Hoja ya Gwajima nchi kukosa maono kwa sababu ya kila Rais kuja na lake ni uongo mkubwa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,245
45,497
Ni vyema Askofu Gwajima na wote walioguswa na hoja yake leo bungeni kupitia mchango wake kwamba tatizo kubwa letu nchi za Africa ni ukosefu wa dira na mipango ya muda mrefuuu wafahamu hili ambalo Gwajima amekuwa akirudia kulisema sio ukweli bali ni uongo mkubwa, na ni Professorial Rubbish.

Hizo nchi Gwajima anazoona zimeendelea sana hazikuendelea kwa sababu ya kuweka mipango ya miaka 5,10, 20 au 50. Tukichukua mfano wa US, hawa hana hata mpango wa miaka 5 kama sisi. Wao nchi yao ina muendelezo kwa sababu maamuzi makubwa yanaamuliwa katika ngazi za mabunge ya Taifa na majimbo, mahakama na taasisi nyingine nyingine nyingi. Rais anakuwa na nafasi finyu sana ya kufanya maamuzi makubwa kama haunguwi mkono na hivyo vyombo.

Nikirejea maneno ya Aliyekuwa Rais wa Marekani Baraka Obama alipozuru Ghana mwaka 2009 alisema "Africa haihitaji viongozi majabari bali inahitaji Taasisi imara"

Tatizo kubwa la Africa ni Taasisi za nchi kuwa dhaifu.Ukiondoa Africa Kusini na nchi nyingine kwa chache ,kwingine kote Africa Marais wana nguvu na mamlaka kubwa sana ya kuweza kuamua uelekeo wowote nchi zao.

Hili ni tatizo kubwa kwa sababu ukosefu huu wa "checks and balances" unasababisha wengi wao kuyatumia madaraka yao vibaya na kulazimisha ndoto na maono yao badala ya wananchi walio wengi kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na taasisi.

Pia mfumo huu hauchochei uvumbuzi na ubunifu kwa sababu washauri wote na viongozi wa chini wanatenda na kumuambia kiongozi mkuu kile ambacho angependa kusikia badala ya kile ambacho anagepaswa kusikia na hapo ndipo tunapokwama.

Hata tuwe na dira na mipango mirefuuuu ya maendeleo ya miaka 100 au 200 ijayo maendeleo nchini hapa na Africa kwa ujumla hayatakuja kwa kasi kama mfumo wetu wa utawala utabaki wa kuongozwa na viongozi jabiri zaidi kuliko taasisi imara zenye kuchekiana.

#Gwajima Apuuzwe.
 
Huu mfumo siyo mbaya ila watu ndio hawajui kuutumia, shida ya Afrika siyo mfumo kwani Nigeria wana huo mfumo wa USA ulioungelea copy& paste lkn ndo masikini wa kutupwa, hao Magavana wa States ndo corrupt kuliko hata hapa Bongo, huu mfumo wetu umetumika kwingine na umewasaidia mfano Singapore wana mfumo kama wetu hata Ufaransa wana powerful president, huu mfumo ulitumiwa na nchi ya Uingereza na uliwasaidia pia, na ndio waliouleta hapa, Mauritius ilitawaliwa na Uingereza pia lkn wametuzidi mbali sana.
Japan pia wana mfumo karibia sawa na wa kwetu na umewaendeleza.

Shida ni watu wenyewe na utamaduni wetu na siyo aina ya mfumo, maendeleo ni utamaduni wa watu, mtakopi mifumo yote lkn hakuna kitakachobadilila …
 
Kama tutaendelea na mentality hii ya kumiliki maghorofa kwa pesa za kufisadi basi tutakuwa wa hapahapa kama nchi. Maana kila kiongozi alie madarakani anawaza kumiliki mahoteli kila mkoa, muulize yule wa fedha anawaza nn
 
Ni vyema Askofu Gwajima na wote walioguswa na hoja yake leo bungeni kupitia mchango wake kwamba tatizo kubwa letu nchi za Africa ni ukosefu wa dira na mipango ya muda mrefuuu wafahamu hili ambalo Gwajima amekuwa akirudia kulisema sio ukweli bali ni uongo mkubwa, na ni Professorial Rubbish.

Hizo nchi Gwajima anazoona zimeendelea sana hazikuendelea kwa sababu ya kuweka mipango ya miaka 5,10, 20 au 50. Tukichukua mfano wa US, hawa hana hata mpango wa miaka 5 kama sisi. Wao nchi yao ina muendelezo kwa sababu maamuzi makubwa yanaamuliwa katika ngazi za mabunge ya Taifa na majimbo, mahakama na taasisi nyingine nyingine nyingi. Rais anakuwa na nafasi finyu sana ya kufanya maamuzi makubwa kama haunguwi mkono na hivyo vyombo.

Nikirejea maneno ya Aliyekuwa Rais wa Marekani Baraka Obama alipozuru Ghana mwaka 2009 alisema "Africa haihitaji viongozi majabari bali inahitaji Taasisi imara"

Tatizo kubwa la Africa ni Taasisi za nchi kuwa dhaifu.Ukiondoa Africa Kusini na nchi nyingine kwa chache ,kwingine kote Africa Marais wana nguvu na mamlaka kubwa sana ya kuweza kuamua uelekeo wowote nchi zao.
Hili ni tatizo kubwa kwa sababu ukosefu huu wa "checks and balances" unasababisha wengi wao kuyatumia madaraka yao vibaya na kulazimisha ndoto na maono yao badala ya wananchi walio wengi kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na taasisi.

Pia mfumo huu hauchochei uvumbuzi na ubunifu kwa sababu washauri wote na viongozi wa chini wanatenda na kumuambia kiongozi mkuu kile ambacho angependa kusikia badala ya kile ambacho anagepaswa kusikia na hapo ndipo tunapokwama.

Hata tuwe na dira na mipango mirefuuuu ya maendeleo ya miaka 100 au 200 ijayo maendeleo nchini hapa na Africa kwa ujumla hayatakuja kwa kasi kama mfumo wetu wa utawala utabaki wa kuongozwa na viongozi jabiri zaidi kuliko taasisi imara zenye kuchekiana.

#Gwajima Apuuzwe.
Huo ndio ukweli wenyewe.

Madaraka makubwa ya Rais, yamewafanya Watanzanua wengi kuwa vibaraka wa Rais, vibaraka wa Serikali na waabudu Rais.

Na mbaya zaidi wale wanafiki wanaojipendekeza kwa Rais, na wakanufaika wao binafsi, hawataki kuwe na mabadiliko.
 
Nigeria bado ni nchi yenye taasisi dhaifu Rais ana madaraka makubwa sana.Yeye ndiye anateua IGP na wakuu wa majeshi bila bunge kuhusika kuwaadhinisha, mkuu wa Tume ya uchaguzi anamteua yeye.Pia ni nchi iliyopitia utawala wa kijeshi kwa muda mrefu mara tu baada ya kupata uhuru. Sio sahihi kuitolea mfano na kuulinganisha mfumo wake na US hata kwa mbali tu.

Ufaransa ina powerful presidency ila haina "Urais wa kifalme". Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa. Rais wa Ufaransa anachekiwa kwa kiasi kikubwa na Bunge pamoja na mahakama.

Uingereza na Japan wana mabunge imara sana ambayo huwa yamewaondoa mawaziri wakuu mara nyingi. Hizi ni nchi ambazo waziri mkuu akiteleza kidogo tu anaweza kupoteza nafasi yake.

Dunia ya leo ni vigumu kukubali "benevolent dictatorship" kama ile ya Singapore ya miaka ya 1970. Watu wengi wanaamini maendeleo yanaweza kupatikana katika demokrasia kubwa bila kuzitoa haki za raia na uhuru kafara.
Huu mfumo siyo mbaya ila watu ndio hawajui kuutumia, shida ya Afrika siyo mfumo kwani Nigeria wana huo mfumo wa USA ulioungelea copy& paste lkn ndo masikini wa kutupwa, hao Magavana wa States ndo corrupt kuliko hata hapa Bongo, huu mfumo wetu umetumika kwingine na umewasaidia mfano Singapore wana mfumo kama wetu hata Ufaransa wana powerful president, huu mfumo ulitumiwa na nchi ya Uingereza na uliwasaidia pia, na ndio waliouleta hapa, Mauritius ilitawaliwa na Uingereza pia lkn wametuzidi mbali sana.
Japan pia wana mfumo karibia sawa na wa kwetu na umewaendeleza.

Shida ni watu wenyewe na utamaduni wetu na siyo aina ya mfumo, maendeleo ni utamaduni wa watu, mtakopi mifumo yote lkn hakuna kitakachobadilila …
 
Ni vyema Askofu Gwajima na wote walioguswa na hoja yake leo bungeni kupitia mchango wake kwamba tatizo kubwa letu nchi za Africa ni ukosefu wa dira na mipango ya muda mrefuuu wafahamu hili ambalo Gwajima amekuwa akirudia kulisema sio ukweli bali ni uongo mkubwa, na ni Professorial Rubbish.

Hizo nchi Gwajima anazoona zimeendelea sana hazikuendelea kwa sababu ya kuweka mipango ya miaka 5,10, 20 au 50. Tukichukua mfano wa US, hawa hana hata mpango wa miaka 5 kama sisi. Wao nchi yao ina muendelezo kwa sababu maamuzi makubwa yanaamuliwa katika ngazi za mabunge ya Taifa na majimbo, mahakama na taasisi nyingine nyingine nyingi. Rais anakuwa na nafasi finyu sana ya kufanya maamuzi makubwa kama haunguwi mkono na hivyo vyombo.

Nikirejea maneno ya Aliyekuwa Rais wa Marekani Baraka Obama alipozuru Ghana mwaka 2009 alisema "Africa haihitaji viongozi majabari bali inahitaji Taasisi imara"

Tatizo kubwa la Africa ni Taasisi za nchi kuwa dhaifu.Ukiondoa Africa Kusini na nchi nyingine kwa chache ,kwingine kote Africa Marais wana nguvu na mamlaka kubwa sana ya kuweza kuamua uelekeo wowote nchi zao.
Hili ni tatizo kubwa kwa sababu ukosefu huu wa "checks and balances" unasababisha wengi wao kuyatumia madaraka yao vibaya na kulazimisha ndoto na maono yao badala ya wananchi walio wengi kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na taasisi.

Pia mfumo huu hauchochei uvumbuzi na ubunifu kwa sababu washauri wote na viongozi wa chini wanatenda na kumuambia kiongozi mkuu kile ambacho angependa kusikia badala ya kile ambacho anagepaswa kusikia na hapo ndipo tunapokwama.

Hata tuwe na dira na mipango mirefuuuu ya maendeleo ya miaka 100 au 200 ijayo maendeleo nchini hapa na Africa kwa ujumla hayatakuja kwa kasi kama mfumo wetu wa utawala utabaki wa kuongozwa na viongozi jabiri zaidi kuliko taasisi imara zenye kuchekiana.

#Gwajima Apuuzwe.
Tatizo la siasa za mitandao ni kundi fulani kulewa mno madaraka halafu wakajiona kama vile hakutatokea siku moja wakaparaganyika. Wanaanza kufanya mambo ya kijinga wakijua watadumu mpaka kifo kiwakute kumbe ndio wanajiongopea mchana kweupe.

Askofu Gwajima ni wa lile kundi maarufu la hayati JPM, ni kama vile kaambiwa aongee neno fulani baada ya Mpina kushushuliwa na Musukuma siku chache zilizopita.

Ni kama wanasema bado wapo hivyo wanataka kuonyesha uwepo wao kama wafuasi wa JPM na sera zake. Lakini JK akiwa kiongozi wa kundi la SSH ni bingwa wa mikakati ya kisiasa.
 
Kama hautaki Nigeria nakupa India, Mexico zote hizo ni federalism kama USA lkn bado ni masikini.

Nipe mfano mmoja wa nchi ambayo imejengwa from scratch na demokrasia hii ya leo na ikawa tajiri, isitoshe labda nikuulize kwa nini China imeendelea kuliko India wakati wana Population karibia sawa? India democracy vs China one party dictatorship?
 
Hakuna mahali nimezungumzia federalism kama nguzu muhimu ya maendeleo. Uzi wangu umejikita katika uimara wa TAASISI.
India bado imekuwa na changamoto ya "kuabudu" viongozi, taasisi zake sio thabiti na huru sana kwani zinaathiriwa na siasa za vyama kitaifa na ngazi ya majimbo ambavyo vimehodhiwa na familia au castes fulani.

Mexico ukiondoa tatizo la dawa za kulevya ni nchi nzuri yenye uchumi mkubwa na imepiga maendeleo kuzizidi nchi nyingi kama sio zote barani Africa.

Dictatorship ya China sio ya mtu mmoja ni ya kitaasisi, ya Chama cha Kikomunisti(CCP). Maamuzi mengi yaliyofanyika ya kuufungua uchumi wa China na kufanya mageuzi makubwa mwaka 1980 yalikuwa na msukumo wa kichama. Chama cha Kikomunisti cha China huwa kinaweka tu miongozo ya ujumla katika ngazi ya kitaifa halafu kinaachia maamuzi ya mipango mingine mahususi katika ngazi za wilaya hadi vijiji/mitaa. Miaka ya Karibuni ya Xi ndio kumeibuka cult of personality ya kiongozi mkuu.

Nchi iliyoendelea from the "Scratch" ikiwa na mfumo wa demokrasia ni USA.
USA tangu imepata uhuru wake mpaka leo imekuwa ni taifa la kidemokrasia.
Kama hautaki Nigeria nakupa India, Mexico zote hizo ni federalism kama USA lkn bado ni masikini.

Nipe mfano mmoja wa nchi ambayo imejengwa from scratch na demokrasia hii ya leo na ikawa tajiri, isitoshe labda nikuulize kwa nini China imeendelea kuliko India wakati wana Population karibia sawa? India democracy vs China one party dictatorship?
 
Ni vyema Askofu Gwajima na wote walioguswa na hoja yake leo bungeni kupitia mchango wake kwamba tatizo kubwa letu nchi za Africa ni ukosefu wa dira na mipango ya muda mrefuuu wafahamu hili ambalo Gwajima amekuwa akirudia kulisema sio ukweli bali ni uongo mkubwa, na ni Professorial Rubbish.

Hizo nchi Gwajima anazoona zimeendelea sana hazikuendelea kwa sababu ya kuweka mipango ya miaka 5,10, 20 au 50. Tukichukua mfano wa US, hawa hana hata mpango wa miaka 5 kama sisi. Wao nchi yao ina muendelezo kwa sababu maamuzi makubwa yanaamuliwa katika ngazi za mabunge ya Taifa na majimbo, mahakama na taasisi nyingine nyingine nyingi. Rais anakuwa na nafasi finyu sana ya kufanya maamuzi makubwa kama haunguwi mkono na hivyo vyombo.

Nikirejea maneno ya Aliyekuwa Rais wa Marekani Baraka Obama alipozuru Ghana mwaka 2009 alisema "Africa haihitaji viongozi majabari bali inahitaji Taasisi imara"

Tatizo kubwa la Africa ni Taasisi za nchi kuwa dhaifu.Ukiondoa Africa Kusini na nchi nyingine kwa chache ,kwingine kote Africa Marais wana nguvu na mamlaka kubwa sana ya kuweza kuamua uelekeo wowote nchi zao.
Hili ni tatizo kubwa kwa sababu ukosefu huu wa "checks and balances" unasababisha wengi wao kuyatumia madaraka yao vibaya na kulazimisha ndoto na maono yao badala ya wananchi walio wengi kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na taasisi.

Pia mfumo huu hauchochei uvumbuzi na ubunifu kwa sababu washauri wote na viongozi wa chini wanatenda na kumuambia kiongozi mkuu kile ambacho angependa kusikia badala ya kile ambacho anagepaswa kusikia na hapo ndipo tunapokwama.

Hata tuwe na dira na mipango mirefuuuu ya maendeleo ya miaka 100 au 200 ijayo maendeleo nchini hapa na Africa kwa ujumla hayatakuja kwa kasi kama mfumo wetu wa utawala utabaki wa kuongozwa na viongozi jabiri zaidi kuliko taasisi imara zenye kuchekiana.

#Gwajima Apuuzwe.
Mkuu, umerudia mlemle kwa Gwajima kwa maneno tofauti ila dhana ni ileile
 
Ila kusema ukweli Tanzania imekuwa na dira tangu enzi za Mkapa.
Vision 2025, Mkukuta, Mkurabita nk. Ni mipango labda Gwajima alizama kwenye mambo ya ufufuo.
 
Tatizo la siasa za mitandao ni kundi fulani kulewa mno madaraka halafu wakajiona kama vile hakutatokea siku moja wakaparaganyika. Wanaanza kufanya mambo ya kijinga wakijua watadumu mpaka kifo kiwakute kumbe ndio wanajiongopea mchana kweupe.

Askofu Gwajima ni wa lile kundi maarufu la hayati JPM, ni kama vile kaambiwa aongee neno fulani baada ya Mpina kushushuliwa na Musukuma siku chache zilizopita.

Ni kama wanasema bado wapo hivyo wanataka kuonyesha uwepo wao kama wafuasi wa JPM na sera zake. Lakini JK akiwa kiongozi wa kundi la SSH ni bingwa wa mikakati ya kisiasa.
Nafikiri hata wadanganye vipi ukweli Utakuja shinda tu Kwaio ni swala la muda tu. Hakuna cha bingwa wa siasa wala nini.
 
Kama hautaki Nigeria nakupa India, Mexico zote hizo ni federalism kama USA lkn bado ni masikini.

Nipe mfano mmoja wa nchi ambayo imejengwa from scratch na demokrasia hii ya leo na ikawa tajiri, isitoshe labda nikuulize kwa nini China imeendelea kuliko India wakati wana Population karibia sawa? India democracy vs China one party dictatorship?
Tazama data zako vizuri mkuu. Umaskini kwa kulinganisha na nini?
 
S
Huu mfumo siyo mbaya ila watu ndio hawajui kuutumia, shida ya Afrika siyo mfumo kwani Nigeria wana huo mfumo wa USA ulioungelea copy& paste lkn ndo masikini wa kutupwa, hao Magavana wa States ndo corrupt kuliko hata hapa Bongo, huu mfumo wetu umetumika kwingine na umewasaidia mfano Singapore wana mfumo kama wetu hata Ufaransa wana powerful president, huu mfumo ulitumiwa na nchi ya Uingereza na uliwasaidia pia, na ndio waliouleta hapa, Mauritius ilitawaliwa na Uingereza pia lkn wametuzidi mbali sana.
Japan pia wana mfumo karibia sawa na wa kwetu na umewaendeleza.

Shida ni watu wenyewe na utamaduni wetu na siyo aina ya mfumo, maendeleo ni utamaduni wa watu, mtakopi mifumo yote lkn hakuna kitakachobadilila …
Singapore wameongozwa na chama kimoja toka uhuru ila wako mbali. Tati ni watu wetu, tatizo ni sisi.
 
Hoja zako ni nzuri sana na umeelezea vizuri, lakini pia hoja za Gwajima sio za kupuuza ata kidogo yupo sahihi pia maana swali alilojiuliza kuhusu waafrika na wenye asili ya Africa maendeleo yetu kusuasua na mm nilishajiuliza pia, kwangu mimi nahisi kuondoa mifumo sijui maono binafsi nahisi kuna tatizo la msingi kubwa zaidi kwetu weusi, probably uwezi wetu wa kufikiri sio sawa jumlisha ubinafsi maanza haiwezekani kila sehemu dunia hii penye majority ya watu weusi kuna umasikini compared na weupe
 
Back
Top Bottom