Hoja ya "Muungano wa Mkataba" ni Muflisi!

Napenda sana kutoa hoja kabla ya kumwita mtoa hoja mbadala" mjinga, hajasoma mpumbavu na mambo mengine kama haya" Hoja ndiyo itakayofunua ujinga au ueledi wa mtoa hoja.
Katika maelezo yako unasema, nanukuu " Tukienda mataifa ya nje kuomba misaada ya hiki au kile tuanaambiwa Waziri wa Mambo wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa hapa. Tumempatia" Swalilangu ni kuwa mtu anayekwenda kwenye Taasisiza za kimataifa kuomba misaada kwa nini anapita kinyemela (By pass) kwenda huko kuomba huko nje hajui aanzie kwenye Wizara husika. Kinidhamu ya utumishi kumruka kiongozi wako ni utomvu wa nidhamu. Ina maana Viongozi wa Serikali ya Zanzibar ni watomvu wa nidhamu au hawajui jinsi ya mawasiliano.
Kama sheria ni kikwazo, kwa nini sheria mbaya isibadilishwe? Ni mara nyingi tunashuhudia sheria zinabadilishwa ili kukidhi matakwa ya kisheria kwa wakati mwafaka, kwa nini hii ishindikane.
Katika hadidu zake za rejea, Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia alisema " tusihoji Muungano",lakini mtamshi ya Rais sio sheria. Mwenyekiti wa Kamati ya kukusanya Maoni ya mabadiliko ya Katiba Mheshimiwa Jaji Sinde Warioba alisema maoni yote yatasikilizwa na kuwasilishwa. Nilidhani nifursa nzuri kutoa maoni yanayopendekeza kujitoa kwenye Muungano wa Serikalimbili. Angalizoni kwamba kama fursa hii itatumika kuonyesha hasira kwa njia ya matusi itawanyag'anya Wazanzibar uwezo wa wa saili wa kuona lililo jema na baya. Vitabu vitakatifu Bliblia inatahadhalisha kwa kusema " Hasira hukaa kifuani pa wa pumbavu'
Watu toeni hoja pasipo kutukana mtu yeyote, ikiwa hoja ni ya msingi itasikilizwa tu, hapana haja kutumia msuli ili ueleweke.
Haya mawazo yako ya kijinga hayana mashiko yoyote kwa samaki, wewe huwezi kujua zanzibar inaisaidia vipi tanganyika ,mambo haya mtu wa kawaida kama wewe huwezi kujua ,samaki ukimuuliza atakuwambia.

Kuna mambo haya ambayo tanganyika hufaidika kwa muavuli wa muungano.

kwanza kimataifa, utambue jambo lolote ambalo la muungano au silo la muungano, akiindia rais wa united repulic of tanzania ujue linawakilishwa kimuungano, zanzibar huambulia patupu, kama kuna furushi la bilioni dola 200 zitatolewa huko UN basi munafaidika nyie zanzibar huambulia patupu.

zanzibar ikienda njee kuomba msaada wakifika tu huko, huwambiwa ah membe kafika hapa kashaondoka na furushi, kwani hamujapatiwa chenu huko zanzibar ? nyie si muna serikali ya muungano ? Ah hatujapata kitu, jibu mutajuana wenyewe.

Climate change

Imetoa furushi kwa maneo ambayo yamezungukwa na bahari kwa mfano mafia, zanzibar, comoros, na sehemu nyengine, ambazo huwathirika na tabia nchi, maji kupanda juu na mengine , mfuko huu hutolewa na jumuiya ya mataifa, tanzania hupata dongo nono sana ,bahati mbaya zanzibar huambulia patupu,tukienda kuomba msaada huo tunaambiwa tushapewa,tukiulizia huko tanganyika jamani tupeni chetu, ah hichi chetu tumepewa sie dai chenu, haya ndio matunda ya muungano ,wewe mwanakijiji unajidai hufaidikia basi muulize membe waziri wako atakuwambia.

Kuna mengi sana ambayo munafaidika na muungano,lakini hayo ni machachetu mpumavu kama wewe ambae hukusoma au sijui ukaidi tu huelewi ,hutaki ukweli, nafikiri ungelisoma masuala ya uchumi, ungelielewa zaidi na vipi munafaidika katika muungano huu. zanzibar imeanguka kiuchumi kutokana inashindwa kujiamulia mambo yake wenyewe hasa pale inapotaka kufanya ushirikiana na nchi nyengine katika nyanja za kiuchumi, haiwezi bila ya kuomba kibali kwa membe, na hilo ndio kikwazo.

zanzibar ilitaka kujiunga na OIC kwa vile zanzibar ina asilimia 99 waislamu, muungano umewazuiya hilo suala kwa nini ? Munajenga hoja za siasa chafu na kibaguzi eti waislamu sijui magaidi, sijui usultan tunataka kuleta , yaani upumbavu mtupu,,, kwa nini munatuingilia katika maamuzi yetu ?

Hatutaki tena, tunataka zanzibar yetu.

Na kumalizia jiulize kwa nini tunataka muungano wa mkataba ? wakati huo huo tunadai zanzibar huru? Suali zuri sana, na nitakujibu .

Ukweli ni kwamba sheria ambayo inatupa uhuru wa kujadili muungano, ni sheria ambayo inatupa kuuboresha tu na sio kuvunja, na hilo ndilo suala ambalo wazanzibari limetugusa katika katiba mpya, muungano tu na sio chengine katiba yetu tunayo.

kama ulitaka tutoe maoni ya kudai zanzibar huru tu, na tuukatae muungano kabisa tukutae eac basi mwambie rais wako kikwete aabadilishe kifungu chake katika hadidu rejea kuwa kila raia ana haki ya kuhoji muungno kuvunja au kubosha atamke hivyo kisheria basi sisi wazanzibari mutakuwa mushatufungulia mlango,lakini kwa sasa inabidi tuvunje ukuta ndio tupate mlango, ndio huo mkataba, na najua mkata muta ukataa wenyewe, sio ndio heri yetu, mutuachie zanzibar huru hatutaki muungano ,just ujirani mwema ka uk na marekani huko unako kusifu wewe.
 
Ulitakiwa tu ujue kuwa yupo pale kuwaonyesha kuwa Mnaweza kuanzisha biashara za kawaida tu na mkaweza kuendelea bila kutegemea ukabaji na ujambazi.

Hilo ni somo tosha kwenu kwa mwenye kufikiri.

mie nadhani anatoa somo kwenu kuwa maendeleo ni kujituma na sio kutegemea OIC na UN.pia anawafundisheni umuhimu wa muungano kwenu.ndio maana nimeongea kwa utani lakini kuna fumbo lenye maana ndani yake,kwamba kwa nini ajenge viwanda pale TAZARA badala ya mji mkongwe na kwamba kwa nini alipoachana na urojo zenj na kuja bara kuuza koni na mikate ndipo alipoyatoa maisha?hebu huyu bwana awe mfano kwenu na sio nyie mnaopiga kelele kuwa mnanyonywa na kumbe mnajinyonya wenyewe kwa kutokupenda kufanya kazi na kuleta useless weeping humu!hebu fanyeni kazi bwana!barubaru,uza urojo yakhee,unalipa,ukipata milioni 5 njoo bara nikupe michongo sheikh,huu wimbo unaoimba humu jf utaubadilisha na kuwa mwanaharakati wa kuhakikisha muungano unadumu.ukishapata kaduka kako ka simu za mchina pale tandika utakaa kimyaa..na jf hatutakusikia tena!
 
akuhofu chochote.

Nyerere alikuwa muumini wa Africa moja kama inchi, kwasababu ukifuatilia historia Africa ni berlin conference ndo iliweka mipaka na kutuanzishia inchi hizi. Ndo mana makabila ya watu wanao tuzunguka Tanzania yanashabiana katika mengi.
Nyerere aliona umuhimu wa kuwa na Inchi moja kati ya ZnZ na Tanganyika ndio mana alikazania sana muungano. Alitaka wanachi wake tukienda sehemu tujitambulishe kama Watanzania sio Mtanzania lakini upande wa Bara au Mtanzania lakini mzanzibari.

Muungano wowote siku zote ni positive na una positive result katika walicho unganikia. Wazee wetu waliliona hilo tangu zamani wakatutengenezea Muungano ni sisi ilitakiwa tuje tuuimarishe na kuuboresha. ila wakatokea watu fulani wakiwaaminisha wenzao kwamba wananyonywa,wananyimwa uhuru, tuwe wenyewe, tujitenge.

Lazima tuwe wakweli kwa hili. Nyerere hakuwa na NIa njema na waZnz na Znz kijumla. kama yeye kweli alikuwa na nia ya kuunganisha Afrika na kuifanya kitu kimoja. KWANINI YEYE NDIO ALIKUWA CHANZO CHA KUVUNJIKA KWA EAST AFRICA.

Kama aliweza tumia ushawishi wake kuvunja EAC kwanini aikumbatie Znz kama sio unafiki. Pasi na shaka alikuwa na agenda ya Siri ndani ya mvungano wenu nayo ni kuinyonya Znz kiuchumi, kijanii na hata kiutamaduni.

Huyo ndio chanzo kikubwa sana kwa Tanzania kuwa miongoni mwa nchi masikini duniyani kwa sababu ya Sera zake za kujipendekeza kisiasa na kuumaliza uchumi wake.

Watanganyika wenzangu mura Mwanakijiji wakati umefika kuwaacha wanzanzibar waende zao mbona nchi yetu bado kubwa sana ile hali Zanzibar ni overpopulated island na threat from raising sea level watamulia majini, watu wanavikimbia visiwa pacific, jambo la kusitikisha kwamba wanaotaka uhuru na mkataba wako bara na nje ya Zanzibar. Yangu macho
 
Asilimia 11 za Zanzibar ziko benki kuu? au katika mtaji wa Benki ya Tanzania Zanzibar ilichangia asilimia 11? Tanganyika ilikuwa na asilimia ngapi kwenye mtaji huo?

Hapa ndio unatoa sababu kubwa zaidi ya kutaka kujitoa. Kusanyikeni na wenzako fanyeni walichofanya Wamisri; andamaneni hadi Ikulu ya Zanzibar mtake Shein ajiuzulu ili mpate Rais wenu. Shein si mtu wa bara na siyo Mzanzibari?
Unaniuliza mimi asilimia ngapi ilitoa tanganyika kwani hesabu hujui au wajipumbaza ?

Unasema tujikusanye kama wamisri sisi sio wamisri sisi ni wazanzibari na kila nchi ina siasa zake na historia zake, mara ngapi tushaandamana mbona haijawa kitu, umesahau mauwaji ya 2001 ya wazanzibari ya maandamano ? Au ndio unataka tena hayo mufanye ili muje kutuulia ndugu zetu ?
 
Usichezee serikali nyinyi, wako wanao beza wazanzibari juu ya matakwa yao eti tuandamane kama wamisri hivi mumesahau mauwaji ya wazanzibari 26-27 januar 2001

KWA haya, hakuna atakayeepuka kukamatwa na Fatou Bensouda "Ocampo" wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) mjini The Hugue, Uholanzi. Fuatana nami.
Fatuma "Ocampo" aweza kuchunguza wahusika katika kutekwa, kupigwa na kujeruhuwa kwa Dk. Steven Ulimboka, mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari nchini.
Dk. Ulimboka – mtetezi wa maslahi ya madaktari na haki za wagonjwa – alitekwa, kuteswa, kupigwa na kisha kutupwa katika msitu wa Majipande, nje ya jiji la Dar es Salaam na wanaoitwa na serikali, "watu wasiojulikana."
Katika hili, "Ocampo" aweza kuchunguza Rais Kikwete ama kubariki au kunyamazia; au ama kuzembea kiapo chake cha kulinda uhai wa raia.
Aweza kuchunguzwa pia kwa uzembe wa kushindwa kupata suluhu kwenye mgogoro kati ya serikali na madaktari.
Uchunguzi unaweza kuanzia pale Dk. Ulimboka anapotaja jina la mtu aliyemteka na kusema ni "mwajiriwa wa Ikulu."
Dk. Ulimboka anasema anamfahamu aliyemteka; na aliwahi kukutana naye wakati wa mgogoro wa kwanza wa madaktari.
Kikwete ameliambia taifa kuwa serikali yake haihusiki na kutekwa kwa Dk. Ulimboka. Akatuhumu madaktari kuendesha mgomo kwa kile alichodai "ni kinyume na maagizo ya mahakama."
Serikali ikamkamata kiongozi wao, Dk. Namala Mkopi. Ikamfungulia mashitaka ya jinai mahakamani kwa madai ya "kukiuka amri halali ya mahakama."
Katika mgogoro huu, ni serikali iliyokimbilia mahakamani kuzuia mgomo; lakini haikurudi huko kuiridhisha mahakama kuwapo kwa ukiukwaji wa amri yake.
Aidha, "Ocampo" aweza kuchunguza kigugumizi cha rais cha kunyamazia wito wa kutaka kundwa kwa tume huru.
Ni tofauti na ilivyokuwa kwenye mauwaji ya wafanyabiasahara watatu wa madini mkoani Morogoro mwaka 2006. Hapa rais aliunda kwa haraka, tume huru ya Jaji Mussa Kipenka.
Orodha ya wanaoweza kuchunguzwa ni ndefu. "Ocampo" aweza kuchunguza minendo ya siri ya kachero Na. 2 katika idara ya usalama wa taifa, Jack Zoka anayetajwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ndiye aliyepanga mpango wa siri wa mauaji, utekaji na utesaji wa Dk. Ulimboka.
Aweza kuchunguza mauaji ya raia katika kipindi cha kuelekea chaguzi ndogo za Arumeru, Igunga na baadhi ya kata.
Katika chaguzi hizo, ndiko wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza, Salvatory Machemli (Ukerewe) na Highness Kiwia (Ilemelela), walijeruhiwa kwa mapanga.
Inadaiwa kuwa wabunge hawa walishambuliwa mbele ya askari polisi; na gari iliobeba washambuliaji inamilikiwa na mmoja wa viongozi wa CCM.
Kazi ya uchunguzi ya kifo cha Mbwana Masoud aliyefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha wakati wa kuelekea uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Igunga, yaweza kufanyika. Mbwana alikuwa mfuasi wa upinzani.
Katika kipindi hicho, ndipo pia mwenyekiti wa CHADEMA katika kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo alichinjwa kama kuku na wanaoitwa na serikali, "watu wasiofahamika."
Mbwambo alikuwa mkosoaji mkuwa wa serikali na alikuwa mwiba kwa viongozi wa chama kilichopo ikulu.
Mauwaji ya 5 Januari 2011, jijini Arusha yaliofanywa na jeshi la polisi, nayo yaweza kuchunguzwa.
Vurugu za kisiasa za kisiasa za 26 na 27 visiwani Zanzibar, nazo zaweza kuchunguzwa na kumpa kazi "Ocampo."
Katika mauaji hayo ya Januari 2001, visiwani Zanzibar, polisi kwa kushirikiana na vikosi vya serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wanaripotiwa kutumia risasi za moto kuondoa maisha ya raia. Hadi leo hii, hakuna hatua zilichokuliwa.
Si hivyo tu: Katika kipindi cha utawala wa Mkapa, watu zaidi ya 52 wanadaiwa kufukiwa chini ya mgodi wa dhahabu wakiwa hai, huko Bulyanhulu, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
Ukatili huu dhidi ya mwanadamu ulifanyika kati ya 30 Julai hadi 7 Augosti 1996. Watu wengine wanaokadiriwa kufikia laki nne, walifukuzwa kwenye makazi yao na wamiliki wa mgodi.
Ilifahamika baadaye kuwa polisi walitekeleza ukatili huu baada ya kulipwa ujira wa kiasi cha dola za Kimarekani 3,000 (sawa na Sh. 13.5 milioni wakati huo) na kampuni ya Sutton Resources Limited ya nchini Canada.
Kampuni hii ilidai kumiliki mgodi huo kupitia kampuni ya Kahama Mining Corporation Ltd.
Jeshi la polisi lilifanyakazi ya kuhamisha watu kwa nguvu, licha ya kuwapo zuio la mahakama kuu kanda ya Tabora. Hapa "Ocampo" aweza kuangalia ushiriki wa Mkapa na serikali yake katika mauaji na ukatili huo.
Mbali na Mkapa mwingine anawajibika kuulizwa hili, ni Tuamini Kiwelu, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga wakati mauaji yanafanyika.
Huyu ndiye anayethumiwa kusimamia zoezi la uhamishaji watu, wakati kukiwa na amri halali ya mahakama.
"Ocampo" hapa aweza kuchunguza juu ya tuhuma za kubariki; au kunyamazia vitendo vya ukatili vilivyofanywa na polisi dhidi ya binadamu, matumizi mabaya ya madaraka hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Awezaye kuulizwa hili, ni Omari Mahita, aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi wakati wa utawala wa Mkapa.
Kiongozi huyu wa polisi, kinyume na kiapo chake, alijipa kazi ya kupigia kampeni CCM. Siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2005, huku akijua kuwa ni uwongo, Mahita alilitangazia taifa kuwa Chama cha Wananchi (CUF) kimeingiza silaha aina ya visu na majambia.
Mwingine ambaye "Ocampo" anaweza kuanza kuuliza, ni aliyekuwa rais wa Zanzibar, Dk. Salimin Amour.
Pamoja na kwamba kiongozi huyu hakuwa na dola, lakini ndiye aliyekuwa anatoa kauli zilizochochea uhasama visiwani Zanzibar.
Katika kipindi cha utawala wake – Oktoba 1990 hadi Januari 2001 – Salimin aliliongoza taifa hilo kwa njia ya kibaguzi. Baadhi ya kauli zake ndiyo chimbuko kuu la mauaji ya haraiki ya Januari 2001 Unguja na pemba.
Naye Adadi Rajabu, aweza kuchunguzwa juu ya ushiriki wake wa moja kwa moja; au kushindwa kutimiza wajibu wake, katika kipindi achoshika nafasi ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai.
Adadi ambaye sasa, ni balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, aweza kujibu tuhuma za uhalifu zilizofanywa na baadhi ya polisi waliokuwa chini yake.
Hivyo hivyo kwa Robert Manumba. Aweza kuhojiwa kwa uzembe au kubariki yale yaliokuwa yanafanywa na Adadi na mengine ya sasa.
Katika mshololo huu, mtu pekee anaweza kuikoa serikali kuchunguzwa, ni rais Kikwete pale atakaporidhia uundwaji wa tume huru kuchunguza, pamoja na mambo mengine, waliomteka Dk. Ulimboka.
Kwa haya, mwendesha mashitaka mkuu wa ICC, aliyechukua nafasi ya Luis Moreno Ocampo, bila shaka amepata kazi nchini.
 
Napenda sana kutoa hoja kabla ya kumwita mtoa hoja mbadala" mjinga, hajasoma mpumbavu na mambo mengine kama haya" Hoja ndiyo itakayofunua ujinga au ueledi wa mtoa hoja.
Katika maelezo yako unasema, nanukuu " Tukienda mataifa ya nje kuomba misaada ya hiki au kile tuanaambiwa Waziri wa Mambo wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa hapa. Tumempatia" Swalilangu ni kuwa mtu anayekwenda kwenye Taasisiza za kimataifa kuomba misaada kwa nini anapita kinyemela (By pass) kwenda huko kuomba huko nje hajui aanzie kwenye Wizara husika. Kinidhamu ya utumishi kumruka kiongozi wako ni utomvu wa nidhamu. Ina maana Viongozi wa Serikali ya Zanzibar ni watomvu wa nidhamu au hawajui jinsi ya mawasiliano.
Kama sheria ni kikwazo, kwa nini sheria mbaya isibadilishwe? Ni mara nyingi tunashuhudia sheria zinabadilishwa ili kukidhi matakwa ya kisheria kwa wakati mwafaka, kwa nini hii ishindikane.
Katika hadidu zake za rejea, Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia alisema " tusihoji Muungano",lakini mtamshi ya Rais sio sheria. Mwenyekiti wa Kamati ya kukusanya Maoni ya mabadiliko ya Katiba Mheshimiwa Jaji Sinde Warioba alisema maoni yote yatasikilizwa na kuwasilishwa. Nilidhani nifursa nzuri kutoa maoni yanayopendekeza kujitoa kwenye Muungano wa Serikalimbili. Angalizoni kwamba kama fursa hii itatumika kuonyesha hasira kwa njia ya matusi itawanyag'anya Wazanzibar uwezo wa wa saili wa kuona lililo jema na baya. Vitabu vitakatifu Bliblia inatahadhalisha kwa kusema " Hasira hukaa kifuani pa wa pumbavu'
Watu toeni hoja pasipo kutukana mtu yeyote, ikiwa hoja ni ya msingi itasikilizwa tu, hapana haja kutumia msuli ili ueleweke.

Ndugu yangu.

Hizi wizara ambazo sio za muungano pia unataka tuombe ruhusa kutoka kwenu ? Hili halipo katika makubaliano ya muungano, na ndio maana wapokwenda nje viongozi wetu katika kuomba vifaa mfano vya hospital wizara ya afya wanapofika katika mataifa tajiri wanajikuta tayari wameshachelewa, kivipi ? Waziri wa afya wa jamuhuri ya muungano anapokwenda njee huko wao humtambua kama ni waziri wa muungano ni sio waziri wa tanzania bara kama wenyewe munavyo jina badala ya tanganyika.

Wakati wizara hio sio ya muugano, huoni hapo kuna mparaganyiko ? Yaani kitu chetu wenyewe lazima tuombe ruhusa ? Hilo ndio kero kubwa kwa wazanzibar, rais wetu akienda nje anaonekana kama waziri wa kawaida, kutokna na mfumo wa muungano.

Tunaka zanzibar iliyo huru ya mwaka 1963. Tuacheni tupumue. sema jengine kaka.
 
mie nadhani anatoa somo kwenu kuwa maendeleo ni kujituma na sio kutegemea OIC na UN.pia anawafundisheni umuhimu wa muungano kwenu.ndio maana nimeongea kwa utani lakini kuna fumbo lenye maana ndani yake,kwamba kwa nini ajenge viwanda pale TAZARA badala ya mji mkongwe na kwamba kwa nini alipoachana na urojo zenj na kuja bara kuuza koni na mikate ndipo alipoyatoa maisha?hebu huyu bwana awe mfano kwenu na sio nyie mnaopiga kelele kuwa mnanyonywa na kumbe mnajinyonya wenyewe kwa kutokupenda kufanya kazi na kuleta useless weeping humu!hebu fanyeni kazi bwana!barubaru,uza urojo yakhee,unalipa,ukipata milioni 5 njoo bara nikupe michongo sheikh,huu wimbo unaoimba humu jf utaubadilisha na kuwa mwanaharakati wa kuhakikisha muungano unadumu.ukishapata kaduka kako ka simu za mchina pale tandika utakaa kimyaa..na jf hatutakusikia tena!

Muungwana yoyote inakuwa kwake kwanza taifa halafu ndio mengine,hata zanzibar ikiachwa ipumue hayo yatakuwepo hamtokuwa na uwezo wa kuyazuia,jamhuri ya watu wa z'br kwanza ice-cream baadae.
 
Watanganyika wenzangu mura Mwanakijiji wakati umefika kuwaacha wanzanzibar waende zao mbona nchi yetu bado kubwa sana ile hali Zanzibar ni overpopulated island na threat from raising sea level watamulia majini, watu wanavikimbia visiwa pacific, jambo la kusitikisha kwamba wanaotaka uhuru na mkataba wako bara na nje ya Zanzibar. Yangu macho

Wale uamsho wanatoka wapi?unaota!!
 
Muungwana yoyote inakuwa kwake kwanza taifa halafu ndio mengine,hata zanzibar ikiachwa ipumue hayo yatakuwepo hamtokuwa na uwezo wa kuyazuia,jamhuri ya watu wa z'br kwanza ice-cream baadae.

ungekuwa muungwana mwenye utaifa rohoni mwako ungetanguliza utanzania wako kabla ya uzanzibari kama sie tulioacha usukuma,uchagga na uzaramo wetu.wewe huna utaifa ndio maana sio shida kwako kuibomoa tanzania ili upate zanzibar na haitakuwa shida kwako kuibomoa zanzibar ili upate pemba,na haitakuwa shida kwako kuibomoa pemba ili uupate uarabu na ubara.hamna utaifa hapo,ni ubinafsi,chuki,roho mbaya na ubaguzi tu!
 
na wote wenye sera za aina hii hawana tofauti na MAKABURU! NI MAKABURU TU!na wewe ustaadhi wangu Nurdin hata sikuonei haya,wewe nawe KABURU TU!
 
This is what I wrote in another thread earlier on and I think it might be relevant to this thread too:

Its time for Zanzibari's to make up their minds..no more bullshiting, no more ambiguous statements, no more standing over the fence..The first step is to answer the question that, do you want to be part of the Union or not? If not, then end it now because everything anyone( whichever government in power does will be in vain)..if yes, then other measures can follow up.

The solutions on my part is as follows: It seems that Zanzibaris dont want to lose their identity, they want to be identified as Zanzibaris first then Tanzanians second. This is what makes the union so fragile, example..I'm a muhaya by tribe, but I have never ever identified myself as Muhaya from Muleba first then Tanzanian second..Its always I'm a Tanzanian then if a person asks me specifically for my tribe, i will tell him a haya..this is direct opposite of Zanzibari's, they dont want to be fully committed to being Tanzanian that's why they are ever complaining of being intruded in their policy matters by Tanganyikans. The only way forward is for Zanzibaris to accept that they are Tanzanians first then Zanzibari's second..if they cant, let them break off from the union and be a republic.

The other solution is not a straight forward one and it might lead to more harm than good: the solution is devolution of powers from the Tanzanian mainland government towards the Zanzibaris government, that is giving the parliament of Zanzibar more autonomy so that they can determine their own policies..the only powers that the Tanzanian government will be left are important issues ones such as defence, national security etc..I personally do not condone this approach because of the simple reason that it leads to further lack of clarity of what should be in the union and what should not.

The author of the page asked for the Tanganyikans opinions: here is my opinion: we Tanganyikan's are already Tanzanians..we accept Tanzania for good or for bad, for better or for worse..its high time for Zanzibari's to answer a simple question: are you a Tanzanian or not?

Here Mwanakijiji spoke very clearly about the situation..its Zanzibaris to decide what course is their country heading for, all this other bullshit of "we want this but not this, we want that, but not that" lacks clear clarity and a fundamental objective..If I had the power, I would recommend that Zanzibar becomes a region of Tanzania, just like Mwanza..one nation, one people, one government..We are all Tanzanians under one roof, we are not Tanzanians and Zanzibari's..all I'm asking for is further unity.
 
na wote wenye sera za aina hii hawana tofauti na MAKABURU! NI MAKABURU TU!na wewe ustaadhi wangu Nurdin hata sikuonei haya,wewe nawe KABURU TU!

Kuitwa Kaburu sio issue kubwa na wala sio dhambi kama mtu anadai haki yake.

zanzibar inataka uhuru wake na kurejeshewa utaifa wake kwani hilo ni haki yao kama nchi huru. na kumbuka haki haiombwi bali inadaiwa.
 
Mkuu wangu, asante kwa ufafanuzi mzuri. Kumbe hapa tatizo sio Muungano na wala sio viongozi wa serikali. Tatizo ni wale wanaotoa majibu na wanaomba misaada kwa upande wa Zanzibar. Nasema hivi kwa sababu moja kuu. Kwanini watoe misaada kwa Wizara zizokuwa za muungano kwenye serikali ya muungano? Viongozi wa Zanzibar wanaoenda kuomba hiyo misaada kwenye taasisi za Kimataifa wanashindwaje kutetea hoja zao zikaeleweka katika taasisi za kimataifa? Lipi jambo rahisi hapa, kuvunja muungano au kueleza bayana jinsi muungano wetu ulivyo? Sifa moja ya kiongozi ni yule anayeielwa siasa, anaweza kuieleza na kuitetea. Ikiwa Wazanzibar hawauelewi muungano, hawawezi kueleza na kuutetea inakuwa shida watu wa nje kuuelewa vizuri muungano wetu.
Jambo lingine ninaloliona ni kama la aibu kidogo, ndugu hatugombani kwa sababu ya ugomvi wetu kama vile Watanzania bara ni wakorofi dhidi ya ndugu zao wa Tanzania visiwani la hasha! Tunagombana kwa sababu ya misaada ya watu. Ni kama ndugu wa tumbo moja wanagombana sababu ya mke, tena mke wa mtu. Kwa nini tusifanye kazi kutumia rasilimali zetu halafu tujadiliane ni namna gani tugawane? Tutatengana sababu ya kupata misaada na wenye misaada wakakataa kutupa baada kutengana, itakuwaje?
Tangu kale wahenga walisema " Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu" Hekima hii ndiyo iliwaongoza Mwalimu Nyerere na Karume kutaka kuungana. Ni kawaida mwenye hekima kujua neno la hekima na asiyehekima kupingana nalo. Pia kwenye jamii yoyote ile wenye hekima huwa wachache kuliko wasiokuwa nayo. Wasio na hekima wakipewa uongozi hubeza kila neno la hekima. Mwisho wake huwa majuto na ndiyo maana majuto huitwa mjukuu kwa sababu huja mwisho. Kama kawaida sikio la kufa halina dawa, tuendelee na taratibu za kuuvunja muungano, lakini tujiandae kujuta.
Ndugu yangu.

Hizi wizara ambazo sio za muungano pia unataka tuombe ruhusa kutoka kwenu ? Hili halipo katika makubaliano ya muungano, na ndio maana wapokwenda nje viongozi wetu katika kuomba vifaa mfano vya hospital wizara ya afya wanapofika katika mataifa tajiri wanajikuta tayari wameshachelewa, kivipi ? Waziri wa afya wa jamuhuri ya muungano anapokwenda njee huko wao humtambua kama ni waziri wa muungano ni sio waziri wa tanzania bara kama wenyewe munavyo jina badala ya tanganyika.

Wakati wizara hio sio ya muugano, huoni hapo kuna mparaganyiko ? Yaani kitu chetu wenyewe lazima tuombe ruhusa ? Hilo ndio kero kubwa kwa wazanzibar, rais wetu akienda nje anaonekana kama waziri wa kawaida, kutokna na mfumo wa muungano.

Tunaka zanzibar iliyo huru ya mwaka 1963. Tuacheni tupumue. sema jengine kaka.
 
Natangaza dau kwa yoyote mwenye hati ya muungano wa nyerere aje nayo,natoa 20milio kwa kila mwenye nayo,naamini ikipatikana hiyo inaweza ikatupa muongozo sio kukaa hapa na kudharauliana.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom