa? Chezea tz wewe? Naye anapenda wanae waende haja! Tanzania ya sasa inatekeleza sera ya IF YOU CAN NOT FIGHT THEM..........
 
Huyo Nyalandu si katokea USA na alisema ana uwezo mkubwa?kumbe naye njaa kihivyo?
 
Nadhan kila waziri na baadhi ya wanasiasa kama sio wao basi lazima wawe na ID humu. JF kweli imekuwa source ya habari kuliko hata media nyingine kwa sasa.

asa hapa nadhan hii 3d ni mpango although maelezo yanaweza kuwa sawa. Hongeren JF Founders.
 
Shida ya mfumo wetu waziri hana autonomy ya ku act

Hili ndilo tatizo kubwa linalo kabiri Taifa letu kwa kuongeza urasimu husiyo na maana yoyote, kuna baadhi ya viongozi kule tu kutehuliwa na Rais basi nakuwa ndio nongwa umwambii chochote, wanaishia kukuta baadhi ya Mawaziri kutoelewana na makatibu wakuu wake - mimi binafsi niliwahi kushuhudia Katibu mkuu anapuuzia mahagizo ya Waziri wake anayakalia tu bila ya kuyafanyia kazi na hajali chochote!! Sasa hii inaleta picha gani kuhusu ngazi za Uongozi - ni janga tupu.

Kuna umuhimu wa JK kujikakamua na ku-reverse trend hii ya mambo, yaani kazi yake ibaki kutehua Waziri mkuu tu basi, mawaziri (wasiwe Wabunge) wateuliwe na Waziri mkuu na kuthibitishwa na Bunge kama wabunge wana wasi wasi na utehuzi wa Mawaziri fulani basi wasikubaliwe - hii itampa mamlaka Waziri mkuu kuwashughulikia Mawaziri bila ya kuwa na woga, makatibu wakuu wateuliwe na Mawaziri wakishirikiana na Waziri mkuu nao vile vile utehuzi wao uthibitishwe na Wabunge, wakifanya hivyo uwajibikaji utaongezeka marudufu na majungu yatapungua SANA.
 
Kwa hiyo kuhifadhi mazingira hakuna umuhimu wowote kwa ustawi wa binadamu, yaani Watu wa magharibi/Ulaya wanafikia hatua ya kutoa motisha wa watu wanaoishi kwenye equatorial belt na Savannah waifadhi miti - sisi tunaona hawajui lolote including Waziri anaye tetea uhifadhi wa mazingira!! Sisi wabantu ni binadamu wa aina gani lakini?

Kaka umejibu vizuri ila kumbuka wanaotetewa sio Wabantu ila ni wa Tanzania. Maasai sio wabantu tukirudi katika Historia ndo maana jamaa anawa equate na vitu vingine
 
...trend ya matatizo TZ ambayo ni systemic Jk hawezi kui reverse..na ndio sababu tunaona baadhi ya mawaziri hata wawe effective namna gani...bado wanashindwa kutafta ufumbuzi wa matatizo kwenye wizara zao...Sasa hivi nguvu ni kupeleka kwenye katiba tu....Kwanza hii kizazi ya viongozi wachovu lazima iondoke kwanza.....yaani nchi ianze upya na mifumo mipya ya uongozi na jinsi ya kuwapata viongozi...bila hivyo kwa hali iloyopo tz hata kubadili viongozi sasa naona wala haisaidii....maana wote (almost)wameozeshwa na system...We need to start afraish as a country....with a new constitution in place.....no other way out...
 
Kaka umejibu vizuri ila kumbuka wanaotetewa sio Wabantu ila ni wa Tanzania. Maasai sio wabantu tukirudi katika Historia ndo maana jamaa anawa equate na vitu vingine

Mkulu labda nilipaswa kusema black people badala ya Wabantu,Nilotic, Pygmy, Bushmen nk; mkuu hajalishi unatoka taifa gani Africa mambo yetu ndio hivi hivi.
 
Kagasheki hana lolote

Hakuna waziri anayefanya kazi kama Kagasheki, Magufuli na Mwakyembe. Huyu mzee hapumziki, ukikutana naye amechoka utamuonea huruma. anajituma, hana majivuno na hana makuu. Ubovu ni wale wazembe wachumia tumbo waliomzunguka. Kuanzania TTB na TANPA yote uozo. Inabidi apangue safu nzima awafukuze hao wazembe. Pale wizarani ndo wote wanawaza posho na kuiba kutumia dili. Chonde chonde Mheshimiwa wewe ndo jembe
 
Waziri Kagasheki ni mfano wa kuigwa. Swala la Loliondo siyo swala lake. Kapewa mbuzi ndani ya gunia hana la kufanya. Mzee mchapakazi sana. Amepewa Wizara ngumu iliyooza.

Nadhani nyinyi mumezoea mawaziri vilaza kama Mulugo na mwenzie Kawambwa. Kagasheki anytime. Jamaa ana class na hana longo longo. Hongera mheshimiwa


Angekuwa muadilifu angekataa suala la kuchukua ardhi ya wamaasai Loliondo na kusingizia uhifadhi wa mazingira.
 
Back
Top Bottom