Hoja ya "Muungano wa Mkataba" ni Muflisi!

Aman karume alikuwa na nia njema ndio mana ilikubali kuunda umoja wa wazanzibari, GNU,lakini kwa sasa shein hawezi kufanya kama hivyo munavyotaka nyinyi,unless akubali rais shein kuvunja matakwa ya dodoma ili kuipa zanzibar uhuru wake wa dec 10.
 
Kama watanganyika humjawahi kuona muungano wa mkataba ukoje basi na huu wa nyerere haukuwahi kuwepo duniani.
 
Unaishi sayari ipi ndugu yangu?mkataba ni maoni ya waz'br kwenye ile tume,na nyie pelekeni yenu kwenye ile tume tupate kuwaelewa mkitakacho.

Watu wa bara hawajawahi kulalamika kuwa Zanzibar inawaonea; ni Wazanzibari ambao wamekuwa wakitishia kutoka lakini kutoka hawataki. Hapa mmoja anasema ati tuwafungulie na milango; mwisho mtasema tuje na kuwabebea mizigo yenu. Kama kweli mnataka Zanzibar huru ichukueni tu yote imo mikononi mwenu.
 
Haya mawazo yako ya kijinga hayana mashiko yoyote kwa samaki, wewe huwezi kujua zanzibar inaisaidia vipi tanganyika,
Ndio maana samaki hana ujanja...si tu anavuliwa, anageuzwa kitoweo! Zanzibar kuisaidia Tanganyika? Tanganyika ipi? Ama hizo ndio akili za samaki! GHIBUU, JF inakuzidi uwezo...please go back where you came from! Naona idadi ya watu mliozoea mijadala miepesi kwenye kumbi zisizo makini mnazidi kuongezeka siku hadi siku, silaha pekee mliyo nayo ikiwa ni gunia la matusi mnapokosa hoja.
mambo haya mtu wa kawaida kama wewe huwezi kujua, samaki ukimuuliza atakuwambia.
Bahati mbaya ndani ya JF tunajadiliana tu na watu wa kawaida, si samaki! Kwa ufahamisho tu ni kwamba samaki kuambiwa hawezi kukwea mti hatukanwi, ndio maumbile yake!
Kuna mambo haya ambayo tanganyika hufaidika kwa muavuli wa muungano. kwanza kimataifa, utambue jambo lolote ambalo la muungano au silo la muungano, akiindia rais wa united repulic of tanzania ujue linawakilishwa kimuungano, zanzibar huambulia patupu, kama kuna furushi la bilioni dola 200 zitatolewa huko UN basi munafaidika nyie zanzibar huambulia patupu.
Ehee, endelea @NGIBUU...
zanzibar ikienda njee kuomba msaada wakifika tu huko, huwambiwa ah membe kafika hapa kashaondoka na furushi, kwani hamujapatiwa chenu huko zanzibar ? nyie si muna serikali ya muungano ? Ah hatujapata kitu, jibu mutajuana wenyewe.
Hii sidhani kama ni kweli hata kidogo...yaani Zanzibar iombe msaada kama Zanzibar, furushi apewe Membe? Kama hata Mag3 anaweza kuomba msaada akapewa, huyo mtu mwingine wa kupewa furushi anaingiaje hapo? Au unaongelea msaada unaotolewa kwa nchi? Kumbuka huko nje tunayo nchi moja tu, Jamhuri ya Tanzania, period.
Climate change Imetoa furushi kwa maneo ambayo yamezungukwa na bahari kwa mfano mafia, zanzibar, comoros, na sehemu nyengine, ambazo huwathirika na tabia nchi, maji kupanda juu na mengine , mfuko huu hutolewa na jumuiya ya mataifa, tanzania hupata dongo nono sana ,bahati mbaya zanzibar huambulia patupu,tukienda kuomba msaada huo tunaambiwa tushapewa,tukiulizia huko tanganyika jamani tupeni chetu, ah hichi chetu tumepewa sie dai chenu, haya ndio matunda ya muungano ,wewe mwanakijiji unajidai hufaidikia basi muulize membe waziri wako atakuwambia.
Mbona unajichanganya? Hili dai lako ni uwongo uliopitiliza. Mara unadai Tanzania kupewa donge nono, hapo hapo unalalamika Zanzibar kuambulia patupu! Nilidhani Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na hiyo Tanganyika unayoionglea unaijua wewe tu, huko nje hawaijui.
Kuna mengi sana ambayo munafaidika na muungano,lakini hayo ni machachetu mpumavu kama wewe ambae hukusoma au sijui ukaidi tu huelewi ,hutaki ukweli, nafikiri ungelisoma masuala ya uchumi, ungelielewa zaidi na vipi munafaidika katika muungano huu. zanzibar imeanguka kiuchumi kutokana inashindwa kujiamulia mambo yake wenyewe hasa pale inapotaka kufanya ushirikiana na nchi nyengine katika nyanja za kiuchumi, haiwezi bila ya kuomba kibali kwa membe, na hilo ndio kikwazo.
Kama wewe ni mfano wa mtu aliyesoma basi kazi ipo. Hata hivyo, mbona Mwanakijiji kawasaidia kwa kuwaonesha njia bora iwapo Zanzibar inaona inaonewa, nayo ni kujitoa na kuwa nchi huru. Katoa mifano ya nchi kadhaa ambako kura za maoni zimepigwa na wananchi wakaamua kujitoa ama kutojitoa kwenye muungano. Kipi kinakushindeni kuelewa hapo? Ama kama samaki na wewe unasononeka kwamba kushindwa kwako kukwea mti ni dalili ya kukosa akili! Hapana, ni maumbile tu!
zanzibar ilitaka kujiunga na OIC kwa vile zanzibar ina asilimia 99 waislamu, muungano umewazuiya hilo suala kwa nini ? Munajenga hoja za siasa chafu na kibaguzi eti waislamu sijui magaidi, sijui usultan tunataka kuleta , yaani upumbavu mtupu,,, kwa nini munatuingilia katika maamuzi yetu ?
Sheria za OIC ndizo zilizowazuia kujiunga kwa sababu Zanzibar haitambuliki kimataifa kama nchi kipengele ambacho kwa akili za samaki, mlishindwa kukizingatia. Mlitaka kuingia kama vile mnaingia msalani...mswahili bwana! Mlidanganya na uwongo ulipogundulika kuwa Zanzibar haina sifa mliambiwa sheria hairuhusu na kwamba ni nchi Tanzania tu ingeweza kujiunga na si vinginevyo.
Hatutaki tena, tunataka zanzibar yetu.
Hapa sasa unaongea, tupo ukurasa moja na sisi tunawatakia kila la heri ila isije ikawa huku wataka na kule wataka
yahe! Hiyo tabia wanayo waoga, wanafiki na walafi. Kinachowazuieni si serikali ya Muungano, ni serikali yenu kwa kuogopa Zanzibar kumeguka vipande vipande nje ya Muungano.
Na kumalizia jiulize kwa nini tunataka muungano wa mkataba ? wakati huo huo tunadai zanzibar huru? Suali zuri sana, na nitakujibu. Ukweli ni kwamba sheria ambayo inatupa uhuru wa kujadili muungano, ni sheria ambayo inatupa kuuboresha tu na sio kuvunja, na hilo ndilo suala ambalo wazanzibari limetugusa katika katiba mpya, muungano tu na sio chengine katiba yetu tunayo.
Huu ni uwongo, uwongo, uwongo...ni kutafuta tu visababu vya kung'ang'ania kubaki ndani ya Muungano mnaodai hamuutaki kumbe kuna lililojificha, mnaiogopa Zanzibar nje ya Muungano! Hiyo sababu haikuizuia Sudani Kusini isianze mchakato wa kujitenga...kwa kweli wengine wenu ni wanafiki wakubwa. Mnataka mpikiwe, muwekewe mezani, mlishwe na na ikiwezekana mtafuniwe! Hapana, acheni uvivu na woga, mtaka cha uvunguni sharti ainame!
kama ulitaka tutoe maoni ya kudai zanzibar huru tu, na tuukatae muungano kabisa tukutae eac basi mwambie rais wako kikwete aabadilishe kifungu chake katika hadidu rejea kuwa kila raia ana haki ya kuhoji muungno kuvunja au kubosha atamke hivyo kisheria basi sisi wazanzibari mutakuwa mushatufungulia mlango,lakini kwa sasa inabidi tuvunje ukuta ndio tupate mlango, ndio huo mkataba, na najua mkata muta ukataa wenyewe, sio ndio heri yetu, mutuachie zanzibar huru hatutaki muungano ,just ujirani mwema ka uk na marekani huko unako kusifu wewe.
Na hapa ndipo nashindwa kuwaelewa...nadhani mnafaidika na Muungano na hizi kelele zenu, kama alivyosema Baba wa Taifa, ni kama za mtoto mdogo...ukimpakata anakunyea, ukimwacha analia. Zanzibar kama ilivyo inao uwezo wa kuamua kutoka ama kubaki kwenye Muungano...mna katiba, mna serikali, mna baraza la Wawakilishi, vyombo ambavyo Sudani Kusini hawakuwa navyo! Wao walitambua kuwa kukaa tu wakilialia hakutawapa uhuru walioutaka, walichukua hatua, je na ninyi?
 
Last edited by a moderator:
Zanzibar pia ilijitangazia uhuru wake mnamo tarehe 10-12-1963 na kuwa mwana chama wa UN siku moja na kenya,watanganyika waliivamia z'br tarehe 12-1-1964,hadi leo wameifanya z'br kama mkoa,rejea pinda pale bungeni aliposema z'br sio nchi,unataka mfano upi tena kama c wa timor,rudi darasani.

sasa hapa ndio ipo sababu kubwa zaidi ya nyinyi kujitangaza uhuru kwa vile mlivamiwa! PLEASE DO THE NEEDFUL.
 
Yeah, lakini serikali ya Muungano haijawahi kulalamika kuwa kuibeba Zanzibar ni mzigo. Lakini vile vile akianzisha Rais wa Muungano mchakato Wazanzibari hawa hawa wataanza "unaona hawatutaki kwenye Muungano". Hili linatakiwa kuwa ni suala la Wazanzibari wenyewe. Lakini mfano wa East Timor unaweza usiwe mzuri kwa sababu East Timor haikuwa na serikali yake na vyombo vyake isipokuwa vile vya Umoja wa Mataifa.

Na pia historia ya East Timor siyo sawa na Zanzibar; East Timor ilijitangaza huru lakini ikavamiwa na Indonesia na kufanywa Jimbo la 27 la Indonesia. Serikali ya Muungano wa Tanganyika haikuvamia Zanzibar wala kuigeuza Zanzibar mojawapo ya mikoa yetu. Mfano wako wa East Timor hapa haufai.
Umesahau samuel sitta alipoongea bungeni kuwa zanzibar ni mzigo, wakati wabunge wa zanzibar walipokuja juu suala la muungano, samuel sitta akaja juu na hoja ya kuwa wanaidai zanzibar bilioni 50 za umeme,walipwe ndio muungano ujadiliwe, lakini walisahau kuwa katika bank kuu zanzibar kuna asilimia 11,wanaipa asilimia 4.5 mbona husemi ? kama mzigo kwenu munatusaidia vya kutosha na munaona hatuna shukurani mbona mzigo hamutaki kuutua ? mara ngapi wabunge wa zanzibar wanaleta hoja suala la muuungano ? munakuwa wakali sana mukitajiwa uhuru wa zanzibar.

Zanzibar mumeikalia kijeshi, rais wa zanzibar ni kibaraka wenu, ametoka ndani ya dodoma, hivi kwa akili yako anaweza kuuvunja muungano ? Unajua kuwa urais wa zanzibar shein kaupata kwa njia gani ?
 
Na hapa ndipo nashindwa kuwaelewa...nadhani mnafaidika na Muungano na hizi kelele zenu, kama alivyosema Baba wa Taifa, ni kama za mtoto mdogo...ukimpakata anakunyea, ukimwacha analia. Zanzibar kama ilivyo inao uwezo wa kuamua kutoka ama kubaki kwenye Muungano...mna katiba, mna serikali, mna baraza la Wawakilishi, vyombo ambavyo Sudani Kusini hawakuwa navyo! Wao walitambua kuwa kukaa tu wakilialia hakutawapa uhuru walioutaka, walichukua hatua, je na ninyi?
Hivi nyie watanganyika kwa nini hamutaki kusoma, yaani hamuwezi kutoa hoja lazima mumtaje nyerere ? Kwani nyerere mtume au mungu ambaye kwamba akisema jambo lina ukweli ? Nyerere ameleeni vibaya sana badala ya kukupeni elimu anakupeni upumbavu na ulimbukeni.

Nyerere alitamka zahiri kwa mdomo wake kuwa zanzibar inamuumiza kichwa ,na ndio aliamua kufanya mapinduzi na kumchukua okelo kutoka uganda kuja kufanya uhaini zanzibar na kuwaiwa wazanzibari. lete hoja wewe usimsujudie nyerere hapa kashakufa huyo ..
 
Mwanakijiji naamini viongozi wa juu waserikali ya muungano hawana mawazo kama yako , na hii inaonyesha wewe ni kweli mwanakijiji na sio mwana siasa bila shaka mtu kama wewe na wale kutoka bukoba na kwengineko lakini ni watu wa kawaida hawawezi kuona faida ya kuishikilia Zanzibar katika huu tunaouita muungano.

Na ndio mana tumewasikia kila kiongozi anekuja nasema bila ya aibu ataulinda muungano hata ikibidi kutumia nguvu ya dola kwa nini waseme hivi bila shaka kuna kitu amabcho wewe na watu wa kawaida kama wewe utasumbuka kukijiua, kauli ya mwisho ni ya Kikwete inayoendana na marekebisho ya katiba tumemsikia akisema wananchi wapo huru kutowa maoni yaokuhusu katiba lakini sio kuhoji muungano kwa nini ? baada ya kutokea vurugu za uamsho akabdili kauli akasema fujo za nini wakati tume ndo inakusanya maoni alisha sahau ni yeye alisema hakuna kujadili muungano.

Wazanzibar mda huu hawajadili katiba kila anaetowa maoni yupo katika muungano ndio tatizo lao kubwa, na huu muungano kama ungekua upo sawa kwa nini wale majirani zetu hakuna hata mmoja alievutiwa kujiunga nao tayari walishaliona hili ni janga ana badala yake wanumiza vichwa wapo kwenye East African community sio zaidi ya hapo.

Mungano huu ni zaidi ya kituko tokea muungano uundwe mkuu wa nchi muda wote ni kutoka upande mmoja sasa huu muungano gani siku zote rais wa muungano lazima atoke tanganyika kibaya zaidi rais wa tanganyika ndie mwenye mamlaka kikatiba kumteuwa waziri mkuu pamoja na mawaziri wote bila kuhojiwa sasa hapa mwanakijiji kwanini rais wa jamhuri hii asitoke zanzibar hata mara moja ? na jee akitoka zanzibar mtakubali waziri mkuu na mawaziri wengine wachaguliwe kwa mtindo huu ?

muungano wa mktaba kama ni mkataba na sio mazabe ya mkataba wa muungano huu tulionao nadhani itakua suluhisho na hata kama hakutakua na mkataba itakua sawa , Mauritius ,a kina Seychelles wanaweza vipi sisi tusiweze ?, mwanakiji wale wawakilishi kwa siku za karibuni hawawezi na hawatoweza kulisimamia suala hili kwa miaka ya karibuni kwani wao ndio madalali wa kubwa wa huu muungano kwa manufaa ya matumbo yao na watoto wao kama ilivyo kwa viongozi wa Tanganyika.

Na ndio maana unakuta mtu alishafika post ya kuwa waziri mkuu na umri pia umekwenda leo anatanga tanga kukusanya maoni badala ya kukaa akalea vijukuu na kula pension yake.

sifa yako lazima nikupe makala yao ina changamoto nyingi ambazo ni zaukweli .
 
Umesahau samuel sitta alipoongea bungeni kuwa zanzibar ni mzigo, wakati wabunge wa zanzibar walipokuja juu suala la muungano, samuel sitta akaja juu na hoja ya kuwa wanaidai zanzibar bilioni 50 za umeme,walipwe ndio muungano ujadiliwe, lakini walisahau kuwa katika bank kuu zanzibar kuna asilimia 11,wanaipa asilimia 4.5 mbona husemi ?

Asilimia 11 za Zanzibar ziko benki kuu? au katika mtaji wa Benki ya Tanzania Zanzibar ilichangia asilimia 11? Tanganyika ilikuwa na asilimia ngapi kwenye mtaji huo?

Zanzibar mumeikalia kijeshi, rais wa zanzibar ni kibaraka wenu, ametoka ndani ya dodoma, hivi kwa akili yako anaweza kuuvunja muungano ? Unajua kuwa urais wa zanzibar shein kaupata kwa njia gani ?

Hapa ndio unatoa sababu kubwa zaidi ya kutaka kujitoa. Kusanyikeni na wenzako fanyeni walichofanya Wamisri; andamaneni hadi Ikulu ya Zanzibar mtake Shein ajiuzulu ili mpate Rais wenu. Shein si mtu wa bara na siyo Mzanzibari?
 
Tatizo la Zanzibar ni kwamba they want to eat their cake and have it. Keki wanataka kubaki nayo huku wakitaka kuila, haiwezekani. Wachague kimoja, union or no union, kama tumeshindwana katika huu muungano wetu wanadhani tutawezana na mikataba.

Tatizo wanatuona sisi hamnazo, wanadhani bado wataendelea ku-exert the same kind of influence as now, they are dead wrong. Kwetu Zanzibar itakuwa kama Kenya, Sudan etc, waache waende halafu tuje kuonana kwenye majadiliano ya mkataba ndio watajua kama hata huku nationalists kama kina Jussa wapo.
 
Wazanzibar wana hoja ya msingi kuhusu Muungano lakini hoja zao zinafichwa na wanasiasa wao ili waonekane kama wako pamoja na wananchi katika hoja zao huku wakija na vijineno vya mitaani kama 'muungano wa mkataba'.

Wazanzibari hawajui kama kikwazo katika hoja zao siyo wananchi au wanasiasa wa Tanzania bara bali ni serikali ya mapinduzi na balaza la wawakilishi ambao kwa ubinafsi wa kimaslahi na ufahari wanataka kuiaminisha jamii ya wazanzibari kama tatizo ni Tanzania bara.

Ni kama wanapoteza muda kwa sababu wanadai 'haki yao' kusiko, haki yao iko kwa wanasiasa wao ambazo wanawajaza maneno huku wakijificha kwenye mgongo wa katiba ya nchi kama kufanya hivyo ukiwa serikalini ni kukaribisha mashitaka ya uhaini wakati kuna balaza la wawakilishi ambalo liko huru kujadili mstakabali wa Wazanzibari.

Matendo na utekelezaji ndiyo yanayofautisha kati ya Mwanasiasa na kiongozi mpigania maslahi ya watu wake na maslahi ya tumbo lake. Ndiyo haya tunayoyaona kutoka kwa Seif Shariff Hamad
 
@[QUOTE=GHIBUU Mkuu mbona hueleweki? Baada ya kusoma hoja zako hata sijui unachokitaka, yani sitaki-nataka unaonekana. Amua moja- you are either in or out! MMK amekupa solutions nzuri sana, not sure kama umesoma na kutafakari points zake.
 
Naona watanganyika vipovu vya mdomo vinawatokeni midomoni kisa waz'br kutaka muungano wa mkataba,jamani c kila mtu ana mawazo yake acheni kuwa na akili za samaki,kabla hamjakosoa mawazo ya wenzenu wekeni na nyie mawazo yenu ili yajulikane,kama mnaona bora uwe hivihivi muungano huu sasa kuna haja gani ya tume ya warioba kuharibu pesa za walala hoi kuchukua maoni?hivi hadi leo bado watanganyika mnaogopa kivuli cha nyerere?

Wazenj bwana sijui mna matatizo gani. Kama umesoma vizuri bandiko la Mwanakijiji ametoa ufafanuzi na "precedents" mbalimbali ambazo zinahusiana na kile Znz mnachodai. Hayo ndiyo ya mawazo yake na kwa kiasi kikubwa ya Watanganyika. Sasa ni juu yenu kuamua. Ila bottom line ni kuwa hakuna cha "Muungano wa Mkataba". Kama wanavyosema waingereza "You cannot eat you cake and have it".

Ambacho mnachoweza kufanya ni kuanzisha tu process ya kujitoa ndani ya Muungano na kujiunga na mataifa ya Kiarabu, ambalo ndiolo linaonekana kuwa lengo lenu kubwa. Mnaaamini kabisa kuwa Znz inapaswa kuwa "Dubai Ndogo" ila tu ni fitna za Wabara ndio zinakukwamisheni.

Kama wazee wenu waliweza kufanya Mapinduzi kumng'oa Sultan 1964, kimewashindeni nini kufanya mapinduzi mengine kumng'oa Sultan Mbara?
 
Hivi nyie watanganyika kwa nini hamutaki kusoma, yaani hamuwezi kutoa hoja lazima mumtaje nyerere ? Kwani nyerere mtume au mungu ambaye kwamba akisema jambo lina ukweli ? Nyerere ameleeni vibaya sana badala ya kukupeni elimu anakupeni upumbavu na ulimbukeni.

Nyerere alitamka zahiri kwa mdomo wake kuwa zanzibar inamuumiza kichwa ,na ndio aliamua kufanya mapinduzi na kumchukua okelo kutoka uganda kuja kufanya uhaini zanzibar na kuwaiwa wazanzibari. lete hoja wewe usimsujudie nyerere hapa kashakufa huyo ..
Wanajamvi, Kabla sijachangia hoja mwanana na maridhawa ya mwanakijiji, napenda nionyeshe alichokisema Nyerere na kama alivyorudia Mwanakijiji kwa ushahidi ''live''

Nyerere alisema nje ya muungano Zanzibar si salama. Ukisoma hiyo quote ya Ghibuu ambaye hoja zake zinatawaliwa na matusi kuliko mantiki unaweza kupata jambo moja muhimu sana.

Ghibuu anasema Nyerere alimwita Okello afanye mauaji ya Wazanzibar 1964.
Naomba tukubaliane naye kinadharia na katika kiwango chake cha uelewa.

Anachokisema Ghibuu ambacho Wazanzibar wengine pia wanaamini ni kuwa Mapinduzi ya mwaka 1964 hayatokani na Wazanzibar na hivyo si halali.

Hiyo ni tofauti na hoja ya Wazanzibar wengine wanaosema Mapinduzi daima. Hii maana yake ni kuwa wapo wanaosema Mapinduzi daima na wapo wanaosema huo ni uhaini. Hadi hapo ZNZ ina tatizo kama alivyoonyesha Ghibuu na kufuatana na hoja za Mwalimu. Tuachane na Ghibuu kwasababu ni sehemu ya waimba kwaya wasiojua maana ya tungo

Mwanakijiji ameandika kuwa kwa vile GNU ilipatikana kwa ridhaa ya Wazanzibar na kutumia vyombo vyao, hakuna tatizo wao kutoshiriki tume ya Warioba na badala yake waanze mchakato kama ule wa GNU ili kupata Zanzibar huru.

Mwanakijiji, naomba niende mbali zaidi katika hoja zako. Tunapoambiwa muungano wa mkataba kwanza tunatakiwa tuvunje uliopo halafu tufikirie kama kuna muungano wa aina yoyote.
Nasema tufikirie kwasababu Tanganyika haitakuwa tayari kuungana na ZNZ kwa kigezo kimoja tu, ili ipate faida gani.

Lakini pia tukumbuke kuwa katika mchakato wowote au proposal ya jambo ni lazima anayehusika aweke wazi mada yake ili ieleweke. Hao wanaodai muungano wa mkataba kwanza watuambie ni kitu gani, pili nini faida zake na tatu unatekelezwaje na kwa mambo gani.

Haiwezekani tuambiwe muungano wa mkataba bila kujua ukoje, kwanini na kwa jambo gani.
Hao wanaodai muungano wa mkataba sijawahi kuwasikia hata siku moja wakieleza jambo moja tu ambalo wanadhani liwe la mkataba. Kwa maneno ya mitaani yaani wanatuambie twendeni bila kujua wapi kufanya nini,kwa utaratibu gani ili tupate nini. Wanasisitiza twendeni tena kwa hasira wakiamini tutaamka na kukunja viti tuwafuate tu

Kitu kimoja kinachoshangaza katika majadiliano haya ni kuwa Wazanzibar wamejipa haki ya kuamua aina ya mkataba.
Katika kongamano la Oktoba 6 pale Bwawani, Jusa alisema kuwa wao tayari wana muungano wa mkataba ambao wamemkabidhi Seif na katibu wa baraza la Mapinduzi na nje ya hapo hawakubali lolote.

Mansour Himid akasema, endapo muungano wa mkataba hautakubaliwa basi wajumbe wa BLW itabidi wafanye maamuzi magumu sana. Alimaanisha wavunje muungano.

Ni nani amewapa hawa wazanzibar wachache ridhaa ya kuamua mkataba na kwanini Wazanzibar hawajui mkataba unasemaje, yet kundi hilo linashinikiza matakwa yao yakubaliwe?

Je kulikuwa na mchakato wa kuchukua maoni ya Wazanzibar na kuyaweka katika huo mkataba ambao ni siri na unashinikizwa ukubaliwe?

Na je Tanganyika ikikataa mkataba ZNZ itachukua hatua gani na kwanini wasichukue hatua hizo sasa hivi ili kuondoa kadhia hii mapema kwa kujua kuwa muungano wa mkataba unalazimu kwanza uvunjwe uliopo.

Lakini muhimu zaidi ni Wazanzibar kuelewa kuwa Tanzania ikiamua kujitoa EAC ambao ni makubaliano tu, nchi zingine hazitaulizwa kuwa zinakubali au la.

Na kwanini Zanzibar idhani kuwa Tanganyika inapaswa kujadili hili suala la ZNZ kujitoa au la.
Hata kama Tanganyika itashiriki bado jukumu la kujitoa ni la Wazanzibar na hivyo kuokoa muda na gharama ni vema ZNZ yenye eneo dogo na watu wachache sana wafanye maamuzi yao haraka ili tujue wapi tunaelekea.

Kitu kimoja ambacho ni dhahiri ni kuwa matokeo yoyote yale ya mchakato, mahusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar yatakuwa na matatizo. Leo hii Watanganyika wanaelewa kuwa kumbe wao ndio ndio wamebeba muungano.
Hakuna jambo litakaloafikiwa bila Tanganyika kuangalia masilahi yake kwanza siku za mbeleni.

Kwa mantiki hiyo hamkani si shwari na tuwaombe Wazanzibar wafanye maamuzi ya kukamilisha taratibu ili tuvunje dau na tugawane mbao kama zipo za kugawana.
 
Samaki tayari wameshaanza kulewa! Ngoja tusubiri kama jahazi hili lililosheheni malaki ya VIJANA, WAZEE WANAWAKE, WATOTO na WENGINEO kama litaweza kuvutwa na hoja za KIUTASHI kama hizi! Hili wimbi kubwa sana mwanangu na ukijaribu kulipa kifua litakuchana ubavu. Time will tell.
 
Na kwanini Zanzibar idhani kuwa Tanganyika inapaswa kujadili hili suala la ZNZ kujitoa au la.
Hata kama Tanganyika itashiriki bado jukumu la kujitoa ni la Wazanzibar na hivyo kuokoa muda na gharama ni vema ZNZ yenye eneo dogo na watu wachache sana wafanye maamuzi yao haraka ili tujue wapi tunaelekea. .

Unajua tulivyoanza 2012 nilidhani Wazanzibari wangekiunguza mwaka huu hivi juzi (tarehe 10) nilidhani ndio Zanzibar ingekuwa huru. Lakini hakuna mswada wowote wa kura ya maoni ambao kina Jussa wamejaribu kuuleta kwenye baraza la wawakilishi. Inabidi tuendelee kuwahamiza wafanye hivi haraka ili tujue mchakato wa Katiba Mpya ambao unaendelea unahitaji kuangalia Zanzibar au Tanganyika tu. Maana Zanzibar tayari wana katiba yao 'mpya'.
 
Back
Top Bottom