Hoja ya kuongezewa muda wa Rais kubakia madarakani itaendelea kwa Rais Samia Suluhu Hassan?

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Awali ya yote tupeane pole kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na Mh Rais John Pombe Magufuli,hakika hayakuwa haya maisha ya dunian ila ni kitu chenye kupita tu.

Hapa karibuni kulikuwa na hoja ya kumuongezea muda wa kubakia madarakani Mh Rais John Pombe Magufuli na wengine wakaenda mbali na kusema kwamba akikataa tumlazimishe, pasipo na kujua kwamba ahadi ya uhai na maisha siri hii ipo kwa Mwenyezi Mungu. Leo hayupo Tena kwenye mgongo wa ardhi, hayupo tena.

Je, wale wahafidhina wa mitano Tena na kuongezwa kwa muda wa kukaa RAIS MADARAKANI, wataendelea na HOJA hii kwa MH RAIS Mama SAMIA SULUHU au walii-personalise kwa Hayati Mh RAIS Magufuli?

Aongezewe au Asiongezewe.
 
Wale walikua ni wa mapambio.
Samia hawezi kutaka Yale Mambo ya kisifa.

Magufuli ndie alikua anataka abaki madarakani.

Akaanza kupandikiza watu waseme kua aongezwe Muda atake asitake.
Mbinu alizokua anatumia za kijinga za kumbakisha madarakani ndio yaliyomperekea kununua hata wapinzani.

Sasa kwa mfano Patrobas katambi kua usalama wa taifa ili iweje, alikua anataka nini.
 
Wachumia tumbo bado wanasikilizia upepo wa Madam kama ataendelea kuwabeba basi na wao watendelea kupendekeza aongezewe muda.
What if kama umepeleka HOJA Kama hiyo na katiba ikabadilishwa, then all of the sudden RAIS huyo anafariki dunia Kama ilivyotokea hivi sasa, then akapatikana RAIS mwingine ambae ni mbovu na muovu, je tutarudi Tena kubadilisha katiba na kupunguza muda wa RAIS KUBAKIA MADARAKANI??
 
Itategemea na jinsi mama atakavyoishi vizuri na CCM mtandao. Hao ndio wenye uwezo wa ku sway the wind on her favor au 'kuharibu kila kitu'.
 
Itategemea na jinsi mama atakavyoishi vizuri na CCM mtandao. Hao ndio wenye uwezo wa ku sway the wind on her favor au 'kuharibu kila kitu'.
Msiba huu hauwez kuwa somo kwao kuwa uhai wa mwanadamu ni mfupi na kwamba hauwez kuutumain katika mabadiliko ya maisha ya watu?instead wakajikita katika kujenga strong institutions badala ya kutegemea strong personalities..?
 
Waliokwa wanataka muhula wa Magufuli uongezwe walikuwa na ajenda binafsi.

Wote walikuwa wanafikiria matumbo yao na jinsi walivyopata vyeo wasivyostahili.

Walijua Magufuli akiendelea kutawala kwao ni ulaji muendelezo.
Sasa hawawezi kutetea hoja hiyo maana hawajui maslahi yao ya kula yapo au hayapo.

Tufuate katiba katika hili.
 
Waliokwa wanataka muhula wa Magufuli uongezwe walikuwa na ajenda binafsi.
Wote walikuwa wanafikiria matumbo yao na jinsi walivyopata vyeo wasivyostahili.
Walijua Mgufuli akiendelea kutawala kwao ni ulaji muendelezo.
Sasa hawawezi kutetea hoja hiyo maana hawajui maslahi yao ya kula yapo au hayapo.
Tufuate katiba katika hili.

Tuiheshimu katiba
 
Awali ya yote tupeane pole kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na Mh RAIS John Pombe Magufuli,hakika hayakuwa haya maisha ya dunian ila ni kitu chenye kupita tuh,

Hapa karibun kulikuwa na HOJA ya kumuongezea muda wa KUBAKIA MADARAKANI Mh RAIS John Pombe Magufuli,na wengine wakaenda mbali na kusema kwamba akikataa tumlazimishe,pasipo na kujua kwamba ahad ya uhai na maisha siri hii ipo kwa mwenyezmungu,leo hayupo Tena kwenye mgongo wa ardhi,hayupo Tena.,he is very dead and very gone..!

Je,wale wahafidhina wa mitano Tena na kuongezwa kwa muda wa kukaa RAIS MADARAKANI,wataendelea na HOJA hii kwa MH RAIS Mama SAMIA SULUHU au wali-Epersonalise kwa Hayati Mh RAIS Magufuli??...

Aongezewe au Asiongezewe...
Duh......long time!
 
Moja ya maradhi ya kudumu ya watu wa Kanda ya Ziwa ni kupenda kusifiwa kupitiliza …

Sie huku Pwani ukinizidishia Sifa naanza kuwa na tahadhari nawe!

Chawa wa awamu ya sita ndani ya tano wawe makini …Mf Lemutuz kaanza kumsifia Mama eti Kanyaga Twende…tumechelewa sana…yaan mara Hii Magu alikuwa anatuchelewesha!?…

Machawa mataahira hayana fursa awamu hii bila shaka
Samia now atake asitake ataongezewa mda..
Au nasema uongo ndugu zangu??
 
Moja ya maradhi ya kudumu ya watu wa Kanda ya Ziwa ni kupenda kusifiwa…

Sie huku Pwani ukinizidishia Sifa naanza kuwa na tahadhari nawe!

Chawa wa awamu ya sita ndani ya tano wawe makini …Mf Lemutuz kaanza kumsifia Mama eti Kanyaga Twende…tumechelewa sana…yaan mara Hii Magu alikuwa anatuchelewesha!?…

Machawa mataahira hayana fursa awamu hii bila shaka
Umenichekesha.
Nimecheka kwa sauti alafu Niko peke yangu.
 
Back
Top Bottom