HOJA ya Zitto yawasilishwa kwa spika

Zito akaze buti lazima kieleweke mawaziri wa jk, wanatuzingua sana hawa. na baadae wapite kwa wananchi kuwaelimisha juu ya sakata hilo.
 
"@zittokabwe: Taarifa ya Maandishi ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu (ibara 53A ya Katiba) imewasilishwa rasmi kwa Spika."

"@zittokabwe: Mchana Leo HOJA ya kutaka Azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itakabidhiwa kwa Spika (kanuni 133(2)(3)). 'Taarifa vs Hoja'"

Zitto angalia na maisha yako wasije waka kumwakwembe, "ujasili ni chanzo cha mafanikio"
 
Tunahita viongozi wenye kuthubutu kama Mh. Zitto bravo kwa wabunge wote waliotia sain. Aluta continua mapambano ndo yameanza jamani
 
Zitto,ni sawa na magamba 100,tena siyo km Lusinde,.labda wenye uwezo km yule **** wa bumbuli sijui anaitwa nani?kama kuna anayekumbuka jina anikumbushe.
 
Anaweza kutumia kanuni ya kiti kupinga hoja huyo ndo bi kiroboto
 
Aliondoka Lowasa, Karamagi, Msabaha. Tukadhani nafuu itapatikana. Hakuna lolote. Mambo ni mabaya zaidi! Tunataka Pinda aondoke au mawziri wengine wanane. Kuna nafuu yoyote itapatikana? Hivi kweli hatujui tatizo hasa ni nani au ni nini? Tuendelee kuzugana tu na kujizolea umaarufu usio na tija!

Tatizo la binadamu ni USAHAULIFU, mara baada ya kutoka Lowasa na wenzake utulivu na adabu vilikuwepo serikalini lakn baada ya miaka 4 naona wabunge wameshasahau kwa sababu wengi wao kipindi hicho walikua wabunge wa kawaida. Tabia ya kuwajibishana ikiendelea mawaziri watakua na akili ya uwajibikaji, lakini kuna umuhimu pia wa kumujibisha RAIS katika siku zijazo manake nae amekua kama chanzo cha haya yanayotokea kutokana na kuwavumilia na kuyafumbia macho maovu yao.
 
Kila jambo na wakati wake,nadhani umefika na nguo zinaanza kudondoka hatimaye huenda Serikali ikabaki uch*********.
 
Zitto safi sana sisi wananchi wa kawaida wapenda mageuzi tuna nyuma yenu
Misemo ya kizamani kwa watu wa Kisasa! Wapenda Mageuzi kamwe hawatakiwi kuwa nyuma ya mtu yeyote bali wawe naye sambamba ktk kuleta Mageuzi. Ukiwa nyuma ya mtu maana yake mtu huyo akijikwaa au maadui wakimmaliza na nyie wote mmekwisha, sawa sawa kabisa na msafara wa nyumbu ambapo yule aliyetangulia akianguka nyumbu wote wanafuatia huangukia pale pale alipoangukia aliyekuwa amewatangulia! Misemo kama hii inahitaji kurekebishwa iendane na wakati na hali halisi ya sasa.
 
ZITO KABWE,tupo nyuma yako kukusapoti uciogope vitisho au ucikubali ahadi ya pesa,madaraka na ujanjajanja,komaa kamanda,kwa sasa magamba yamewafika kwenye makalio.MUNGU akulinde na kukutia nguvu.
 
Back
Top Bottom