HOJA ya Zitto yawasilishwa kwa spika

HOJA ya Zitto yawasilishwa kwa spika

"@zittokabwe: Taarifa ya Maandishi ya kutaka kuleta hoja ya
kutokuwa na imani na Waziri Mkuu (ibara 53A ya Katiba) imewasilishwa rasmi kwa Spika."

"@zittokabwe: Mchana Leo HOJA ya kutaka Azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itakabidhiwa kwa Spika (kanuni 133(2)(3)). 'Taarifa vs Hoja'"


Mkuu sijui kwa nini PM haoni kuwa kuti alilokalia ni kavu.....!!! kwani amekuwa akiandamwa sana na misukosuko ya KUANDALIWA kwa kutumia udhaifu wa mambo yanayojitokeza ndani ya Serikali ya JK ili EL arudi kwenye nafasi yake ya uPM........Pia waTZ nao wamekuwa Bendera fuata upepo hawatafakari yanayojitokeza ni kwa maslahi ya nani?.......URAFIKI, URAFIKI utatumaliza...........Pinda najua magumu yanayokukuta lakini usijali ni mapito tu hayo......Wa TZ nao
Wanafurahia hili hawaangalii ni kwa faida ya nani? ni nani anaratibu hili na kwa maslahi ya nani? ni kweli sishabikii udhalimu na ufisadi na kutokuwajibika Lakini nguvu inapotoka Nchi nyingine Aaaaaaaaaaaaaaaaaah tumekwisha......si sawa hata kidogo naongea kwa uchungu......URANIUM. maliasili zetu.....Kuna msemo usemao MBEGA ALIPONZWA KWA UZURI WAKE.....
Hakuna wakati mbaya kwa Binadamu kimaamuzi na wenye kutafakari zaidi basi ni wakati anapokuwa na MSONGO WA MAWAZO NA FURAHA YA MOYONI......Natafuta Nchi ya kukimbilia nikawe Mkimbizi......


POLE PM........

MY WORD IS MY BOND.
 
Hapa ishu ishazimwa,Bi kiroboto ashafanya mambo yake..atajifanya amesahau au atavuruga time table
 
Hakika Serikali ya JK haibebeki kabisa , leo Kamati ya Ardhi Maliasili na Mazingira ya Bunge kwa mara nyingine imemlipua waziri maige na watumishi wa Wizara ya Mali asili na utalii kwa kashfa kubwa ya kugawanya vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa rushwa na pia utoroshaji wa wanyama pori kwenda Nje.
 
Kansa no 1 Tanzania ni huyu SPIKA WA BUNGE, kama si yeye ungekuta kikwete si rais, pinda si waziri Mkuu, wala hao mawaziri wanaotuhumiwa wasingekuwepo madarakani.
 
Tatizo ni bi Kiroboto, inabidi TUNDU LISSU atangulie kuichambua sheria ya kumbana Spika kabla ZITTO KABWE hajatoa hoja. HAWA WAPAMBANAJI 2 WAKISHIRIKIANA KWA KILA HATUA bi kiroboto atakuwa kwenye wakati mgumu sana mana hajui sheria

Spika atatumia rungu lake kwa mujibu wa kanuni za bunge kwa kuitupilia mbali hoja ya Zitto.

akileta ubishi atasimamishwa vikao vya bunge kwa muda mrefu hadi mwezi wa tisa hivyo atakosa bunge lote lijalo na huo utakuwa mwisho wa hoja hiyo.
 
Hongera sana zitto, wale wabunge ambao hawakusaini kama akina january na wengineo, wape pole waambie wananchi hatudanganyiki! Mungu ibariki TANzania, walaani mafisadi na wale wabunge ambao hawakusaini!
 
Aliondoka Lowasa, Karamagi, Msabaha. Tukadhani nafuu itapatikana. Hakuna lolote. Mambo ni mabaya zaidi! Tunataka Pinda aondoke au mawziri wengine wanane. Kuna nafuu yoyote itapatikana? Hivi kweli hatujui tatizo hasa ni nani au ni nini? Tuendelee kuzugana tu na kujizolea umaarufu usio na tija!
 
Kansa no 1 Tanzania ni huyu SPIKA WA BUNGE, kama si yeye ungekuta kikwete si rais, pinda si waziri Mkuu, wala hao mawaziri wanaotuhumiwa wasingekuwepo madarakani.

mchumbie utusaidie kumthibiti kwa kutumia faragha.
 
Wera wera zitto.But kuna mbunge wangu mpya na anasapoti mafisadi hajasaini naye ni Augostino manyanda masele jimbo la mbogwe wilaya ya mbogwe mkoani geita mpya.Na nilazima akalie kuti kavu 2015 harudi mjengoni badala yake naingia mim via pipoz pawa.

Bila shaka atakuwa mi wa ccm huyo
 
Hongera sana zitto, wale wabunge ambao hawakusaini kama akina january na wengineo, wape pole waambie wananchi hatudanganyiki! Mungu ibariki TANzania, walaani mafisadi na wale wabunge ambao hawakusaini!

Tushukuru kuwapata hao 73 ambao hawakusaini ni haki yao ya kikatiba tukilazimisha sana tutakuwa tunavunja haki yao kikatiba.

Demokrasia ni suala pana sana inauma na kupuliza
 
[h=1]HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA LEO[/h]
· Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
· Ni mwendelezo wa ‘operesheni uwajibikaji’
Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

“taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge leo tarehe 23/04/2012 nitawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘operesheni uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge na watanzania wote waiunge mkono ili kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu;

…………………………….

Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.

22/04/2012.
 
Spika atatumia rungu lake kwa mujibu wa kanuni za bunge kwa kuitupilia mbali hoja ya Zitto. akileta ubishi atasimamishwa vikao vya bunge kwa muda mrefu hadi mwezi wa tisa hivyo atakosa bunge lote lijalo na huo utakuwa mwisho wa hoja hiyo.
nani aliyemtuma akatumie marungu bungeni? Kwa mujibu wa sheria Zitto yuko sahihi, huyu mama hajui sheria yoyote na hana uwezo wa kumtoa zitto bungeni hata ye mwenyewe anajijua kuwa ni kila.za.
 
Mapindunduzi ya Tz yanaletwa na waTz wenyewe heko Zitto kwani hata wakija na vifungu vya kifisadi haki na kweli utasimama kifua mbele siku zote kwani tutaanza na Mungu kuikomboa Tz na tutamaliza na Mungu
 
Aliondoka Lowasa, Karamagi, Msabaha. Tukadhani nafuu itapatikana. Hakuna lolote. Mambo ni mabaya zaidi! Tunataka Pinda aondoke au mawziri wengine wanane. Kuna nafuu yoyote itapatikana? Hivi kweli hatujui tatizo hasa ni nani au ni nini? Tuendelee kuzugana tu na kujizolea umaarufu usio na tija!

ukitaka kubomoa jumba bovu ongeza nyufa za kutosha,litaanguk lenyewe taratiiibu na kufika 2015 ni skrepa tupu.
 
Tushukuru kuwapata hao 73 ambao hawakusaini ni haki yao ya kikatiba tukilazimisha sana tutakuwa tunavunja haki yao kikatiba. Demokrasia ni suala pana sana inauma na kupuliza
haki ya kikatiba ni kuiba na kutetea majizi? Tafakari kabla hujaandika chochote vinginevyo utaonekana limbukeni.
 
Back
Top Bottom