Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 10,059
- 13,484
no gentleman,Hata mimi nakubaliana kabisa ni majadiliano ya kiungwana. Nisichokubaliana nacho ni ' exploitation ya sehemu ya jamii yetu' ili kutengeneza mazingira fulani. Ukisoma hiyo article kama si msomaji utakubaliana nayo 100%.
Ukiwa na weledi itakupa ghadhabu kwasababu kinachofanyika ni 'exploitation' tu
Ninafuatilia lakini pia siwezi kuendelea kuinajisi akili yangu kwa kuamini kuna 'Federation ya nchi mbili, Tanzania na Zanzibar''. Hapana aisee! Huu upotoshaji wa Tanzania ni nchi tofauti kabisa na Zanzibar ni wa ki-CCM.
Well kama ni utimbakwiri let it be, ninachosema hapa ni kwamba sikubaliani na upotoshaji.
Nafahamu watu wengi wanachanganyikiwa hivyo ni muhimu wale wanaoelewa wasikae kimya
Huu muungano unaosema kwamba ni 'adhimu na adimu' bila kujua maana yake unachanganya.
Tunawezaje kusema ni Raia wa nchi moja wakati Raia wa Tanganyika hawana haki Zanzibar.
usiwanyime publics mawazo na maoni ya yako ya maana na muhimu juu ya jambo hili, ambayo inaashiria kabisa dhahiri shahiri unayo. usiwe mchoyo au mbinafsi sana kwenye vitu vya maana, vizito na muhimu hivi bana.....
ni kwasabb ya uelewa na ufahamu usio wa kutosha, juu ya jambo hili la muungano, ndio maana, tupo hapa tulipofikia hususani kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.
jambo hili linaelezwa na kujadiliwa nusu nusu, tena kwa ukali usio na sababu, bila kueleza au kujadili mpaka mwisho, ili kusudi waTanzania waelewe nyeusi na nyeupe bayana.....
sasa hii shule na darasa la kupanic na kusema sitaki tena majadiliaona wakati nafasi na jukwaa ndio hili, sio jambo lenye afya kwa academicians na visionary professionals who are aiming at transforming a certain agenda into other form or established formation 🐒
ni uchoyo na ni ubinafsi wa kuwanyima waTz uelewa na ufahamu zaidi kwenye suala hili la muungano.
Natoa wito wa majadiliano kuendelea licha ya setbacks, dhihaka na vitimbi miongoni mwetu na kwa baadhi ya wachangiaji. Hivyo vitu hochee kujadiliana zaidi.
Tusuonge kwa pamoja kwa upendo, mpaka mwisho kwenye hili safari hii, huku amani miongoni mwetu ndio ikawe hitimisho la majadiliano na hoja yenyewe 🐒