Hoja ya Gwajima nchi kukosa maono kwa sababu ya kila Rais kuja na lake ni uongo mkubwa

Lakini jk kiongozi wa kundi la ssh ni bingwa wa mikakati ya kisiasa*
1.jk ni kiongozi wa ssh
2.amefanikisha mkakati upi wa kisiasa?
3
Mikakati mingi tu mkuu, ya zamani wakati wa Lowassa akiutaka urais na hii ya sasa akiwa anamtetea SSH nyuma ya pazia bila ya kuonekana.

Ukipambana na SSH jua kuwa yupo JK nyuma yake, hivyo jiandae kupigwa nguma na usiye muona.
 
Kwa hiyo jk ndiye mentor wa Samia mbona ccm wanakanusha hili.
 
Ni vyema Askofu Gwajima na wote walioguswa na hoja yake leo bungeni kupitia mchango wake kwamba tatizo kubwa letu ni ukosefu wa dira na mipango ya muda mrefuuu, sio ukweli bali ni uongo mkubwa, na ni Professorial Rubbish.

#Gwajima Apuuzwe.
Duh...!.
Unamaanisha Gwaji Boy ni muongo?.
Please acha kumsingizia Mhe. Mbunge wetu kuwa ni muongo!. Hiki alichosema ni ukweli mtupu ila ni ukweli mchungu!.
P.
 
Nigeria bado ni nchi yenye taasisi dhaifu Rais ana madaraka makubwa sana.Yeye ndiye anateua IGP na wakuu wa majeshi bila bunge kuhusika kuwaadhinisha, mkuu wa Tume ya uchaguzi anamteua yeye.Pia ni nchi iliyopitia utawala wa kijeshi kwa muda mrefu mara tu baada ya kupata uhuru. Sio sahihi kuitolea mfano na kuulinganisha mfumo wake na US hata kwa mbali tu.

Ufaransa ina powerful presidency ila haina "Urais wa kifalme". Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa. Rais wa Ufaransa anachekiwa kwa kiasi kikubwa na Bunge pamoja na mahakama.

Uingereza na Japan wana mabunge imara sana ambayo huwa yamewaondoa mawaziri wakuu mara nyingi. Hizi ni nchi ambazo waziri mkuu akiteleza kidogo tu anaweza kupoteza nafasi yake.

Dunia ya leo ni vigumu kukubali "benevolent dictatorship" kama ile ya Singapore ya miaka ya 1970. Watu wengi wanaamini maendeleo yanaweza kupatikana katika demokrasia kubwa bila kuzitoa haki za raia na uhuru kafara.
Akili zako ni ndogo.
 
Bahati nzuri sana au sijui niseme bahati mbaya, katika Taifa letu kuna watu wamekuwa wana mawazo mazuri sana wanapuuzwa sana na kundi la vigele gele na shangwe na kundi linaangalia nani kasema. Ukweli ni lazima tuwe na Taifa lenye maono ya miaka 100 kwenda mbele, na si nchi inayoendeshwa na "projects" ambazo mipango inapangwa na "deal makers". Lazima tuwe na viongozi wenye maona na si tu viongozi ila viongozi wa kweli. Na hawa lazima tuwaandae.

Ukiangalia Tanzania ya mwaka 2030 hujui inakwenda wapi ? Kuna mtu anasema kuwa mataifa makubwa ya wenzetu hayana dira, si kweli. Wao walishajipanga miaka na miaka iliyopita.
 
Ni vyema Askofu Gwajima na wote walioguswa na hoja yake leo bungeni kupitia mchango wake kwamba tatizo kubwa letu nchi za Africa ni ukosefu wa dira na mipango ya muda mrefuuu wafahamu hili ambalo Gwajima amekuwa akirudia kulisema sio ukweli bali ni uongo mkubwa, na ni Professorial Rubbish.

Hizo nchi Gwajima anazoona zimeendelea sana hazikuendelea kwa sababu ya kuweka mipango ya miaka 5,10, 20 au 50. Tukichukua mfano wa US, hawa hana hata mpango wa miaka 5 kama sisi. Wao nchi yao ina muendelezo kwa sababu maamuzi makubwa yanaamuliwa katika ngazi za mabunge ya Taifa na majimbo, mahakama na taasisi nyingine nyingine nyingi. Rais anakuwa na nafasi finyu sana ya kufanya maamuzi makubwa kama haunguwi mkono na hivyo vyombo.

Nikirejea maneno ya Aliyekuwa Rais wa Marekani Baraka Obama alipozuru Ghana mwaka 2009 alisema "Africa haihitaji viongozi majabari bali inahitaji Taasisi imara"

Tatizo kubwa la Africa ni Taasisi za nchi kuwa dhaifu.Ukiondoa Africa Kusini na nchi nyingine kwa chache ,kwingine kote Africa Marais wana nguvu na mamlaka kubwa sana ya kuweza kuamua uelekeo wowote nchi zao.

Hili ni tatizo kubwa kwa sababu ukosefu huu wa "checks and balances" unasababisha wengi wao kuyatumia madaraka yao vibaya na kulazimisha ndoto na maono yao badala ya wananchi walio wengi kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na taasisi.

Pia mfumo huu hauchochei uvumbuzi na ubunifu kwa sababu washauri wote na viongozi wa chini wanatenda na kumuambia kiongozi mkuu kile ambacho angependa kusikia badala ya kile ambacho anagepaswa kusikia na hapo ndipo tunapokwama.

Hata tuwe na dira na mipango mirefuuuu ya maendeleo ya miaka 100 au 200 ijayo maendeleo nchini hapa na Africa kwa ujumla hayatakuja kwa kasi kama mfumo wetu wa utawala utabaki wa kuongozwa na viongozi jabiri zaidi kuliko taasisi imara zenye kuchekiana.

#Gwajima Apuuzwe.
Wakati wa mwendazake kwani ilikuwa na dira?
 
Gwajiboy ni mjengaji wa hoja,ila huwa anasahau Jana alizungumza nini?
Mfano.
Awamu yaTano alisema"Ukiwa na safari halafu njiani ukakutana na mbwa wanabweka waache wabweke wewe endelea safari"
Alipigiwa makofi sana na wabunge mbele ya Simba wa Yuda a.k Mfalme Herode
 
Mimi nawapuuza wote wanaompuuza Askofu JOSEPHERT GWAJIMA kwa hili na mengine ila kwa leo naanza na wewe mtoa mada
 
Ni vyema Askofu Gwajima na wote walioguswa na hoja yake leo bungeni kupitia mchango wake kwamba tatizo kubwa letu nchi za Africa ni ukosefu wa dira na mipango ya muda mrefuuu wafahamu hili ambalo Gwajima amekuwa akirudia kulisema sio ukweli bali ni uongo mkubwa, na ni Professorial Rubbish.

Hizo nchi Gwajima anazoona zimeendelea sana hazikuendelea kwa sababu ya kuweka mipango ya miaka 5,10, 20 au 50. Tukichukua mfano wa US, hawa hana hata mpango wa miaka 5 kama sisi. Wao nchi yao ina muendelezo kwa sababu maamuzi makubwa yanaamuliwa katika ngazi za mabunge ya Taifa na majimbo, mahakama na taasisi nyingine nyingine nyingi. Rais anakuwa na nafasi finyu sana ya kufanya maamuzi makubwa kama haunguwi mkono na hivyo vyombo.

Nikirejea maneno ya Aliyekuwa Rais wa Marekani Baraka Obama alipozuru Ghana mwaka 2009 alisema "Africa haihitaji viongozi majabari bali inahitaji Taasisi imara"

Tatizo kubwa la Africa ni Taasisi za nchi kuwa dhaifu.Ukiondoa Africa Kusini na nchi nyingine kwa chache ,kwingine kote Africa Marais wana nguvu na mamlaka kubwa sana ya kuweza kuamua uelekeo wowote nchi zao.

Hili ni tatizo kubwa kwa sababu ukosefu huu wa "checks and balances" unasababisha wengi wao kuyatumia madaraka yao vibaya na kulazimisha ndoto na maono yao badala ya wananchi walio wengi kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na taasisi.

Pia mfumo huu hauchochei uvumbuzi na ubunifu kwa sababu washauri wote na viongozi wa chini wanatenda na kumuambia kiongozi mkuu kile ambacho angependa kusikia badala ya kile ambacho anagepaswa kusikia na hapo ndipo tunapokwama.

Hata tuwe na dira na mipango mirefuuuu ya maendeleo ya miaka 100 au 200 ijayo maendeleo nchini hapa na Africa kwa ujumla hayatakuja kwa kasi kama mfumo wetu wa utawala utabaki wa kuongozwa na viongozi jabiri zaidi kuliko taasisi imara zenye kuchekiana.

#Gwajima Apuuzwe.
Then lazima tupate katiba mpya kwanza ambayo itatoa muongozo vinginevyo ni upuuzi tu.
 
Kama Kuna mtu anaweza kuipinga hoja ya Gwaji boy atakuwa na shida yake,hoja yake alikuwa amekwepa tu kusema tunahitaji katiba mpya itakayokuwa muongozo wa nchi ila akatumia neno "maono"............Kwa alilosema Gwajima yuko sahihi kabisa nchi inacheza ngoma Kwa mdundo wa Rais aliyepo hatuwezi kufika nchi kukosa vipaumbele,kila kitu kina guswa guswa tu na kuachwa
 
Back
Top Bottom