Mzee Mwanakijiji umeliweka vizuri sana hili suala na hicho wanachoibuka nacho akina Ghibuu na Nurdin ni kulialia tu bila hoja ya msingi. Kwa upande mwingine wazenji hawa wawili wamenipa somo moja muhimu sana kupitia maandishi yao; wanasema ZNZ inakosa misaada mingi kutoka jumuiya ya kimataifa kwavile hubanwa na kuwepo kwake ndani ya muungano. Kwamba mara kadhaa wakiomba misaada hujibiwa kuwa Membe kishachukua kwa niaba ya muungano. Hitimisho ni kuwa msingi mkuu wa ZNZ kutaka "kujitoa" kwenye muungano ni kupata fursa nzuri na ya wazi ya kupata misaada kutoka mataifa tajiri taasisi za misaada za kimataifa. Lengo kama ni hilo naionea huruma ZNZ na nisifiche mtazamo wangu kuwa wanachopigania wanaharakati hawa wakizenji ni sawa na kulenga shabaha gizani kwa bunduki ya rasharasha kwani hutapata shabaha hiyo na balaa kubwa zaidi risasi hizo zaweza hata kuwapata wazazi na ndugu zako.
Historia ya ulimwengu inaonyesha harakati zote za kujikomboa kama wanavyodai wanaharakati hawa wakizenji lengo kuu ni kupata uhuru ili kutumia fursa hiyo kujiendeleza kwa kupanga mipango ya maendeleo kwa vipaumbele vya haki na vyenye manufaa kwa wananchi wengi wa jamii husika, lakinin hili la ZNZ limeniacha hoi kwamba watoke kwenye muungano ili wawe OMBA OMBA wazuri kimataifa. Shame on you!
Pili kisingizio cha kuwa sheria ya kukusanya maoni ya katiba inawabana na kuwazuia kujitoa kwenye muungano ni uongo wa mchana. Ninachojua wazenji wanauhitaji sana muungano kuliko wabara wanavyouhitaji isipokuwa kuna matapeli wachache kama akina Ahmed Rajabu, Ismail Jussa etc ndiyo ambao wanawaingiza mkenge na hoja muflisi ya muungano wa mkataba. Ukiamua kutoka toka, muungano wa mkataba wa nini tena? Watu kama akina Ghibuu na Nurdin wamedandia gari kwa mbele bila kujua liendako.
Nasisitiza ZNZ inatingisha tu kiberiti lakini inauhitaji sana muungano, ZNZ ina baraza la wawakilishi ni lini iliwahifikishwa huko hoja ya kujitoa katika muungano, mbona kuna mengi tu yamewahifikishwa huko ikiwemo kura ya maoni na mpaka kuundwa kwa SUK vipi hili la muungano liwashinde. Kwani kuundwa SUK mliomba ruhusa kwa Mhe Kikwete?